Swali
Je ufufuo wa Yesu Kristo ni wa kweli?
Jibu
Bibilia yatupa ushaidi wa kutosha ya kwamba Yesu Kristo hakika alifufuka katika wafu. Ufufuo wa Yesu umenakiliwa katika Mathayo 28:1-20; Mariko 16:1-20; Luka 24:1-53 na Yohana 20:1-21:25. Yesu aliyefufuka anaonekana katika kitabu cha Matendo ya Mitume (Matendo ya Mitume 1:1-11). Kutoka ukurasa huu utapata utipitisho wa kutosha wa ufufuo wa Yesu. Kwanza ni kule kubadilika kwa ghafula kwa mitume. Walienda kutoka kwa kikundi cha watu waliofia na kujificha hadi kuwa wenye nguvu, wakishuudia kwa ujaziri injili na kuhubiri kote ulimwenguni. Nini kinachoweza kuelezea huu mpadiliko wa ghafula mbali na Kristo aliyefufuka na kuonekana kwao?
Pili ni maisha ya mtume Paulo. Ni kitu gani kilichompadilisha kutoka kutesa kanisa na kuwa mtume katika kinisa? Ni wakati Kristo aliyefufuka kutoka kwa wafu alimwonekania akiwa njiani kuelekea Dameski (Matendo ya Mitume 9:1-5). Ushaidi wa tatu wa kuaminika ni kaburi iliyo tubu. Kama Yesu hakufufuka, mwili wake uko wapi? Wanafunzi wa Yesu na wengine waliliona kaburi alimozikwa Yesu. Wakati walirudi, mwili wake haukuwa pale, malaika akasema kwamba, amefufuka kutoka kwa wafu vile alivyo aidi (Mathayo 28:5-7). Nne, ushaidi mwingine wa ufufuo wake ni watu wengi alioneekania (Mathayo 28:5,9,16-17; Mariko 16:9; Luka 24:13-35; Yohana 20:19,24,26-29, 21:1-14;Matendo ya Mitume 1:6-8; 1Wakorintho 15:5-7).
Tibitsho linguine ni ule izito mitume walitunikia ufufuo wa Yesu. Kifungu kinacho angazia ufufuo wa Yesu in 1Wakorintho15, katika mlango huu Paulo anaeleza ni kwa nini ni muimu kuelewa na kuamini ufufuo wa Kristo. Ufufuo ni wa maana kwa sababu sifuatazo 1) Ikiwa Yesu hakufufuliwa kutoka kwa wafu, waumuni hawataamini (1Wakorintho 15:12-15) kama Kristo hakufufuliwa kutoka wafu tabihu yake ya dhambi haitoshi (1Wakorintho 15:16-19). Ufufuo wa Yesu wathibitisha kwamba kifo chake kilikubaliwa na Mungu kama tabihu ya dhambi. Kama alikufa tu na kusalia kwa wafu, hiyo itaonyesha tabihu yake haitoshi. Basi kutokana na hiyo, waumini hawatapata msamaha wa dhambi zao, kwa hivyo watabaki kuwa mvu hata wakifa (1Wakorintho 15:16-19). Kwa hivyo hakutakuwa na kitu kama uzima wa milele (Yohana 3:16). “Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala” (1Wakorintho 15:20).
Hatimaye maandiko yameleeza wasi kwamba wale wote wanaomwamini Yesu Kristo watafufuliwa vile alivyofufuliwa (1Wakorintho 15:20-23). Wakorintho wa Kwanza 15 yaendelea kuelezea vile ufufuo wa Yesu waweza kuthibitisha ushindi wake juu ya dhambi ni kutupa uwezo kuishi maisha ya ushindi juu ya dhambi (1Wakorintho 15:24-34). Inaelezea hali ya utukufu ya ufufuo wa mwili tutaupokea (1Wakorintho 15:35-49). Yasema kwa ufufuo wa Kristo, wote wanaomwamini watakuwa na uwezo juu ya kifo (1Wakorintho 15:58-59).
Ni utukufu wa aina gani ulio katika ufufuo wa Kristo! “Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana” (1Wakorintho 15:58). Kulingana na Bibilia, ufufuo wa Yesu Kristo hakika ni kweli. Bibilia imenakili ufufuo wa Kristo, imenakili kwamba ilishuudiwa na watu saidi ya 400 na kuendelea kujenga funzo la Kikristo juu ya historia ya ufufuo wa Yesu.
English
Je ufufuo wa Yesu Kristo ni wa kweli?