Swali
Kuna makosa gani ya kutazama ponografia, ikiwa simtamani mtu huyo?
Jibu
Kwanza, ni vizuri kutambua kwamba tamaa ni dhambi (Mathayo 5:28; 1 Yohana 2:16). Hata hivyo, ni muhimu pia kuwa waaminifu kwetu wenyewe. Picha za kingono na ashiki zote zinakusudiwa kuchochea tamaa moyoni. Sababu pekee ya ponografia ni kwamba watu wengi wakubali mawazo ashiki. Haiwezekani kutazama ponografia na ukose kujaribiwa na tamaa-tamaa ya kutaka kuwa na kitu au kufanya kitu ambacho kinapinga mapenzi ya Mungu. Hata kama mtu hatamani mtu mwingine katika picha au sinema mtu huyo anazidisha tamaa zinazopingana na utakatifu wa Mungu. Kutazama ponografia ni dhambi kila wakati.
Tunawajibika kulinda mioyo yetu dhidi ya tamaa (Mithali 4:23). Hili ni muhimu kwa sababu kulegeza ulinzi wetu kunaweza sababisha maafa: “Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.” (Yakobo 1:14-15).
Kujaribu kufupisha ufafanuzi wa tamaa au kuweka tofauti isiyostahili kuhusu kitu cha tamaa ni njia ya kufanya dhambi kuonekana kukubalika zaidi. Lazima tukumbuke udanganyifu wa dhambi (Waebrania 3:13). Mwili husema, “Ninahitaji hiki,” na Mungu anaseama, “La, sio bora kwako.” Huo ndio wakati Shetani anaingilia na kusema, “Labda tunaweza kuwa na maelewano.”
Ikiwa tunatamani kitu ambacho Mungu ametukataza, basi tuna tamaa. Yesu alisema kwamba tamaa moyoni ni dhambi machoni pa Mungu sawa na tendo halisi la uzinzi (Mathayo 5:27-28). Mungu amebariki muungano wa mume na mke (Wimbo 5:1), na Ametoa maonyo makali dhidi ya ngono nje ya ndoa (k.m., Waebrania 13:4). Hakuna mtu ana haki ya kuutazama uchi wa mtu mwingine-au kumwangalia mtu aliyevalia nguo kwa kumtamani-isipokuwa ameolewa na mtu huyo.
Ni vigumu kuishi kwa utakatifu katika ulimwengu mchafu, na sisi sote tunapambana na suala hili. Tunahitaji silaha za Mungu tunapopigana vita hivi (Waefeso 6:10-18). Tunapaswa kufuata mfano wa Yusufu, ambaye, wakati alikabiliwa na majaribu alitoroka (Mwanzo 39:12; taz. 2 Timotheo 2:22). Tunapaswa kujitolea kwa utakatifu kama vile Ayubu alifanya: “Nimefanya agano na macho yangu yasimtazame msichana kwa kumtamani” (Ayubu 31:1). “Bali jivikeni Bwana Yesu Kristo, wala msifikiri jinsi mtakavyotimiza tamaa za miili yenu yenye asili ya dhambi” (Warumi 13:14).
English
Kuna makosa gani ya kutazama ponografia, ikiwa simtamani mtu huyo?