settings icon
share icon
Swali

Ni nini maana ya uchungu katika Kitabu cha Ufunuo?

Jibu


“Uchungu” ni jina la nyota katika kitabu cha Ufunuo 8:10-11: “Malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake, na nyota kubwa iliyokuwa ikiwaka kama taa ikaanguka kutoka angani, ikaangukia theluthi ya mito na chemichemi za maji- nyota hiyo inaitwa Uchungu. Theluthi ya maji yakawa machungu na watu wengi wakafa kutokana maji hayo kwa maana yalikuwa machungu.” Hii ni “hukumu ya tarumbeta” ya tatu inayofafanuliwa katika kitabu cha Ufunuo. Hizo tarumbeta saba ni hukumu ya muhuri wa saba (Ufunuo 8:1-5). Tarumbeta ya kwanza husababisha mvua ya mawe na moto anaoharibu mimea mingi duniani (Ufunuo 8:7). Tarumbeta ya pili husababisha kile kinachoonekana kuwa kimondo, kometi au chombo kinginecho cha mbinguni kinachopiga bahari na kusababisha theluthi ya vifo vya viumbe waishio baharini (Ufunuo 8:8-9). Tarumbeta ya tatu ni sawa na ya pili isipokuwa inaathiri maziwa na mito ya ulimwengu badala ya bahari (Ufunuo 8:10-11). Itasababisha theluthi ya maji yote safi duniani kuwa machungu na watu wengi watafariki kwa kuyanywa.

Neno “uchungu” linatajwa hapa tu katika Agano Jipya, lakini linaonekana mara nane katika Agano la Kale, kila mara linahusishwa na uchungu, sumu na kifo. Kifungu hicho katika kitabu Cha Ufunuo kinaweza kuwa hakisemi kuwa watu duninani kwa kweli wataiita nyota inayoanguka duniani Uchungu. Badala yake, uchungu ulikua mmea chungu uliojulikana sana katika nyakati za Biblia, kwa hivyo tunaambiwa kwamba kwa kuita nyota Uchungu,madhara yake yatakuwa kuyatia uchungu maji ya dunia, hivi kwamba maji hayanyweki. Maji hayatakuwa machungu tu, bali yatakuwa sumu. Ni rahisi kuona jinsi machafuko na hofu itatokea ikiwa maji ya kunywa yatakuwa hayapatikani kwa theluji ya wakazi wa ulimwengu. Wanadamu wanaweza kuishi siku chache tu bila maji na wakazi wa maeneo yaliyoathirika watakata tamaa na kuyanywa maji yenye sumu na kusababishwa vifo vya maelfu ya watu, ikiwa sio mamilioni ya watu.

Huu ni unabii ambao bado waja katika miaka saba ya mwisho ya enzi hii, ambayo pia inajulikana kama juma la 70 la Danieli. Hii mojawapo tu ya majanga ya asili katika tarumbeta saba ambayo yatakaribisha kuibuka kwa Mpinga Kristo na kuwa na mamlaka ya kiulimwengu kwa haraka (tazama Ufunuo mlango wa 15). Hii tu ni sehemu ya hukumu kutoka kwa Mungu, kwa vile theluthi moja ya ulimwengu inaharibiwa na hukumu hizi za tarumbeta. Ghadhabu yake kamili bado haijaachiliwa.

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini maana ya uchungu katika Kitabu cha Ufunuo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries