settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema ni umri gani unaofaa kwa ndoa?

Jibu


Biblia haisemi hususani umri wa mtu kuoa; badala yake, inazungumza kwa maneno ya jumla ya ndoa kuwa ya wale ambao “wamekomaa” (ona Ruthu 1:12-13). Lugha na tamaduni zote mbili za Biblia zinaunga mkono kwa dhati wazo kwamba kubalehe, kwa kiwango cha chini kabisa, ni hali ambayo lazima itimizwe kabla ya kuwa mwenzi wa mtu. Hili linapatana na mojawapo ya madhumuni ya kihistoria ya ndoa—kupata mimba na kulea watoto. Uthibitisho wa kimaandiko unaonyesha kwamba wale ambao ni wachanga sana kwa kuzaa hawapaswi kuolewa, ingawa hakuna umri unaotajwa wazi katika Biblia.

Ni busara kuangalia mazoea ya Uyahudi wa kale kwa masuala ya kitamaduni juu ya umri sahihi wa ndoa. Kulingana na mila, wavulana hawakuzingatiwa kuwa “wanaume wamekomaa,” na kwa hiyo hawakuweza kuoa, hadi umri wa miaka 13. Wasichana hawakuzingatiwa “wanawake” hadi umri wa miaka 12. Umri huu zaidi au chini yake unafanana na mwanzo wa kubalehe. Ingawa enzi hizo zinaweza kuonekana kuwa changa sana kwetu, sio umri wa kawaida wa kuoa, kihistoria. Imekuwa tu ni ndani ya karne iliyopita kwamba umri wa wastani wa kuolewa umekuwa ni mwishoni mwa miaka ya ishirini na mwanzoni mwa miaka ya thelathini.

Ni muhimu pia kukumbuka kuwa ukomavu—mara nyingi hutumika kama kigezo cha kuruhusu kujamiiana katika ndoa—hii san asana ni kitamaduni. Katika nchi za kisasa za Magharibi, watu hawatarajiwi kwa ujumla kujitegemea hadi wawe na umri wa karibu miaka ishirini, au hata baadaye. Walakini, kwa sehemu kubwa ya hisoria ya mwanadamu, watu walitarajiwa “kukua” haraka zaidi. Umri wa kuoa kwa kawaida ulikuwa mchanga, kwani kila mtu alitajariwa kukomaa kijamii na kihemko haraka kuliko leo hii.

Lugha ya Kiebrania pia inaunga mkono wazo kwamba kubalehe ni takwa halali la ndoa. Ezekieli 16 ina sitiari ya uhusiano wa Mungu na Israeli. Katika kifungu hiki, Mungu anajali Israeli, anayeonyeshwa kama msichana yatima katika hatua mbalimbali za ukuaji. Bwana kwanza huona kuzaliwa kwake, kisha humwona akikua: “Ukakua na kuongezeka sana, ukawa kito cha thamani kuliko vyote. Matiti yako yakatokeza na nywele zako zikaota, … Baadaye nikapita karibu nawe, nilipokutazama na kukuona kuwa umefikia umri wa kupendwa, nililitandaza vazi langu juu yako” (mistari 7-8). Katika kielezi hiki, ni baada ya msichana tu kufikia ukomavu wa kimwili, wakati fulani baada ya (si wakati) wa balehe “anapokuwa na umri wa kutosha kupendwa,” ndipo yuko tayari kwa ndoa.

Kiebrania, kama lugha zingine, hutumia maneno tofauti kwa washiriki wachanga na wazee wa jinsia yoyote. Na’ar inarejelea vijana, huku yeled ikirejelea wavulana wenye umri wa miaka 12 au chini. Kwa wanawake, neno na’arah linamaanisha “mwanamke wa kuolewa,” huku yaldah ikirejelea msichana wa miaka 11 au chini— mchanga sana kwa ndoa. Kwa mara nyingine tena, maneno na fasili hizi zinaonekana kutekeleza wazo kwamba mwanzo wa kubalehe ni hitaji la ndoa. Kabla ya wakati huo, mvulana au msichan si wa umri wa kuolewa.

Agano Jipya lina machache ya kusema kuhusu umri wa kuoa au kuolewa. Bado, kuna vidokezo katika Agano Jipya la Kigiriki sawa na zile za Kiebrania. Kwa mfano, 1 Wakorintho 7:36 inatumia neno hyperakmos kurejelea mwanamke. Katika kesi hii, ni mwanamke mchanga ambaye amechumbiwa kuolewa.hyperakmos maana yake halisi ni “kuiva” neno la kawaida katika tamaduni nyingi la kuelezea uwezo wa mwanamke kuzaa watoto. Paulo kujumuisha neno hilo kwa hakika kunaonyesha kwamba umri wa kuolewa ulikuwa wakati fualani baada ya kubalehe, wakati mwanamke amekua kikamilifu. Lakini Maandiko hayana mahali popote ambapo huweka umri dhahiri wa kuolewa; ukomavu wa kimwili ni wa lazima, lakini msichana anapofikia ukomavu unaweza kutofautiana. Mtoto mwenye umri wa miaka 12 katika Marko 5:41-42 bado ni “msichana mdogo” na ni wazi kuwa hayuko tayari kwa ndoa.

Sawa na masuala mengine mengi, umri ufaao wa kuolewa una sehemu ya kitamaduni ambayo Biblia haipuuzi kabisa. Kinachojumuisha umri unaofaa wa ndoa kinaweza kutofautiana kutoka tamaduni hadi tamaduni na bado iwe katika mipaka ya mwenendo ufaao wa kimaandiko. Jambo la msingi ni kwamba ndoa za watoto na ndoa za utotoni hazikubaliwi. Ni lazima mtu awe mzima ili aolewe; lazima awe amekomaa kimwili vya kutosha kwa ajili ya kujamiiana na kuzaa mtoto. Zaidi ya hayo, Biblia haitaji umri wa chini kabisa wa kufunga ndoa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema ni umri gani unaofaa kwa ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries