Swali
Agano la Kale dhidi ya Agano Jipya – kuna tofauti gani?
Jibu
Huku Biblia ikiwa ni kitabu kimoja, kuna tofauti kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Kwa njia nyingi, zinakamilishana. Agano la Kale ni la msingi, na Agano Jipya lajijenga kwa huo msingi na ufunuo zaidi kutoka kwa Mungu. Agano la Kale laanzisha kanuni ambazo zinaonekana kuonyesha ukweli wa Agano Jipya. Agano la Kale lina unabii mwingi ambao unatimia katika Agano Jipya. Agano la kale linatoa historia ya watu i>; Lengo la Agano Jipya ni juu ya Mtu i>. Agano la Kale linaonyesha ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi (kwa kiza cha neema yake) na Agano Jipya linaonyesha neema ya Mungu kwa ajili ya wenye dhambi (kwa kiza cha ghadhabu yake).
Agano la Kale linatabiria Masihi (ona Isaya 53), na Agano Jipya linamdhihirisha masih kuwa yupo ( Yohana 4:25-26). Agano la Kale lakumbukumbu utoaji wa Sheria ya Mungu, na Agano Jipya laonyesha jinsi Yesu Masiya alivyotimiza sheria (Mathayo 5:17, Waebrania 10:9). Katika Agano la Kale, adhabu ya Mungu hasa ni kwa watu wake wateule, Wayahudi; katika Agano Jipya, adhabu ya Mungu hasa ni kwa kanisa lake (Mathayo 16:18). Baraka za kimwili zilizo ahidiwa katika Agano la Kale (Kumbukumbu 29:9) linatoa njia ya baraka za kiroho chini ya Mkataba ya Agano Jipya (Waefeso 1:3).
Unabii wa Agano la Kale kuhusiana na kuja kwa Kristo, ingawa ni wa kina, una kiasi fulani cha utata ambao umerekebishwa katika Agano Jipya. Kwa mfano, Nabii Isaya alisema ya kifo cha Masihi (Isaya 53) na kuanzishwa kwa ufalme wa Masihi (Isaya 26) huku hakuna dalili ya mwenendo wa matukio mawili - hakuna mwanga kwamba mateso na ujenzi wa ufalme utatenganishwa na milenia. Katika Agano Jipya, inakuwa wazi kuwa Masiya ako na ujio aina mbili i>: katika ule wa kwanza aliteseka na akafa (na kufufuka tena), na katika wa pili Yeye ataimarisha ufalme wake.
Kwa sababu ya ufunuo wa Mungu katika maandiko ni endelefu, Agano Jipya huleta katika lengo kali la kanuni kwamba walikuwa kuletwa katika Agano la Kale. Kitabu cha Waebrania kinaeleza jinsi Yesu kweli ni Kuhani Mkuu na jinsi kafara yake moja kuu ni nafasi ya sadaka zote za awali, ambayo ilikuwa kivuli cha yatakayo kuja. Pasaka ya Agano la Kale (Ezra 6:20) inakuwa Mwana-kondoo wa Mungu katika Agano Jipya (Yohana 1:29). Agano la Kale inatupa sheria. Agano Jipya linafafanua kwamba sheria ilikuwa na maana ya kuonyesha watu mahitaji yao ya wokovu na haikukusudiwa kuwa njia ya wokovu (Warumi 3:19).
Agano la Kale liliona Adamu amepotelewa na peponi na Agano Jipya linaonyesha jinsi peponi inapatikana kupitia Adamu wa pili (Kristo). Agano la Kale lasema kwamba mwanadamu alikuwa ametengwa na Mungu kwa njia ya dhambi (Mwanzo 3), na Agano Jipya linasema kuwa mwanadamu anaweza kurejeshwa katika uhusiano wake na Mungu (Warumi 3-6). Agano la Kale lilitabiri maisha Masihi. Injili imerekodi maisha ya Yesu, na Nyaraka hutafsiri maisha yake na jinsi sisi huitikia yote ambayo amefanya.
Kwa muhtasari, Agano la Kale huweka msingi wa kuja kwa Masihi ambaye atatoa nafsi yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi za ulimwengu (1 Yohana 2:2). Agano Jipya limenakili kumbukumbu ya huduma ya Yesu Kristo na kisha inaonekana kutizama nyuma juu ya kile alichofanya na jinsi sisi tunastahili kuhitikia. Agano zote mbili zatangaza huyo Mungu mtakatifu, na wa huruma, na hakia ambaye Analaani dhambi bali atamani kuwaokoa wenye dhambi kwa njia ya sadaka ya upatanisho. Katika Maagano yote mawili, Mungu hujifunua kwetu na inatuonyesha jinsi sisi tunastahili kuja kwake kwa njia ya imani (Mwanzo 15:6; Waefeso 2:8).
English
Agano la Kale dhidi ya Agano Jipya – kuna tofauti gani?