settings icon
share icon
Swali

Je, toba ni badiliko la nia au kugeuka kutoka kwa dhambi?

Jibu


Toba ni badiliko la fikra, si kuacha dhambi. Neno la Kigiriki linalotafsiriwa “toba” ni metanoia, na maana yake ni “badiliko la nia.” Katika matumizi ya kawaida, hata hivyo, mara nyingi tunazungumza juu ya toba kama “kuacha dhambi.” Kuna sababu mwafaka ya hili.

Toba mara nyingi huhusishwa na wokovu katika Maandiko. Ni nini hufanyika wakati Roho Mtakatifu anapoanza kazi Yake ya kumleta mtu katika wokovu? Roho humpa mwenye dhambi ufahamu wa kibinafsi na usadikisho usiokosea kwamba mambo ya hakika kuhusu hali yake ya kiroho ni ya kweli. Mambo hayo ni dhambi yake binafsi, adhabu ya milele anayostahili kwa ajili ya dhambi yake, asili ya kuteseka kwa Yesu kwa ajili ya dhambi yake, na hitaji la kumwamini Yesu ili kumwokoa kutoka katika dhambi yake, na hitaji la kumwamini Yesu ili kumwokoa kutoka katika dhambi yake. Kwa sabau ya kazi hiyo ya kuhukumu ya Roho Mtakatifu (Yohana 16:8), mwenye dhambi hutubu-anabadili mawazo yake-kuhusu dhambi, Mwokozi, na wokovu.

Wakati mtu anayetubu anabadilisha mawazo yake kuhusu dhambi, badiliko hilo la nia kwa kawaida husababisha kutoka katika dhambi. Dhambi haitamaniki tena au kufurahisha, kwa sababu dhambi huleta hukumu. Mtenda dhambi anayetubu huanza kuchukia matendo yake maovu ya hapo kale. Na anaanza kutafuta njia za kurekebisha tabia yake (soma Luka 19:8). Kwa hivyo, hatimaye, matokeoya mabadiliko ya nia kuhusu dhambi ni matendo mema. Mwenye dhambi hugeuka kutoka kwa dhambi hadi kwa imani katika Mwokozi, na imani hiyo inaonyeshwa kwa matendo (ona Yakobo 2:17).

Badiliko la nia (toba) sio sawa kabisa na kuacha vitendo vya dhambi na utendaji unaoonekana wa matendo mema, lakini moja huelekeza kwa lingine. Katika njia hii, toba inahusiana na kuacha dhambi. Watu wanaposema juu ya toba kuwa ni kugeuka kutoka kwa dhambi (badala ya badiliko la mawazo), wanatumia tamathali ya usemi wa kimajazi. Katika kimajazi, jina la dhana fulani hubadilishwa na neno lililopendekezwa na lile la asili.

Kimajazi ni usemi wa kawaida sana katika lugha ya kila siku. Kwa mfano repoti za habari zinazoanza, “Brazili imetoa taafira leo,” zinatumia kimajazi, kwa kuwa jina la nchi hiyo linatajwa badala ya jina la serikali au kiongozi ambaye alitoa taarifa hiyo.

Katika Biblia tunaweza kuona mifano mingine ya kimajazi, katika Marko 9:17 baba anasema kwamba mwanawe ana “pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea.” Pepo mchafu mwenyewe sio bubu. Pepo mchafu anamfanya mwana kuwa bubu. Pepo amapewa jina kulingana na mathara anayosababisha: mtoto bubu. Majazi hapa inachukua nafasi ya chanzo na athari. Vile vile kutumia neno toba kumaanisha “kugeuka kutoka katika dhambi” linabadilisha chanzo kwa athari. Chanzo ni toba, badiliko la nia, athari ni kugeuka kutoka dhambini. Neno linabadilishwa na dhana linalohusiana. Hiyo ni majazi.

Kwa mukhtasari toba ni badiliko la nia. Lakini ufahamu kamili wa kibiblia humaanisha zaidi ya hayo. Katika uhusiano na wokovu, toba ni badiliko la nia kutoka kukumbatia dhambi hadi kukataa dhambi na kutoka kwa kumkataa Kristo hadi imani katika Kristo. Toba kama hiyo ni kitu ambacho Mungu pekee ndiye anayewezesha (Yohana 6:44; Matendo 11:18; 2 Timotheo 2:25). Kwa hivyo, toba ya kweli ya kibiblia itasababisha mabadiliko ya tabia kila wakati. Labda si mora moja, lakini bila shaka ni hatua kwa hatua.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, toba ni badiliko la nia au kugeuka kutoka kwa dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries