settings icon
share icon
Swali

Mkristo anapaswa kuwa na maoni gani kuhusu uhusiano wa masafa marefu?

Jibu


Mahusiano ya masafa marefu yanaweza kuwa magumu, lakini pia yana uwezo wa kuimarisha uhusiano kati ya wahusika ikiwa kila mmoja amejitolea kwenye uhusiano. Upatikanaji wa mtandao hurahisisha uhusiano wa masafa marefu kuliko ilivyokuwa hapo awali. Sasa tuna chaguo la kutumia simu za video na mifumo nyingine nyingi za wakati halisi zinazoturuhusu kuonana na kusikiana kana kwamba tuko katika chumba kimoja. Mtandao pia umefungua mlango wa kukutana na watu kutoka sehemu za mbali, na baadhi ya mikutano hiyo husababisha uhusiano wa masafa marefu. Kuna vipengele vyema na mbaya vya uhusiano wa masafa marefu na tutachunguza machache kati ya hayo.

Wakristo wanaelwa vizuri sana utata na kufadhaika kulioko kwa uhusiano wa masafa marefu kuliko wengi kwa sababu, kwa namna fulani, tuko katika uhusiano wa masafa marefu na Yesu. Ingawa Roho wake yuko pamoja nasi daima, bado tunatamani kumwona uso kwa uso (1 Wakorintho 13:12). Paulo alionyesha hamu ya moyo ya kila mfuasi wa kweli wa Kristo alipoandika, “Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Kama nitaendelea kuishi katika mwili, kwangu hili ni kwa ajili ya matunda ya kazi. Lakini sijui nichague lipi? Mimi sijui! Ninavutwa kati ya mambo mawili: Ninatamani kuondoka nikakae pamoja na Kristo, jambo hilo ni bora zaidi. Lakini kwa sababu yenu ni muhimu zaidi mimi nikiendelea kuishi katika mwili” (Wafilipi 1:21-24).

Wakristo wanapaswa kuwa waangalifu wanapoingia katika uhusiano wa masafa marefu na mtu asiyemjua. Yesu aliwaagiza wafuasi wake wawe “werevu kama nyoka na wapole kama hua” tunaposafiri katika ulimwengu huu wa udanganyifu (Mathayo10:16). Ingawa watu wengi wamepata mapenzi ya kweli kupitia tovuti za uchumba na vyumba vya gumzo, wengine wengi wamenaswa katika hali mbaya. Tahadhari inatukumbusha kwamba mtu anaweza kuandika chochte kwenye mtandao, akijua hakuna njia ambayo taarifa zinaweza kuthibitishwa. Licha ya jinsi mtu anavyoonekana mtandaoni hatumjui kwa kweli.

Hata kati ya marafiki wanaojulikana sana, penzi la masafa marefu huwa na hatari. Kuna uwezekano kwa kila mmoja kupata mtu mwingine karibu. Msemo wa zamani mara nyingi ni wa kweli: “Kutokuwepo hufanya moyo uwe na shauku—kwa mtu mwingine.” Wanadamu hutamani urafiki wa karibu, na ikiwa uhusiano wa masafa marefu haukidhi hitaji hilo, mtu anazweza kushawishika kukomesha uhusiano huo na kuwa na penzi lingine . Ukosefu wa uaminifu huwa kawaida kwa ndoa za masafa marefu kwa sababu ya ukosefu huu wa urafiki. Kwa sababu hiyo, Wakristo waliofunga ndoa ambao hawawezi kuwa pamoja na wenzi wao wanahitaji kulinda mioyo yao na “wasitimize tamaa za miili yao” (Warumi 13:14). Huwa tunahuruhusu mwili kushawishika kutenda dhambi tunapochochea tamaa za mwili zisizotimizwa na kujiweka katika hali ambapo tamaa hizo haziwezi kutimizwa isipokuwa kupitia dhambi.

Kikwazo kingine kwa uhusiano wa masafa marefu ni kwamba, bila ukaribu, hatuwezi kuona tabia katika mipangilio masafa marefumasafa marefu. Anaweza kuwa mzuri kwenye simu za video, lakini anamtendeaje mhudumu kwenye mkahawa? Anaitikiaje anapokasirika— na nini kinachomkasirisha? Anashirikianaje na watu wa familia yake? Vipengele vingine muhimu vya uhusiano haviwezai kujulikana bila kutumia muda pamoja na mtu.

Kwa mtazamo mzuri, mahusiano ya masafa marefu hutoa fursa ya kuzingatia mawasiliano ya moyo kwa moyo bila vikwazo vya maisha ya kila siku. Wanandoa wa kijeshi hushuhudia hili wakati mmoja wao anapotumwa. Ingawa kutengana ni kunahuzunisha, wanaweza kuthamini nyakati wanazopata kutumia pamoja. Hawachukulii kila mmoja kwa kawaida au kuchoka na ushirika wa mwingine. Wanaweza kubuni njia mpya za kuunda ukaribu wa kiroho na kihemko huku wanapokosa fursa ya kuwa pamoja. Kwa wapenzi ambo hawajaoana, uhusiano wa masafa marefu pia husaidia kujilinda dhidi ya marjaibu ya ngono kwa kupunguza fursa zake (1 Wakorintho 6:18).

Wakristo wanapaswa kutathmini uhusiano wa masafa marefu sawa na vile wangefanya katika uhusiano mwingine. Ikiwa uhusiano haujazingatia kujitolea kwa Kristo, sio uhusiano mzuri. Ikiwa hauleti hamu kwa kila mtu kuishi maisha matakatifu zaidi, ya kujitolea, sio uhusiano mzuri. Ikiwa washiriki “hawahimizani katika upendo na matendo mema,” sio uhusiano mzuri (Waebrania 10:24). Hata hivyo, ikiwa pande zote mbili zimejitolea kwa kila mmoja na kwa Bwana, wanaweza kuona msimu wao wa utengano kama uwanja wa mafunzo wa kile ambacho Mungu anataka kufanya katika maisha yao (Yakobo 1:2-4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo anapaswa kuwa na maoni gani kuhusu uhusiano wa masafa marefu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries