settings icon
share icon
Swali

Uwili ni nini?

Jibu


Katika teolojia, dhana ya uwili inakubali kwamba kuna vyombo viwili tofauti-mema na mabaya ambayo yana nguvu sawa. Katika "Ukristo" uwili, Mungu Anawakilisha chombo kizuri na Shetani anawakilisha chombo kibaya.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba hata kama Shetani ako baadhi ya nguvu, yeye hayuko sawa na Mwenyezi Mungu kimamlaka, kwa maana aliumbwa na Mungu kama malaika kabla ya kuasi kwake (Isaya 14:12-15; Ezekieli 28:13-17). Kama Maandiko yanavyosema, "Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na Mungu ninyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia" (1 Yohana 4:4). Kulingana na maandiko, hakuna uwili, hakuna nguvu mbili sawia pinzani ziitwazo mema na mabaya. Wema, unawakilishwa na Mwenyezi Mungu, nguvu kuu zaidi katika ulimwengu bila ubaguzi. Mabaya, na huwakilishwa na Shetani, ni nguvu ndogo kwamba hakuna upinzani kwa ajili ya mema. Mabaya hushindwa kila wakati kuna mapishano yoyote ya ana kwa ana na wema, kwa sababu Mwenyezi Mungu, kiini cha wema, ni mwenye nguvu zote, ambapo uovu, unaowakilishwa na Shetani, sio wenye nguvu.

Wakati fundisho lolote linaonyesha mema na mabaya kama vikosi viwili sawia kupingana, fundisho hilo linaenda kinyume na nafasi ya maandiko matakatifu kuwa wemai, unaowakilishwa na Mwenyezi Mungu, ni nguvu kubwa katika ulimwengu. Kwa kuwa shetani hakuwa, na kamwe hatakuwa sawa na Mungu, mafundisho yoyote yanasema kwamba yeye yuu sawa, yanaweza kuwekwa alama kama mafundisho ya uongo. Ukweli kwamba Shetani alitupwa kutoka mbinguni kwa kujaribu kupanda zaidi ya Mungu haimaanishi kwamba Shetani amekata tamaa ya kujaribu kuwa sawa au bora kuliko Mungu, kama ilivyoshuhudiwa na malengo ya msingi ya "uwili" ambayo yamekuja kwa kiasi kikubwa kupitia kwenye shina la falsafa ya hekima ya binadamu.

Kunaweza kuwa hakuna uwili uliopo katika pembe yoyote ya ulimwengu wetu. Kuna nguvu moja tu ambayo ni kuu, na nguvu hiyo ni Mwenyezi Mungu kama iliyofunuliwa kwetu katika Biblia. Kwa mujibu wa ushahidi wa maandiko, kuna nguvu moja tu kwamba ni Mwenye nguvu, sio mbili. Hivyo, mafundisho yoyote ya uwili ambayo yanakubali kuwa kuna nguvu mbili sawa hupinga kila moja (mema na mabaya) ni mafundisho ya uongo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Uwili ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries