settings icon
share icon
Swali

Je, siku ya Bwana ni?

Jibu


Kifungu "siku ya Bwana" kwa kawaida hubainisha matukio ambayo hufanyika katika mwisho wa historia (Isaya 7:18-25) na mara nyingi karibu kuhusishwa na maneno "siku hiyo." La muhimu katika kuelewa maneno haya ni kwa kumbuka kuwa mara zote hutambua muda wa wakati ambao Mungu binafsi huingilia katika historia, moja kwa moja au kukamilisha baadhi ya kipengele maalum cha mpango wake.

Watu wengi hulinganisha siku ya Bwana na kipindi cha muda au siku maalum ambayo hutokea wakati mapenzi ya Mungu na madhumuni ya dunia yake na kwa ajili ya mwanadamu itatimizwa. Baadhi ya wasomi wanaamini kwamba Siku ya Bwana itakuwa muda refu zaidi kuliko siku moja - kipindi cha muda wakati Kristo atamiliki duniani kote kabla ya kutakasa mbinguni na duniani katika maandalizi kwa ajili ya hali ya milele ya watu wote. Wasomi wengine wanaamini Siku ya Bwana kuwa tukio ghafula wakati Kristo atakaporudi duniani kuwakomboa waumini wake na kutuma wasioamini kwenye laana ya milele.

Kifungu "siku ya Bwana" kimetumika mara kumi na tisa katika Agano la Kale (Isaya 2:12; 13:6, 9; Ezekiel 13:5, 30:3 ; Yoeli 1:15, 2:1,11,31; 3:14; Amosi 5:18,20; Obadia 15; Sefania 1:7,14; Zekaria 14:1, Malaki 4:5 ) na mara nne katika Agano Jipya (Matendo 2:20; 2 Wathesalonike 2: 2, 2 Petro 3:10). Pia limetumika katika vifungu vingine (Ufunuo 6:17; 16:14).

Vifungu vya Agano la Kale vinavyo shughulika na siku ya Bwana mara nyingi hufikisha hisia ya uhalali, ukaribu, na matarajio: "Pigeni kelele za hofu maana siku ya BWANA i karibu a mataifa!" (Isaya 13:6); " Kwa maana siku ile i karibu, siku ile ya BWANA i kariub" (Ezekieli 30:3) ,"Wenyeji wote wa nchi na watetemeke kwa maana siku ya BWANA inakuja. Kwa sababu inakaribia." (Yoeli 2:1); "Makutano makubwa, makutano makubwa wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya BWANA i karibu" (Yoeli 3:14 ); "Nyamaza kimya mbele za Bwana MUNGU! Kwa maana siku ya BWANA i karibu" (Sefania 1:7). Hii ni kwa sababu vifungu vya Agano la Kale vinavyorejelea, siku ya Bwana mara nyingi husema zote utimizo wa sasa na wa mbali, kama ilivyo mengi ya unabii Agano la Kale. Baadhi ya vifungu vya Agano la Kale ambavyo vinarejele siku ya Bwana huelezea hukumu ya kihistoria ambayo tayari imekamilika katika baadhi ya hisia (Isaya 13:6-22; Ezekieli 30:2-19; Yoeli 1:15, 3:14; Amosi 5: 18-20; Sefania 1:14-18), wakati mwingine inahusu hukumu ya Mungu kwamba utafanyika mwishoni mwa umri (Yoeli 2:30-32; Zekaria 14:1, Malaki 4:1, 5).

Agano la Jipya huita hiyo siku " ghadhabu" siku ya "kuonekaniwa" na "siku kuu ya Mwenyezi Mungu" (Ufunuo 16:14) na inahusu utimiza wa siku zijazo wakati hasira ya Mungu itamwagiwa juu ya Wasraeli wasioamini (Isaya 22; Yeremia 30:1-17; Yoeli 1-2; Amosi 5; Sefania 1) na juu ya dunia isioamini (Ezekieli 38-39; Zakaria 1 ). Maandiko yanaonyesha kwamba "siku ya Bwana" itakuja haraka, kama mwizi katika usiku (Sefania 1:14-15; 2 Wathesalonike 2:2), na kwa hiyo Wakristo wanapaswa kuwa waangalifu na tayari kwa ujio wa Kristo wakati wowote.

Licha ya kuwa wakati wa hukumu, pia itakuwa wakati wa wokovu kwa vile Mungu atawakomboa mabaki ya Israeli, kutimiza ahadi yake kwamba "wote wa Israeli wataokolewa" (Warumi 11:26), mwenye kusamehe dhambi zao na kurejesha wake watu waliochaguliwa katika ardhi ya ahadi kwa Ibrahimu (Isaya 10:27; Yeremia 30:19-31, 40; Mika 4; Zakaria 13). Matokeo ya mwisho ya siku ya Bwana itakuwa "Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu tiatashushwa naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo" (Isaya 2:17). Mwisho wa kutimiza unabii kuhusu siku ya Bwana utakuja mwishoni mwa historia wakati Mungu, kwa uwezo wa ajabu, ataadhibu dhambi na kutimiza ahadi zake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, siku ya Bwana ni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries