Swali
Je, ninawezaje kujifunza kutumaini uaminifu wa Mungu?
Jibu
Sehemu nyingi katika Maandiko zinasifu uaminifu wa Mungu. Maombolezo 3:22-23 inasema, “Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii, kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe. Ni mpya kila asubuhi, uaminifu wako ni mkuu.” Hivyo, uaminifu ni nini?
Neno la Kiebrania lililotafsiriwa “uaminifu” linamaanisha “uthabiti, imara, uaminifu.” Kinyume cha kuwa mwaminifu ni kubadilika kila wakati au kuwa dhaifu. Zaburi 119:89-90 inasema, “Ee BWANA, neno lako lasimama Imara mbinguni hata milele. Uaminifu wako upo kizazi baada ya kizazi, Umeiweka nchi, nayo inakaa.” Hapa uaminifu umewekwa sawa na neno la Mungu. Mungu anaongea ukweli usio na mwisho. Ikiwa Mungu aliongea kitu miaka elfu moja iliyopita, bado kinasimama. Ni mwaminifu kwa Neno Lake, kwa sababu Neno Lake ni dhihirisho la tabia Yake. Ahadi alizotoa bado zinashikilia kuwa ukweli kwa sababu habadiliki (Malaki 3:6). Tunaona hili limedhihirishwa kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu katika wanandoa waliooana kwa miaka mingi. Wakati mke analala katika kitanda chake cha kifo, bwanake anaketi karibu naye huku akiwa amemshika mkono wake. Hawezi kumwacha, hata kama hawezi kumtambua. Anabaki kuwa mwaminifu kwa ahadi alizotoa kwake. Kwa njia hiyo hiyo, Mungu anabaki kuwa mwaminifu kwa ahadi Zake, hata kama mara kwa mara sisi sio waaminifu Kwake (2 Timotheo 2:13).
Tunapata kuamini tabia ya mtu kwa kumjua mtu huyo vyema. Hatuwezi mkabidhi mtu mgeni akaunti yetu ya benki ambaye tumekutana naye kwa foleni katika ofisi ya kuchukua barua—hatuna uzoefu naye. Hatujui tabia yake. Kabla ya kumjua Mungu, tunaogopa kumwamini Yeye. Bado hatumjui Yeye ni nani au anaweza kufanya nini. Tunajifunza kumwamini Mungu kwa kujua tabia Yake. Kuna njia tatu tunaweza kumjua Yeye: kusoma Neno Lake, kukagua kazi Zake katika maisha yetu, na kujifunza kufuata sauti Yake.
Tunaposoma Neno la Mungu, mfumo unajitokeza. Tunajifunza kwamba Mungu habadiliki kamwe na hadanganyi kamwe (Hesabu 23:19; 1 Samweli 15:29). Tunajifunza kupitia Maandiko kwamba hajawai kushindwa hapo awali (Isaya 51:6). Kamwe Alikuwa mwaminifu kwa Neno Lake alivyofanya kazi katika maisha ya Waisraeli wa zamani. Wakati aliposema atafanya kitu, alikifanya (Hesabu 11:23; Mathayo 24:35). Tunaanza kujenga imani yetu juu ya tabia Yake iliyothibitishwa. Tunaweza tumaini kwamba Mungu atakuwa mwaminifu kwake mwenyewe. Hawezi koma kamwe kufanya kama Mungu. Hawezi koma kuwa mwenye mamlaka, kuwa mtakatifu, au kuwa mwema (1 Timotheo 6:15; 1 Petro 1:16).
Tunajifunza kupitia historia yetu wenyewe kwamba hajawai kutuaibisha kamwe. Amri moja ambayo Mungu aliwapa Waisraeli wakati wote ilikuwa: “Kumbuka” (Kumbukumbu la Torati 8:2; Isaya 46:9). Wakati walikumbuka yale yote Mungu amewafanyia, waliweza kwa urahisi zaidi kumtumaini Yeye kwa mambo ya baadaye. Kimakusudi tunapaswa kukumbuka njia zote Mungu ametupa na ukombozi hapo awali. Kuweka shajara ya maombi inaweza kusaidia katika hili. Wakati tunakumbuka njia ambazo Mungu amejibu maombi yetu, inatutayarisha kuendelea kumuuliza na kutarajia majibu. Wakati tunakuja Kwake katika maombi, tunajua kwamba anatusikia kila wakati (1 Yohana 5:14; Zaburi 34:15). Anatutolea kile ambacho tunahitaji (Wafilipi 4:19). Na kila wakati atafanya kila kitu kufanya kazi kwa pamoja kwa manufaa yetu wakati tunamtumainia Yeye (Warumi 8: 28). Tunajifunza kuamini uaminifu wa Mungu wa baadaye kwa kukumbuka uaminifu Wake wa awali.
Na pia tunaweza jifunza kumtumainia Yeye kwa kujifunza kutofautisha sauti Yake kutoka kwa sauti zingine ambazo zinashindania kutambuliwa. Yesu alisema, “Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata” (Yohana 10:27). Sisi ambao ni wa Yesu tunapaswa kukuza uwezo wa kumsikia Yeye. Kimsingi anaongea kupitia Neno Lake, lakini pia anaweza kuzumgumza kupitia watu wengine, kupitia hali, na kupitia uthibitisho wa ndani wa Roho Mtakatifu (Warumi 8:16). Tunapotafakari kwa makini Maandiko, Roho Mtakatifu mara nyingi kwa uepesi huelekeza mioyo yetu kwa mstari au kifungu na kutusaidia kukikiri na kukitumia kwa hali yetu ya sasa. Kile Roho anatuonyesha katika Neno Lake kinapaswa kuchukuliwa kwa imani kuwa ujumbe Wake kwetu. Tunajenga tumaini kwa kudai ahadi Zake na kusizitumia katika maisha yetu.
Zaidi ya vitu vyote, Mungu anapenda sisi tuonyeshe imani (Waebrania 11:6). Imani ni kutumainia katika tabia ya Mungu kabla tuone vile anavyoenda kufanya mambo. Ametupa Neno Lake, na ahadi Zake bado zinasimama. Vile tunaona jinsi anavyotimilisha ahadi Zake, tumaini letu katika uaminifu Wake linakua. Jinsi tu tumaini letu kwa watu wengine linakua na marithiano ya kila siku, tumaini letu kwa Mungu linakua kwa njia hiyo hiyo. Tunamtumaini wakati tunamjua, na kumjua ni kumtumaini. Wakati tumemjua Yeye, tunaweza pumzika katika wema Wake, hata wakati hatuelewi hali ambayo inaonekana kinzani. Tunaweza tumaini kwamba mpango wa Mungu kwetu utashinda (Methali19:21). Vile mtoto anatumaini baba anayependa, tunaweza tumaini Baba wetu wa mbinguni kwa kufanya kilicho sahihi kila wakati.
English
Je, ninawezaje kujifunza kutumaini uaminifu wa Mungu?