Swali
Biblia inasema nini kuhusu uvumi?
Jibu
Neno la Kiyahudi lililotafsiriwa "Uvumi" katika Agano la Kale hufafanuliwa kama “mfunuaji siri au mtu mpayukaji ambaye ana habari kuandamana juu ya watu na kuendelea kuyatangaza." Mvumi ni mtu ambaye ana bahati ya kuwa na ujumbe kuhusu watu na kuendelea kufunua habari hiyo kwa wale hawana aja kuijua. Uvumi unatofautishwa kutoka kubadilishana habari na dhamira yake. Wavumi wana lengo la kujijenga wenyewe kwa kufanya wengine kuonekana wabaya na kujiinua wenyewe kama aina fulani ya hifadhi za seli ya elimu.
Katika kitabu cha Warumi, Paulo anaonyesha asili ya dhambi na uasi wa wanadamu, na kuelezea jinsi Mungu alimwaga ghadhabu yake juu ya wale waliokataa sheria zake. Kwa sababu walikuwa wamegeuka mbali na mafundisho na uongozi wa Mungu, aliwapa kwa tamaa zao za dhambi. Orodha ya dhambi ni pamoja na kusengenya na wasingiziaji (Warumi 1: 29b-32). Tunaona kutoka kwenye kifungu hiki jinsi dhambi ya uvumi ni baya na kwamba sifa ya wale walio chini ya ghadhabu ya Mungu.
Kundi jingine ambao walikuwa (na bado wako hii leo) maalumu kwa ajili ya kujiingiza katika uvumi ni wajane. Paul anawaonya wajane dhidi ya kuburudani tabia ya uvumi na ya kuwa wavivu. Wanawake hawa kama ilivyoelezwa "wasengenyaji na wajongezi na wadadisi, wakinene maneno yasiyowapasa" (1 Timotheo 5: 12-13). Kwa sababu wanawake huwa wanatumia muda wao mwingi nyumbani na kufanya kazi kwa karibu na wanawake wengine, wao husikia na kuchunguza hali ambayo inaweza kuwa potofu, hasa wakati inarudiwa mara kwa mara. Paulo anasema kwamba wajane huingia katika tabia ya kwenda kutoka nyumbani kwa nyumbani, kuangalia kitu cha kusiba uvivu wao. Mikono vivu ni karakana ya shetani, na Mungu anaonya dhidi ya kuruhusu uvivu kuingia katika maisha yetu. "Mwenye kitango akisingizia hufunua siri, basi, usishirikiane naye afunuaye midomo yake sana" (Mithali 20:19).
Wanawake kwa hakika si wao tu ambao wamepatikana na hatia ya uvumi. Mtu yeyote anaweza kushiriki katika uvumi tu kwa kurudia kitu kulichosikika kwa kujiamini. Kitabu cha Mithali kina orodha ndefu ya aya ambazo husungumzia hatari ya uvumi na uumivu matokeo yake huleta. "Asiye na akili humdharau mwenziwe, bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza. Mwenye kitango akisingizia hufunua siri, bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo" (Mithali 11: 12-13).
Biblia inatuambia kwamba "Mtu mshupavu huondokesha fitina, na mchongezi huwafarakanisha rafiki" (Mithali 16:28). Urafiki mwingi umeharibika juu ya kutoelewana kwa sababu ilianza na uvumi. Wale ambao hujiingiza katika tabia hii hufanya kitu karaha na kusababisha hasira, uchungu, na maumivu kati ya marafiki. Cha kusikitisha, baadhi ya watu hustawi juu ya hili na hutafuta fursa za kuharibu wengine. Wakati baadhi ya watu hao wanakabiliwa, wao hukana madai na kujibu kwa visingizio na kujumlisha. Badala ya kukubali makosa, wao huwekea mtu mwingine lawama au hujaribu kupunguza uzito wa dhambi. "Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake, na midomo yake ni mtego wa nafsi yake. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo, nayo hushukia pande za ndani za tumbo" (Methali 18: 7-8).
Wale ambao hutunza ndimi zao hujizuilia wao wenyewe kutoka msiba (Mithali 21:23). Kwa hiyo, tunapaswa kutunza ndimi zetu na kujiepusha na tendo la dhambi ya uvumi. Kama sisi husalimisha tamaa yetu ya asili kwa Bwana, atatusaidia kuwa wenye haki. Na zote tufuate mafundisho ya Biblia juu ya uvumi kwa kuzuilia midomo yetu iwe kimya isipokuwa ni muhimu na sahihi kuongea.
English
Biblia inasema nini kuhusu uvumi?