settings icon
share icon
Swali

Je! Daudi atatawala pamoja na Yesu katika kipindi cha miaka elfu moja?

Jibu


baada ya dhiki na vita vya Armagedoni, Yesu ataanzisha ufalme wake wa kipindi cha miaka 1000 duniani. Katika Yeremia 30, Mungu anaahidi Isreaeli kwamba nira ya ukandamizaji wa kigeni itaondelewa milele daima, na “badala yake, watamtumikia Bwana, Mungu wao na Daudi mfalme wao, nitakayemwinua kwa ajili yao” (aya ya 9). Akizungumzia wakati huo huo, Mungu anazungumza kupitia nabii Ezekieli, “Mtumishi wangu Daudi atakuwa mfalme juu yao, nao wote watakuwa na mchungaji mmoja. Watafuata sheria zangu na kuzishika amri zangu kwa uangalifu” (Ezekieli 37:24). Kutoka kwa unabii wa Yeremia na Ezekieli, baadhi wametamatisha kuwa Mfalme Daudi atafufuliwa wakati wa kipindi cha miaka elfu moja na kutawazwa kuwa mtawala mwenza juu ya Isreaeli, akitawala pamoja naye Yesu Kristo.

Unabii wa Yeremia na Ezekieli unapaswa kueleweka namna hii: siku moja Wayahudi watarudi kwa nchi yao wenyewe, nira yao ya utumwa itaondolewa, ushirika wao na Mungu utarejeshwa, na Mungu atawapa mfalme ambaye yeye mwenye atamchagua. Mfalme huyu kwa kadri atakuwa kama Mfalme Daudi wa kale. Vifungu hivi haviwezi rejelea mtu mwingine ila tu Masia, “mtumishi wa Bwana” (angalia Isaya 42:1). Wakati mwingine Wayahudi walimwita Masihi “Daudi” kwa sababu ilijulikana kwamba Masihi atatoka katika ukoo wa Daudi. Agano Jipya lilimrejelea Yesu kuwa “Mwana wa Daudi” (Matayo 15:22; Marko 10:47).

Kando na kuwa Mwana wa Daudi, kunazo sababu zingine, kwamba Masihi anaitwa “Daudi.” Mfalme Daudi katika Agano la Kale alikuwa mtu aliyeupendeza moyo wake Mungu (Matendo 13:22), alikuwa mfalme ambaye hakutarajiwa kuchaguliwa na Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa juu yake (1 Samueli 16:12-13). Basi, Daudi mfano wa Kristo (mfano ni mtu ambaye anawakilisha mtu mwingine). Mfano mwingine wa ufananisho wa aina hii ni Eliya, ambaye huduma yake ilikuwa inaashiria ile ya Yohana Mbatizaji kiwango kwamba Malaki alimwita Yohana “Eliya” (Malaki 4:5; angalia pia Luka 1:17; Marko 9:11-13).

Daudi atafufuliwa mwanzoni mwa kipindi cha Milenia, pamoja na watakatifu wengine wa Agano la Kale. Na Daudi atakuwa mmoja wa wale watatawala pamoja na Yesu katika Ufalme (Danieli 7:27). Hata hivyo, waumini wote watatawala mataifa (Ufunuo 2:26-27; 20:4) na kuhukumu ulimwengu (1 Wakorintho 6:2). Mtume Petro anawaita Wakristo “taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu” (1 Petro 2:9). Katika Ufunuo 3:21 Yesu anasema hivi kuhusu mwamini anayeshinda “nitampa haki ya kuketi pamoja nami kwenye kiti changu cha enzi.” Kwa kiwango fulani, Wakristo watashiriki mamlaka pamoja naye Kristo (angalia Waefeso 2:6). Kunao ushahidi wa kibiblia, kama vile, mfano wa fedha kumi (Luka 19:11-27), kwamba mtu binafsi atapewa mamlaka sawia katika Ufalme kulingana na vile watatekeleza wajibu ambao Mungu amewapa katika kizazi hiki (Luka 19:17).

Yesu ni Mfalme wa wafalme (Ufunuo 19:16). Kuzungumza kibinadamu, Yesu anatoka katika ukoo wa Daudi; lakini kimamlaka, kiutukufu, kiutakatifu, na kwa njia yoyote ile, anafaa kuitwa Daudi Mkuu. “Ufalme utakuwa juu ya mabega yake” (Isaya 9:6). Agano la Kale na Jipya zinaonyesha kuwa ufalme ujao katika kipindi cha miaka elfu moja na milele yote ni Yesu Kristo na ni Yeye pekee (Yeremia 23:5; Isaya 9:7; 33:22; Ufunuo 17:14; 1 Timotheo 6:15).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Daudi atatawala pamoja na Yesu katika kipindi cha miaka elfu moja?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries