Swali
Je! Usalama wa milele ni “kibali” cha kutenda dhambi?
Jibu
Kila mara pingamisho katika mafunzo ya usalama wa milele ni kwamba, yawaruhusu watu kuishi njia yoyote ile waipendayo na bado wataokolewa. Ingawa hii kwa njia “nyingine” yaweza kuwa kweli, lakini kwa ukweli kabisa huu si ukweli. Mtu ambaye amekombolewa na Yesu Kristo hawezi kuishi maisha yanatambulika kwa kutenda dhambi makusudi. Lazima tuweke tofauti jinzi Mkrosto anavyostahili kuishi na inampasa nini ili aupokee wokovu.
Bibilia ii wazi kwamba wokovu ni kwa neema kaitka imani pekee iliyo katika Yesu pekee (Yohana 3:16; Waefeso 2:8-9; Yohana 14:6). Wakati mtu anapo mwamini Yesu Kristo huyo mtu ameokolewa na yuko salama katika wokovu. Wokovu haupatikani kwa imani kisha baadaye udumishwe kwa matendo. Mtume Paulo analiangazia swala hili katika Wagalatia 3:3 wakati anasema, “Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza kaitka Roho, mnataka kukamilishwa sasa kaitka mwili?” kama tumeokolewa kwa imani, wokovu wetu pia umedumishwa na kulindwa kwa imani. Hatuwezi pata wokovu wetu wenyewe. Kwa hivyo, hata hatuwezi kudumisha wokovu wetu kwa nguvu zetu wenyewe. Ni mungu mwenyewe ndiye anausimamisha wokovu wetu (Yuda 24). Ni mkono wa Mungu watushika kaitka viganja vyake na kutudumisha (Yohana 10:28-29). Ni upendo wa Mungu pekee ambao hakukuna kitu kitatutenganisha naye (Warumi 8:38-39).
Kataa lolote la usalama wa milele, kwa hali yake ni sawa na kuamini kuwa ni lazima tusimamishe wokovu wetu kwa matendo yetu mazuri na nguvu zetu wenyewe. Hii ni kinyume na wokovu ni kwa neema. Tumeokolewa kwa sababu ya kazi nzuri ya Yesu, bali si yetu (Warumi 4:3-8). Kusema kwamba ni lazima tulitii neno la Mungu ama kuishi maisha ya utakatifu ndio tusimamishe wokovu wetu ni sawa na kusema kuwa kifo cha Yesu hakitoshi kulipa gharama ya dhambi zetu. Kifo cha Yesu kilitosha kulipa deni ya dhambi zetu, za kale, sasa, na baadaye, kabla ya wokovu, na baada ya wokovu (Warumi 5:8; 1 Wakorintho15:3; 2 Wakorintho 5:21).
Je! Hii inamaanisha Mkristo anaweza kuishi vile atakavyo na bado aokoke? Hili ni swali lizilo na msingi wowote, kwa sababu Bibilia imeliweka wazi kuwa Mkristo hawezi ishi “njia yoyote atakayo.” Wakristo ni viumbe vipya (2 Wakorintho 5:17). Wakristo wanaonyesha matunda ya Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:22-23), si matendo ya mwili (Wagalatia 5:19-21). Yohana wa kwanza 3:6-9 yasema wazi kwamba Mkristo wa kweli hawezi kuendelea katika maisha ya dhambi. Kwa kuyajibu mashtaka kwamba neema yaongeza dhambi, Mtume Paulo anasema, “Tuseme nini basi?Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi?” (Warumi 6:1-2)
Usalama wa milele si kibali cha kutenda dhambi. Ni usalama wa kujua kwamba upendo wa Mungu emeruhusiwa wale wote wanaomwamini Kristo. Kujua na kutambua kipawa cha Mungu cha ajabu cha wokovu kinapita fahamu kwamba neema ya wokovu ni kibali cha kutenda dhambi. Inawezekanaje kwa mtu anayejua gharama Yesu Kristo aliyotulipia na kuendelea katika dhambi (Warumi 6:15-23)? Inawezekanaje mtu anayeelewa kuwa upendo wa Mungu usio kipimo kwa wale waminio, kuchukua huo upendo na kutupa tena mbele za Mungu? Mtu kama huyo anaonyesha si eti usalma wa milele umempa kibali cha kufanya dhambi pekee, bali hashuhudia wokovu katika Yesu Kristo. “Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atenday dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua” (1Yohana 3:6).
English
Je! Usalama wa milele ni “kibali” cha kutenda dhambi?