settings icon
share icon
Swali

Kuna tofauti gani kati ya vipaji na karama za kiroho?

Jibu


Kuna ufanano na tofauti kati ya vipaji na karama za kiroho. zote ni zawadi kutoka kwa Mungu. Zote hukua katika ufanisi na matumizi. Zote zimenuiwa kutumika kwa niaba ya zingine, si kwa ajili ya ubinafsi. Wakorintho wa kwanza 12:7 inasema kwamba karama za kiroho zimetolewa kwa faida ya wengine na si yetu wenyewe. Kama amri mbili kuu husungumzia kumpenda Mungu na wengine, kinachofuata ni kuwa lazima mtu atumie vipaji vyake kwa ajili ya lengo hilo. Lakini ni kwa nani na ni wakati gani vipaji vya kiroho wanapewa hutofautiana. Mtu (bila kujali imani yake katika Mungu au katika Kristo) amepewa kipawa cha asili kama matokeo ya mchanganyiko wa jenetiki (baadhi na uwezo wa asili katika muziki, sanaa, au hisabati) na mazingira (alikulia katika familia ya muziki itachangia katika kuendeleza kipaji kwa ajili ya muziki), au kwa sababu Mungu anataka kuwapatia baadhi ya watu vipaji fulani (kwa mfano, Bazeleel katika Kutoka 31:1-6). Karama za kiroho ni kwa ajili ya waumini wote kwa Roho Mtakatifu (Warumi 12:3, 6) wakati wanaweka imani yao katika Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zao. Wakati huo huo, Roho Mtakatifu anampa muumini karama za kiroho Yeye anatamani muumini kuwa nayo (1 Wakorintho 12:11).

Warumi 12:3-8 inaorodhesha vipawa vya kiroho kama ifuatavyo: unabii, kuwahudumia wengine (kwa maana ya ujumla), mafundisho, kuonya, ukarimu, uongozi, na kuonyesha huruma. Wakorintho wa kwanza 12:8-11 inaorodhesha karama kama neno la hekima (uwezo wa kuwasiliana kwa hekima kiroho), neno la maarifa ( uwezo wa kuwasiliana ukweli wa vitendo ), Imani (kumtegemea Mungu kusio kwa kawaida), matendo ya miujiza, unabii, kupambanua roho, lugha (uwezo wa kusema lugha ambayo mtu hakuisomea), na tafsiri ya lugha. Orodha ya tatu ni inapatikana katika Waefeso 4:10-12, ambayo inazungumzia Mungu anapatia kanisa lake; Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na walimu. Pia kuna suala kuwa kuna vipaji vingapi vya kiroho, kama vile orodha hakuna ya pili inavyotaja kuwa viko sawa. Pia inawezekana kwamba orodha ya Biblia si kamilifu, kwamba kuna zawadi ya ziada ya kiroho zaidi ndio Biblia inataja.

Wakati mtu anaweza kuendeleza vipaji vyake na baadaye kuelekeza taaluma yake au jambo alipendalo pamoja na mistari hiio, vipawa vya kiroho vilipeanwa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya kulijenga kanisa la Kristo. Kwa kuwa, Wakristo wote wanfaa kuchukua sehemu ya kazi yetu katika kueneza Injili ya Kristo. Wote wameitwa na kukingwa na vifaa kushiriki katika "kazi ya huduma" (Waefeso 4:12). Wote wamepewa vipawa ili waweze kuchangia kwa huduma ya Kristo kwa shukrani kwa yale yote amefanya kwa ajili yao. Kwa kufanya hivyo, wao pia hupata ukamilifu katika maisha kupitia kwa kazi yao kwa ajili ya Kristo. Ni kazi ya viongozi wa Kanisa kusaidia kuwajenga watakatifu ili waweze kuimarika zaidi kwa ajili ya huduma ambayo Mungu amewaita. Matokeo yaliyokusudiwa ya vipawa vya kiroho ni kwamba kanisa zima liweze kukua, kuwa na nguvu kwa pamoja kuwaletera mjumbe wa mwili wa Kristo pamoja.

Kwa kufupisha tofauti kati ya karama za kiroho na vipaji: 1) Kipaji ni matokeo ya jenetiki / au mafunzo, huku karama ya kiroho ni matokeo ya nguvu ya Roho Mtakatifu . 2) Kipaji kinaweza kumilikiwa na mtu yeyote, awe Mkristo au kafiri, huku karama ya kiroho inamilikiwa na Wakristo pekee. 3) Wakati vipaji na karama za kiroho zinafaa kutumika kwa ajili ya utukufu wa Mungu na kuhudumia wengine, karama za kiroho ni kulenga majukumu haya , huku kipaji kinaweza kutumika kabisa kwa ajili ya malengo yasiyo ya kiroho.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuna tofauti gani kati ya vipaji na karama za kiroho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries