Swali
Theolojia ya msalaba ni nini?
Jibu
Theolojia ya msalaba, ni neno lililotungwa na mwanatheolojia Mjerumani Martin Luther kuashiria ile imani kwamba msalaba ndio chanzo pekee cha maarifa ya kiroho kuhusu Mungu ni nani na jinsi anavyookoa. Ni katika msalaba pekee ambapo mwanadamu aliyeanguka anapata ufahamu kwamba ni kupitia kwa Roho Mtakatifu kuishi ndani yake katika kukombolewa (1 Wakorintho 12:13; Warumi 8:9; Waefeso 1:13-14). Theolojia ya msalaba inalinganishwa na theolojia ya utukufu, ambayo inazingatia uwezo na akili za binadamu. Luther alitumia neno theolojia crucis kwa mara ya kwanza katika Mdahalo wa Heidelberg wa 1518, ambapo alitetea mafundisho ya mageuzi ya upotovu wa mwanadamu na utumwa wa mapenzi ya dhambi.
Tofauti ya msingi kati ya theolojia ya msalaba na theolojia ya utukufu ni uwezo au upungufu wa mwanadamu kujitetea mbele ya Mungu mtakatifu. Mtaalam wa theolojia ya msalaba anaona kwamba ukweli wa kibiblia kwamba mwanadamu hawezi kupata haki kwa jitihada zake, hawezi kuongeza haki iliyopatikana kwa kafara ya Yesu msalabani, na kwamba chanzo pekee cha haki ya mwanadamu kinatoka nje ya nafsi zetu, hakipaswi kuvunjwa. Mtaalam wa theolojia ya msalaba anakubaliana kabisa na Mtume Paulo kuhusu hali ya kibinadamu: “Kwa maana ninafahamu kwamba hakuna jema lolote likaalo ndani yangu, yaani, katika asili yangu ya dhambi. Kwa kuwa nina shauku ya kutenda lililo jema, lakini siwezi kulitenda” (Warumi 7:18). Mtaalam wa theolojia ya msalaba anapinga wazo kwamba mwanadamu anaweza kufikia haki kwa kiwango chochote kwa kuzingatia matendo ya sheria, lakini anapokea wokovu na utakaso kwa neema pekee (Warumi 3:20; Waefeso 2:8-9).
Kwa upande mwingine, wanatheolojia ya utukufu huona kwamba kuna wema ndani ya binadamu na wanawaelezea kama wenye uwezo wa kufanya yaliyo mema. Wanaamini kwamba, licha ya kuanguka, bado kuna uwezo wa kuchagua mema badala ya maovu na hivyo watachagua mema. La muhimu zaidi, Theolojia ya utukufu inaamini kwamba binadamu hawawezi kukokolewa bila kushiriki au kushirikiana na haki inayopeanwa na Mungu. Huu ni mjadala wa matendo dhidi ya imani ambao umekuwa ukichochea kwa muda mrefu kutokana na kuelewa vibaya wa baadhi ya mistari katika kitabu cha Yakobo. Yakobo 2:17-18 inatafsiriwa kumaanisha kwamba tunahesabiwa haki kwa matendo yetu, wakati Yakobo anasema kwamba wale ambao wamehesabiwa haki kwa imani katika kazi ya Kristo msalabani watazaa matendo mema kama ushahidi wa wongofu wa kweli, si kwamba wongofu unapatikana kwa matendo mema.
Ni vyema kutambua kwamba theolojia ya msalaba si wazo la hisia kwamba Yesu anafanywa kuwa wa kupendeza zaidi kwetu kwa kujitambulisha na majaribu yetu na dhiki zetu. Ingawa Yesu bila shaka anajitambulisha na mateso yetu, mateso yetu hayafanywi kuwa ya heshima kwa sababu hiyo. Mateso yetu ni matokeo ya kuanguka kwa binadamu katika dhambi, huku mateso ya Yesu yalikuwa ya Mwanakondoo asiye na hatia aliyeuawa kwa sababu ya dhambi ya wengine, na sio dhambi zake mwenyewe. Theolojia ya msalaba sio kujitambulisha na kuteseka kwake kupitia mateso yetu wenyewe, ambayo hupungua ikilinganishwa na yale ambayo yeye alipitia. Mwishowe, Yesu aliteseka na kufa kwa sababu hakuna mtu aliyehusishwa Naye. Watu walipisa sauti “Msulubishe!” Mmoja wa wanafunzi wake alimsaliti, mwingine akamkana mara tatu, na wengine wakamwacha na kukimbia. Alikufa peke yake, akaachwa hata na Mungu. Kwa hivyo kujaribu kuungana Naye katika mateso yake ni kudunisha dhabihu yake na kuinua mateso yetu kwa kiwango ambacho hakikusudiwa kamwe na theolojia ya msalaba ambayo Luther alidai.
English
Theolojia ya msalaba ni nini?