Swali
Je ni nini maana ya kuwaheshimu baba yangu na mama?
Jibu
Kuwaheshimu baba yako na mama ni kuwa wa heshima katika usemi na tendo na kuwa na nia ya ndani ya heshima kwa hali yao. Neno la Kigiriki kwa heshima linamaanisha "stahi, tuzo, na thamani." Heshima haileti sifa tu bali hata cheo. Kwa mfano, baadhi ya Wamarekani wanaweza kutokubaliana na maamuzi ya Raisi, lakini wao bado wanapaswa kuheshimu nafasi yake kama kiongozi wa nchi yao. Vile vile, watoto wa umri wote wanapaswa kuwa heshima kwa wazazi wao, bila kujali kama wazazi wao "wanastahili" heshima au hawastahili.
Mungu Anatusihi tuheshimu baba na mama. Anathamini kuwaheshimu wazazi sana hadi akaijumlisha katika amri kumi (Kutoka 20:12) na tena katika Agano Jipya: "Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii nidyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri ukae siku nyingi katika dunia" (Waefeso 6:1-3). Kuwaheshimu wazazi ndio amri pekee katika maandiko inayoahidi maisha ya muda mrefu kama malipo. Wale ambao uheshimuwazazi wao wana heri (Yeremia 35:18-19). Kwa upande mwingine, wale walio na " akili potofu " na wale ambao huonyesha uasi katika siku za mwisho wanatambulika kwa kutotii wazazi (Warumi 1:30, 2 Timotheo 3:2).
Sulemani, mtu mwenye hekima, alitoa wito kwa watoto kuwatii wazazi wao (Mithali 1:8; 13:1; 30:17). Ingawa sisi huenda tusiwe chini ya mamlaka yao tena, hatuwezi kuiondoa ile tabia ya amri ya Mungu kwa heshima ya wazazi wetu. Hata Yesu, Mungu Mwana alinyenyekea kwa wazazi wake wa mwili hapa duniani (Luka 2:51) na kwa Baba yake wa mbinguni (Mathayo 26:39). Kufuatia mfano wa Kristo, tunapaswa tuwachukulie wazazi wetu kwa njia tunayomweshimu Baba yetu wa mbinguni (Waebrania 12:9, Malaki 1:6).
Ni wazi, kuwa tumeamrishwa kuwaheshimu wazazi wetu, lakini jinsi gani? Kuwaheshimu kwa vitendo na tabia (Marko 7:6). Heshimu matarijio yao yaliyotajwa na yale hayajatajwa. "Mwana wa hekima husikiliza mahusia ya baba yake; bali mwenye dharau hasikilizi maonyo" (Mithali 13:1). Katika Mathayo 15:3-9 Yesu aliwakumbusha Mafarisayo amri ya Mungu ya kuheshimu ya baba na mama. Walikuwa wanatii barua ya sheria, lakini wao walikuwa wameiongeza mila zao wenyewe ambazo ziliifutilia mbali amri ya Mungu. Wakati waliheshimu wazazi wao katika neno, matendo yao yalidhihirisha nia yao halisi. Heshima ni zaidi ya huduma ya mdomo. Neno "heshima" katika kifungu hiki ni kitenzi, na kwa hivyo linanahitaji hatua za haki.
Tunapaswa kutafuta kuwaheshimu wazazi wetu njia ile ile sisi hujitahidi kuleta utukufu kwa Mungu-katika mawazo yetu, maneno na matendo. Kwa mtoto mdogo, kutii wazazi huenda sako kwa bako na kuwaheshimu. Hiyo ni pamoja na kusikiliza, kuzingatia na kunyenyekea kwa mamlaka yao. Baada ya watoto kukomaa, utiifu waliojifunza wakiwa watoto utawahudumia vizuri katika kuheshimu mamlaka mengine kama vile serikali, polisi, na waajiri.
Huku tukihitajika kuwaheshimu wazazi,hiyo haijumulishi kuiga wale waovu (Ezekiel 20:18-19). Kama mzazi milele humfundisha mtoto kufanya kitu ambacho ni kinyume na amri za Mungu, huyo mtoto lazima amtii Mungu kuliko wazazi wake (Matendo 5:28).
Heshima huleta heshima. Mungu hawezi heshima wale ambao hawatii amri yake wala kuheshimu wazazi wao. Kama tunatamani kumpendeza Mungu na kuwa na heri, tunapaswa kuheshimu wazazi wetu. Kuheshimu sio rahisi, daima si furaha, na kwa hakika si rahisi kwa nguvu zetu wenyewe. Lakini heshima ni njia fulani kwa lengo letu katika maisha kumtukuza Mungu. "Watoto, watiini wazazi wenu katika kila kitu, maana hiyo humpendeza Bwana" (Wakolosai 3:20).
English
Je ni nini maana ya kuwaheshimu baba yangu na mama?