settings icon
share icon
Swali

Wafu katika Kristo ni akina nani katika 1 Wathesalonike 4:16?

Jibu


Kabla ya kuwatambua “waliokufa katika Kristo,” tunapaswa kutambua muktadha ambamo kifungu hiki kinapatikana. Muktadha wa karibu ni 1 Wathesalonike 4:13-18, ambayo inahusika na swali la ni nini kitatokea wakati wa kurudi kwa Bwana Yesu. Wasomaji wa Paulo walikuwa na wasiwasi kwamba Kristo atakaporudi, wale waliokufa kabla ya wakati huo kwa namna fulani wangekosa. Kusudi kuu la kifungu hiki ni kuwafariji wale waumini ambao wamepoteza wapendwa wao wanaoamini.

Ujumbe wa kifungu hiki ni ujumbe wa matumaini. Wakristo wana tumaini ambalo wasioamini hawana wakati wanapofiwa na wapendwa wao. Kuna tumaini baada ya kaburi kwa Wakristo, na sehemu ya tumaini hilo ni wakati wa kurudi kwa Kristo, wale ambao tayari wamekufa “watafufuka kwanza.” Baada ya hayo, Wakristo ambao bado wako hai watabadilishwa. Vikundi vyote viwili “vitanyakuliwa” na vitakutana na Bwana mawinguni. Paulo anatamatisha sehemu hii kwa maonyo ya kuwatia moyo wengine wenye tumaini hili.

Katika kifungu hiki, Paulo anatumia neno la usafidi la kulala kurejelea wale waliokufa katika Kristo, yaani waumini. Paulo anataka kuwafariji wasomaji wake kwamba wale Wakristo ambao wamekufa kabla ya kurudi kwa Kristo hawatakosa chochote. Ndio maana anaanza sehemu hii kwa kusema, “Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini” (aya ya 13).

Kwa hivyo, ili kujibu swali, waliokufa katika Kristo ni wale waumini ambao wamekufa kabla ya ujio wa pili wa Kristo. (Kumbuka iwe 1 Wathesalonike 4 inarejelea ujio wa pili au unyakuzi ni suala la kujadiliwa). Waumini, iwe wamekufa au wako hai, ni wa Kristo. Tunapata lugha kama hiyo kutoka kwa Mtume katika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho anapoandika, “Lakini kila mmoja kwa wakati wake: Kristo, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja” (1 Wakorintho 15:23). Wafu katika Kristo haitumiki tu kwa hadhira ya awali ya Paulo, bali kwa waumini wote ambao wamekufa katika kile kinachoweza kuitwa kipindi cha “majalio”, au wakati kati ya ujio wa kwanza na wa ujio wa pili wa Kristo.

Swali lingine linaloweza kujitokeza katika muktadha huu ni nini kinatokea kwa waumini wanapokufa? Kwa hakika Paulo anatumia usingizi kurejelea hali yao, lakini je, hii ina maana kwamba waumini hupitia (kwa kukosa neno bora zaidi) hali ya kukosa fahamu kama ya usingizi hadi ufufuo ujao? Wale wanaotetea msimamo huu, unaoitwa usingizi wa nafsi, msingi wao ni katika vifungu kama vile 1 Wathesalonike 4:13-18. Lakini ikumbukwe kwamba “usingizi” kama ulivyotumika hapa ni usafidi. Haikusudiwi kumaanisha usingizi halisi. Kwa kweli, uzoefu wa muumini baada ya kifo na kabla ya mwisho wa enzi wakati Kristo atakaporudi ni ushirika wa ufahamu, wa furaha na Bwana. Paulo anadokeza hili katika mistari kama vile 2 Wakorintho 5:6-8 na Wafilipi 1:23.

Wakati wa kifo, mwili unalala kaburini ukingoja ufufuo wa siku ya mwisho, lakini roho huenda kuwa nyumbani pamoja na Bwana. Hili ni fundisho la hali ya kati. Waumini huona kwa muda thawabu zinazowangojea mbinguni, huku wasioamini wakionja mateso yao ya milele kuzimu (Luka 16:19-31).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Wafu katika Kristo ni akina nani katika 1 Wathesalonike 4:16?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries