Swali
Ukristo ni nini? Wakristo huamini nini?
Jibu
Wakorintho wa kwanza 15: 1-4 inasema, “Tena ndugu zangu, ninawatangazia tena ile injili ambayo nimekwisha kuwahubiri ambayo mmeipokea nakusimama ndani yake; ambayo kupitia hiyo mmeokolewa mkiendelea kukumbuka yale niliyowahubiri msije mkawa mmeamini bure. Kwa kuwa niliwapatia kwanza kile nilichokuwa nami nimepokea, kwa jinsi ile Yesu aliyokufa kwa ajili ya dhambi zetu kulingana na maandiko; na akazikwa, hatimaye akafufuka tena siku ya tatu kulingana na maandiko.
Kwa kifupi hii ndiyo imani ya kikristo. Ukristo ni imani maalum kulinganisha na nyinginezo, Kwa sababu inasimamia zaidi ushirika na Mungu kuliko matendo ya kidini. Kinyume na kushikilia orodha ya masharti ya fanya haya na usifanye yale, Lengo la mkristo ni kutafuta ushirika wa karibu na Mungu Baba. Ushirika huo unawezeshwa na kazi aliyoifanya Yesu pamoja na huduma ndani ya maisha ya mkristo ya Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini ya kuwa biblia ni Neno la Mungu na mafundisho yake ndiyo mamlaka ya mwisho (Timotheo wa pili 3:16, Petro wa pili 1: 20-21). Wakristo huamini juu ya Mungu mmoja akaaye katika utatu, Baba na Mwana (Yesu kristo), na Roho Mtakatifu.
Wakristo huamini yakwamba mwanadamu aliumbwa ili awe na ushirika na Mungu lakini dhambi hutenganisha watu wote na Mungu (Warumi 5:12, Warumi 3:23). Imani ya kikristo hufundisha ya kwamba Yesu kristo alitembea juu ya ardhi akiwa Mungu kamili na huku akiwa pia mwanadamu (Wafilipi 2:6-11), na akafa msalabani. Wakristo huamini ya kwamba, baada ya kifo chake msalabani, Yesu alizikwa, akafufuka na sasa anakaa upande wa kuume wa Mungu Baba akiwaombea waumini milele (Waebrania 7:25). Imani ya kikristo inasema ya kwamba kifo chake Yesu kristo msalabani kilitosha kufidia dhambi za watu wote na hili ndilo linalorejeza ushirika baina ya Mungu na mwanadamu (Waebrania 9:11-14, Waebrania 10;10, Warumi 6:23, Warumi 5:8).
Ili uokolewe, sharti uweke imani yako juu ya kazi Yesu aliyoimaliza msalabani. Mtu akiamini kuwa Yesu alikufa mahali pa yeye ili amlipie gharama zake za dhambi na akafufuka tena basi mtu huyo ameokoka. Hakuna kitu mtu anachoweza kufanya mwenyewe binafsi ili aokoke. Hakun mwema wa kutosha kumpendeza Mungu kwa kuwa sote ni wenye dhambi (Isaya 64:6-7, Isaya 53:6). Lengine ni kwamba hakuna cha ziada maana kazi yote ilifanywa na kristo! Alipokuwa msalabani, Yesu alisema, “Imekwisha” (Yohana 19:30).
Kama vile haikugharimu chochote kuokolewa ila kuamini kazi iliyofanywa na Yesu msalabani vile vile hakuna kazi ambayo unahitajika kufanya ili upoteze wokovu wako. Kumbuka kazi ilifanywa na kumalizwa na yesu! Hakuna chochote kinachotegemea wewe mwenyewe katika wokovu. Yohana 10:27-29 inasema “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na ninawajua na wao hunifuata. Nami huwapa uzima wa milele; nao hawatapotea wala hakuna awezaye kuninyang’anya kutoka mikononi mwangu. Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote na hakuna awezaye kuwatoa kutoka mikononi mwa Baba.”
Wengine hufikiria nakusema, “Nikiokolewa tu naweza kufanya kila nitakacho na wala sitapoteza wokovu wangu!” lakini wokovu si juu ya kuwa huru kufanya mapenzi yako. Wokovu ni kuwa huru kutoka kwa nyororo za dhambi ulizokuwa ukizitumikia iliuwe huru kumtumikia Mungu. Kadri waumini wanavyoishi duniani, kutakuweko na hali ya kupingana na dhambi katika miili yao. Kuishi na dhambi kunazuia ushirika na Mungu na muumini yeyote atakaye amua kuishi na dhambi hatafurahia ushirika wake na Mungu. Hata hivyo wakristo wanaweza kushinda dhambi kwa kulisoma na kulitumia neno la Mungu (biblia) maishani mwao na kuongozwa na Roho Mtakatifu – hiyo ina maana ya kujiachilia uongozwe na Roho katika kila shughuli ya siku na pia kupitia Roho uheshimu neno la Mungu.
Kwa hivyo, huku dini nyingine zikitaka waumini wao watende mambo Fulani Fulani au wasitende mambo Fulani ukristo ni juu ya kuwa na ushirika na Mungu. Deni lako la dhambi limelipwa na unaweza kuwa na ushirika na Mungu. Unaweza kuwa na ushindi juu ya maisha yako ya dhambi na ukatembea na ushirika na Mungu ukiwa mtiifu. Huwo ndiwo ukristo wa kweli unaoelezewa katika Biblia.
English
Ukristo ni nini? Wakristo huamini nini?