settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu uinjilisti wa kabla?

Jibu


Uinjilisti wa kabla inamaanisha vitu tofauti kwa watu tofauti. Baadhi wanaona uinjilisti wa kabla kama kufanya kile Paulo alifanya na wanafalsafa katika Mars Hill. Alianza na kile walichokijua kuhusu “Mungu asiyejulikana” na walibishana kwa kuwepo kwa Mungu wa kibinafsi (Matendo ya Mitume 17:22-34) ambaye anahitaji uadilifu. Aina hii ya uinjilisti wa kabla unatafuta kukutana na watu mahali walipo. Wengine wanaona uinjilisti wa kabla kama “uinjilisti wa urafiki” ambapo muumini anaanzisha uhusiano wa kiurafiki na asiye muumini na, kwa matendo ya ukarimu na kuishi maisha ya Kikristo mbele yake, ukweli wa injili utaonekana ata kabla ya kuushiriki. Wengine wanaona uinjilisti wa kabla kama utayarishaji pana katika kuomba msamaha kabla ya kujaribu kushiriki injili na wengine.

Ingawa hatuwezi kuchulia kuwa watu hii leo wamesikia kuhusu Kristo, tunastahili kuelewa kwamba Warumi 1:19-20 inatuhakikishia kwamba Mungu alituumba hili tujue kuhusu Yeye kwa sababu Yeye amefanya dhahiri ndani ya kila binadamu aliyezaliwa. Ufahamu kuhusu Mungu unaweza patikana kwa kuangalia uumbaji na kuona “asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu” vile Paulo anasema katika kifungu hiki katika Warumi. Mungu alituumba hivyo ili yeyote asidai kamwe kwamba hatujui kuhusu uwepo Wake. Kwa maneno mengine, “hatuna sababu.” Ufahamu huo wa milele wa Mungu kisha unaongoza binadamu kumtafuta Yeye, na tumehakikishiwa ikiwa tutafanya hivyo, Yeye atapatikana kwa sababu “ijapokuwa kwa kweli hakai mbali na kila mmoja wetu” (Matendo 17:24-28).

Hivyo uwepo wa “shimo la umbo la Mungu” ndani yetu inatuongoza kumtafuta Mungu, kumpata Yeye, na kumwabudu Yeye. Kwa kufanya hivyo, tunapata uzima wa milele na uradhi wa kweli, amani, furaha, na kuridhika. Kwa huzuni, watu wengi badala yake wanaanza kuabudu uumbaji, sio Muumbaji (Warumi 1:21-23). Wanajaribu kubadilisha hitaji lao kwa Mungu na kitu chochote kile. Yesu aliagiza wanafunzi Wake wote, wa zamani, na wa sasa, na wa baadaye, waende nje katika dunia na kueneza injili, habari njema ya dhabihu Yake juu ya msalaba kwa ajili yetu. Sababu alitupatia amri hii ni kwamba, ingawa Mungu alituumba sisi sote na uwezo wa kumjua Yeye, wengi bado wanamkataa na kumdharau Yeye. Kumkubali Kristo kama Mwokozi una maana lazima tukubali ukweli kwamba sisi ni wenye dhambi na tunahitaji kukombolewa. Hivyo, kukiri dhambi zetu inamaanisha kuacha kiburi na kuinama mbele za Mungu katika ombi la unyenyekevu la ukombozi. Watu wengi sana, ata baada ya kusikia ujumbe wa Ukweli mara kwa mara, hawawezi kufanya hivyo.

Kufikia watu kwa ufanisi na injili ahitaji wafuasi wa Kristo kuenenda mlango hadi mlango katika uhamazisho wa injili, ingawa katika hali nyingi hiyo ni njia inayofaa, lakini badala yake kuishi wokovu wetu kwa furaha, tumaini, na amani kwamba watu ambao tunakutana nao kila siku haiwezi saidai lakini wanaona Kiristo katika maisha yetu. Vile 1 Petro 3:15 inasema, “mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao..” Sisi wafuasi wa Yesu Kristo kwa kweli ni “taifa teule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu walio milki ya Mungu, mlioitwa ili kutangaza sifa zake yeye aliyewaita kutoka gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu” (1 Petro 2:9).

Tuna wajibu wa kushiriki mwangaza wa injili ya Yesu Kristo na wale watu ambao wako katika nyanja yetu ya ushawishi kila siku, kwa mfano, majirani wetu, watu tuanofanya kazi nao, yeyote ambaye tunakutana naye. Hakuna sadfa inayohusika katika hali inayozunguka watu tunaokutana nao kila siku, fursa pekee inayotolewa na Mungu “nuru yenu na iangaze mbele ya watu” kwamba waweze kumtukuza Baba yetu mbinguni (Mathayo 5:16).

Kuanzisha uhusiano na watu katika nyanja ya ushawishi inatuhitaji tuwajue na kuwa na matakwa mema kwa maisha yao. Mazungumzo ambayo yanayohusisha maswali ili kuwajua zaidi na kisha kisikiza kikamilifu na kuuliza maswali ya kufuatilia ni njia bora sana ya kuanzisha uhusiano. Tunapopata kuwajua watu, tunaweza kuuliza maswali zaidi ya kibinafsi sawa na mstari, “Unaamini katika Mungu?” au “Je, una imani katika nini au unaamini nini katika maisha yako?” jambo ambalo linaweza kutusaidia sana kujua ni nini wanachoona kuwa muhimu zaidi maishani. Hii inaweza kusaidia kuweka msingi tunapotafuta kushiriki Habari Njema na wao.

Kila mtu katika haya maisha anapitia majaribu na dhiki, na kuamazisha watu walio karibu nasi kujua kwamba, wakati tunakumbana na shida, imani na tumaini letu liko katika Kristo, na tunaweza kuwasaidia kutambua kwamba wanamhitaji Yeye pia. Hakuna kinachoweza kuzungumza kwa nguvu zaidi kwa wale wako karibu nasi kuliko ushahidi wa amani ya ajabu ya Mungu katika maisha yetu katikati mwa magumu.

Zaidi ya yote, wakati tunapokuwa na mazungumzo na watu wanaotuzunguka kila siku tunahitaji kutumia ushuhuda wa kibinafsi na Neno la Mungu kama silaha katika sanduku la zana zetu. Kumwambia mtu jinsi tuliweza kuwa na uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo na kutumia Maandiko kuunga mkono inaleta nguvu ya Mungu kwa ushuhuda wetu. Vile tunajua, sio maneno yetu bali ni nguvu ya Roho Mtakatifu ambayo inasadikisha ulimwengu wa dhambi (Yohana 16:8).

Huku tukitengeneza uhusiano na kutafuta fursa ya kushiriki Kristo na wale ambao tunakutana nao kila siku inaweza kuonekana kama sio mpango mzuri, lakini imalizia kuwa njia mwafaka zaidi ya kuinjilisha ulimwengu hii leo. Na sehemu bora ya kushiriki Kristo kwa namna hii, kwa vile uhusiano na mtu huyo tayari upo, inatuweka katika nafasi nzuri ya kumwadhibu anapokuja katika imani. Uwanafunzi ni sehemu muhimu ya ukuaji kiroho na husaidia kuanzisha na kuimarisha msingi imara kwa imani yetu ambayo itakuwa milele.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu uinjilisti wa kabla?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries