settings icon
share icon
Swali

Teolojia ya matendo ya kibiblia ni nini?

Jibu


Mungu aliwaumba binadamu ili wafanye kazi. Agizo la kwanza ambalo Mungu alimpa Adamu lilikuwa ni la kufanya kazi, kutunza bustani ya Edeni (Mwanzo 2:15). Kwa bahati mbaya, katika karne kadhaa, neno kazi limepata maana mbaya. Mara nyingi tunaiona kazi kuwa shughuli ngumu au isiyofurahisha ambayo tunalazimika kufanya. Hata hivyo, kazi ni kushiriki katika juhudi za kimwili au kiakili ili kufikia lengo au matokeo. Kuinua kijiko mdomoni mwa mtu ni kazi. Kutunga wimbo au shairi ili kuelezea yaliyo moyoni ni kazi kwa sababu juhudi kama hizo zinafanywa ili kufikia lengo au matokeo. Katika utamaduni wa magharibi, neno kazi mara nyingi linahusishwa zaidi na taaluma au njia ya kupata riziki, kama vile “ameenda kazini leo”, maana yake, “ameajiriwa katika kazi na atatumia siku nzima kutekeleza majuku yake aliyopewa”.

Kazi ilitolewa kabla ya dhambi kuingia ulimwenguni na kwa hivyo ni sehemu ya uumbaji kamili wa Mungu. Kazi haikuwa matokeo ya kuanguka; kuanguka kuliifanya kazi iwe ngumu zaidi (Mwanzo 3:17-19). Kutunza bustani ya Edeni ilipangwa kuwa kazi ya kufurahisha na yenye thawabu kwa Adamu. Angependa kutunza bustani na angeiona ya kuridhisha na ya maana. Mungu alimuumba Mwanadamu apende kazi ili Mungu aweze kufurahia kumtazama, kama vile wazazi wanavyofurahia kuona watoto wao wakipata ujuzi mpya au kuunda mradi wa sanaa.

Kazi husaidia kutimiza mahitaji na kusudu la mwanadamu. Tofauti na wanyama, ambao wanahamasishwa na asili na mahitaji ya kimwili, binadamu hufanya kazi kutokana na motisha ya juu. Mbali na mahitaji yetu ya kimwili ndio tuishi, tuna hamu ya kuwa na maisha ya maana. Tunahitaji sababu ya kuamka asubuhi. Tunahitaji kujua ni kwa nini tunaishi na kama maisha yana kusudi. Kazi ilipangwa kwa kehesmu kutekeleza mahitaji hayo.

Kazi ni njia tunayokidhi mahitaji yetu ya kimsingi na kusaidia wengine ambao huenda hawawezi kufanya kazi (Waefeso 4:28). Uzembe, tabia ya kukwepa kazi, vinakemewa katika maandiko (Mithali 13:4;21:25). Tunapaswa kukumbatia kazi ambayo Mungu ametupa kufanya na kutoa shukrani kwake kwamba tuna uwezo wa kujikimu sisi wenyewe na familia zetu. Wakolosai 3:23 inasema, “Lolote mfanyalo, fanyeni kwa moyo kama watu wanaomtumikia Bwana, na si wanadamu.” Mungu alianzisha fungu la kumi katika Agano la kale kama ukumbusho kwa watu kwamba ni Mungu ambaye alikuwa akibariki kazi ya mikono yao (Mambo ya Walawi 27:30; Hesabu 18:28-29).

Watu ambao waliotekeleza kutunza familia zao walikemewa na kanisa la kwanza (1 Timotheo 5:8). Paulo alitoa maagizo kwamba, wale wanaokataa kufanya kazi wasiruhusiwe kula (2 Wathesalonike 3:10). Pia aliyakumbusha makanisa kwamba, ingawa alikuwa na haki ya kupata riziki yake kutokana na huduma yake kwao, pia alifanya kazi ya kutengeneza mahema ili kujikidhi yeye mwenyewe (Matendo 18:3; 20:34; 1 Wathesalonike 2:9).

Yesu alifanya kazi. Ingeeleweka kama Mwana wa Mungu angetumia wakati wake wote hekaluni, akifundisha maandiko. Lakini, kwa miaka thelathini ya kwanza ya maisha yake, Yesu alifanya kazi pamoja na baba yake wa kidunia, Yusufu, kama seremala (Marko 6:3; Luke 2:51-52).

Teolojia ya Kibiblia ya kazi ni kwamba kazi ilibuniwa na Mungu kama jukumu la binadamu duniani. Ni njia ya kudumisha maisha yetu na kufanya ufichuzi kuhusu ulimwengu wa Mungu. Tuliumbwa kwa mfano wa Mungu (Mwanzo 1:27), na Mungu anafanya kazi (Zaburi 19:1; Yohana 5:19). Kazi yake ni bunifu, yenye kusudi, na kamili; inamfurahisha na inatufaa (Zaburi 92:4). Siku moja, katika mbingu mpya na dunia mpya, kazi itarejeshwa katika hali yake ya kabla ya kuanguka- itakuwa ya kutosheleza tama zetu na kuwa baraka kwa kila mtu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Teolojia ya matendo ya kibiblia ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries