Swali
Biblia inasema nini kuhusu tabia ya Kikristo?
Jibu
Tunapozungumza kuhusu tabia ya “Kikristo”, tunazungumza kuhusu tabia ya wale ambao wamemkubali Yesu Kristo kwa imani, kama mwokozi wao na kwa hivyo Roho Mtakatifu anakaa ndani yao (Warumi 8:9), na kuwawezesha kutumikia Mungu. Mifano ya tabia za Kikristo imefumwa katika maandiko yote. Kwa hakika, mwokozi wetu mwenyewe alizungumza kwa kina kuhusu jinsi tunavyopaswa kuishi na wengine, marafiki na maadui. Zaidi ya hayo, hata hivyo, maisha Aliyoishi, yalisisitiza upendo na huruma kwa waliopotea, yanatoa mfano kamili wa jinsi tabia ya Kikristo inapaswa kuonekana.
Wakristo ni “kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu ili tupate kutenda matendo mema” (Waefeso 2:10). Na maneno haya manne “tupate kutenda matendo mema” ni ufupisho wa tabia inayomtukuza Mungu na kumfanya Kristo kuwa halisi kwa wengine. Ni kweli kwamba kuna vizuizi katika maisha yetu ya kila siku ambazo hutatiza akili zetu na kuzuia maendeleo yetu ya kiroho, lakini ikiwa tu tu tunaviruhusu. Hata hivyo, wakristo wanahimizwa kuishi maisha ambayo ni “takatifu na yanampendeza Mungu” (Warumi 12:1), na tabia ya kielelezo ya Kikristo ambayo inatuwezesha kujitoa kikamilifu katika kumtumikia Bwana inawezekana tunapowezeshwa na Roho Mtakatifu anayetuwezesha kufanya mapenzi ya Baba (Warumi 8:9). “Kwa kuwa macho ya Bwana hukimbiakimbia duniani kote ili kujionyesha mwenye nguvu kwa ajili ya wale ambao mioyo yao inamtegemea kwa ukamilifu” ( 2 Mambo ya Nyakati 16:9).
Wakristo ni watu teule, watu walio milki ya Mungu, walioitwa ili kutangaza sifa zake (1 Petro 2:9). Ili “kutangaza sifa zake ,” basi, ni muhimu kutumia wakati katika Nelo Lake, sio tu ili tuweze kujifunza jinsi ya kuishi katika mtindo wa Kikristo, bali pia ili tuweze kupigana vota dhidi ya hila za shetani. Kama vile mtume Paulo alivyodokeza, bila ujuzi huu wa Biblia tutashawishiwa na kila fundisho jipya linalokuja, na pia kuangukia “hila za watu, kwa ujanja, kwa kufuata njia zao za udanganyifu” (Waefeso 4:14). Hata hivyo, ujuzi pekee hautoshi, tumeitwa kufanya zaidi ya kujua na kuamini. Wakristo wanapaswa kuwa “watendaji wa Neno” (Yakobo 1:22). Kama vile mtume Yakobo anavyotujulisha, tunajidanganya ikiwa tunafikiri kwamba sisi ni wa kiroho kwa kusikia neno tu. Kusikia sio saw ana kutenda. “Imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa” (Yakobo 2:17, 26). Imani lazima ionyeshwe kwa matendo.
“Matendo” yanayomtukuza Baba wetu wa mbinguni ni yale yanayozaa matunda (Yohana 15:8). Hivi ndivyo , kwa kweli jinsi tunavyoonyesha kuwa sisi ni wanafunzi wake. Kwa hakika, tunda la Roho-Upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi (Wagalatia 5:22-23)- yapaswa kuwa alama ya tabia ya Mkristo, hasa upendo. Ilhali wakati mwingine tunawadharau wasioamini au wale ambao mitindo yao haiambatani na imani yetu ya Kikristo, hapa ndipo maisha ya Kikristo yanaweza kuwa na changamoto. Ni rahisi kuwaonyesha upendo walio na mitindo kama yetu. Sio rahisi kila mara kuwa mkarimu kwa wale wanaodhihaki imani yetu, wanaomdharau Mwokozi wetu, au wanaofanyia mzaha taasisi ambazo Wakristo wanaamini kuwa ni takatifu. Hata hivyo Kristo alitufunza kuwapenda maadui wetu na kuwaombea wanaotutesa. Kumbuka jinsi alivyoshughulika na mwanamke aliyefumaniwa akizini. Waliomkuta akizini walitaka afe; Mwokozi wetu alionyesha huruma ingawa yeye ndiye amabye angekufa kwa ajili ya tabia yake (na tabia yetu) ya dhambi (Yohana 8:11). Yesu Kristo alikuja duniani kuwaokoa wenye dhambi (I Timotheo 1:15), sio kuwahukumu (Yohana 3:17), na ikiwa Kristo hakuja kuwahukumu wenye dhambi, Wakristo pia hawafai kuwahukumu.
Tabia ya Kikristo ni pamoja na kutii wito wa Yesu wa kuwa mashahidi Wake “hadi kiisho ya dunia” (Matendo 1:8). Tunapaswa kushiriki injili ambayo Paulo alifafanua kama kifo, kuzikwa na ufufuo wa Kristo (1 Wakorintho 15:1-4). Uhalali wa ushuhuda wetu umo katika jinsi tunavyoiishi maisha yetu. Katika nusu ya pili ya Waefeso ( vifungu 4-6) Paulo anazungumzia tabia ya Kikristo ambayo inaweza kufupishwa katika maneno haya machache: “ Mfuateni Mungu…mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu” (Waefeso 5:1-2).
Paulo aliwahimiza Warumi “itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai” (Warumi 12:1). Hiki hatimaye ndicho kiini cha tabia ya kweli ya Kikristo- kusalimisha mioyo yetu na kutoa miili yetu kwa Kristo ili aweze kuendeleza kazi ya Mungu kupitia kwetu. Tunapaswa kuwa mianga ya nuru katika ulimwengu wenye giza, huku tukitimia karama zetu za kiroho kuendeleza ufalme Wake. Ni kuishi hapa duniani jinsi Yesu alivyoishi alipokuwa hapa. Pia inamaanisha kushi kumpendeza Mtu mmoja-Mungu. Tunafanya hivi tunapokaa katika Neno Lake na kuishi kulingana na Neno Lake, jinsi tunavyowezeshwa na Roho Wake, kama vile Mwokozi wetu alivyofanya hadi alipovuta pumzi Yake ya mwisho. Alipokuwa akifa msalabani, Kristo aliwaangalia wauwaji Wake na kumwomba Baba yake awasamehe (Luka 23:34). Yesu alikuwa anafanya zaidi ya kutimiza unabii na “kuwaombea wakosaji” (Isaya 53:12) alikuwa akifanya yale aliyoubiri (Luka 6:27-28).
English
Biblia inasema nini kuhusu tabia ya Kikristo?