settings icon
share icon
Swali

Je! Tutakuwa uchi mbinguni?

Jibu


Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa uchi katika bustani ya Edeni kabla ya Anguko (Mwanzo 3), na kwa kuwa hakutakuwa na laana katika Nchi Mpya (Ufunuo 22:3), wengine wanakisia kwamba, vilevile katika umilele, tutakuwa uchi. Ingawa hakutakuwa na chochote kibaya kwa waumini watukufu mbinguni kuwa uchi (hakutakuwa na tamaa huko), haionekani kuwa hali kwamba waumini watakuwa uchi milele.

Viumbe wa kimalaika na wale ambao wamekombolewa wanaelezwa katika Biblia kuwa wamevaa aina fulani ya mavazi. Katika maono ya Danieli, mjumbe (ama malaika au mwonekano wa kabla ya kupata mwili wa Kristo) alikuwa amevaa kitani na mshhipi wa dhahabu safi kiunoni mwake. Vivyo hivyo, malaika anayelinda kaburi la Yesu anaelezewa kuwa amevaa mavazi: “Sura ya huyo malaika ilikuwa kama umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.” (Mathayo 28:3).

Katika Ufunuo 4:4, wazee ishirini na wnane wanaokizunguka kiti cha enzi cha Mungu wanavaa mavazi meupe na taji za dhahabu. Ufunuo 3:5 linatuambia kwamba wale walio wa Kristo watavikwa “mavazi meupe.” Katika mifano ya Biblia ya wakaaji wa mbinguni mavazi yanatajwa mara nyingi. Kamwe hakuna dokezo kwamba mtu yeyote hapo amevuliwa nguo.

Hatutakuwa uchi mbinguni, kama Adamu na Hawa walivyokuwa kabla hawajatenda dhambi. Uchi wao ulikuwa ni ishara ya kutokuwa na hatia na kutokuwa na dhambi. Hatujawahi kuwa katika hali ya kutokuwa na dhambi, kwa hiyo, tunapofika mbinguni, tunaonyeshwa kuwa tumefunikwa na “mavazi” yaliyotolewa na dhabihu ya Kristo (Ufunuo 3:18).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tutakuwa uchi mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries