settings icon
share icon
Swali

Ni wakati ni wakati gani muafaka wa kuoa?

Jibu


Wakati muafaka kwa ajili ndoa ni tofauti kwa kila mtu na wa kipekee kwa kila hali. Ngazi za ukomavu na uzoefu wa maisha ni kigezo tofauti; watu wengine huwa tayari kwa ndoa kuanza miaka 18, na baadhi kamwe hawako tayari kwa ajili yake. Kiwango cha talaka Marekani kinapozidi asilimia 50, ni dhahiri kwamba sehemu kubwa ya jamii yetu haioni kuona ndoa kama ahadi ya milele. Hata hivyo, huu ni mtazamo wa dunia, ambao kwa kawaida huitilafiana na wa Mungu (1 Wakorintho 3:18).

Msingi imara ni muhimu kwa ajili ya mafanikio ya ndoa na lazima uanzishwe kabla ya mmoja kuanza kuchumbia mpenzi. Mwenendo wetu wa kikristo lazima uuzishwe na mengi zaidi mbali na kuhudhuria kanisa tu siku ya Jumapili na kuhusika katika kujifunza Biblia. Ni lazima tuwe na uhusiano binafsi na Mungu ambao unakuja tu kupitia kwa kuamini katika na kumtii Yesu Kristo. Ni lazima tujielimishe wenyewe kuhusu ndoa, kutafuta mtazamo wa Mungu juu yake, kabla ya kujiingiza ndani. Mtu lazima ajue ni nini Biblia inasema kuhusu upendo, ahadi, mahusiano ya kingono, jukumu la mume na mke, na matarajio yake kabla tujiingize katika ndoa . Kuwa na angalau maharusi Wakristo kama mfano wa kuigwa ni muhimu pia. Wanandoa wakomavu wanaweza kujibu maswali kuhusu yale yanayoendelea ndani ya ndoa na mafanikio, jinsi ya kujenga urafiki (zaidi wa kimwili), jinsi imani ni mchango mkubwa sana, nk

Wanaotazamiwa kuwa wanandoa pia wanahitaji kuhakikisha kwamba wao wanajuana vizuri sana. Wanapaswa kujua maoni ya kila mmoja kuhusu ndoa, fedha, mashemeji, ulezi wa watoto, nidhamu, majukumu ya mume na mke, kama ni mmoja tu au ni wote wawili watafanya kazi nje ya boma, na kiwango cha ukomavu kiroho cha mwingine. Watu wengi huolewa kwa kuchukua maneno ya mpenzi wao kuwa yeye ni Mkristo, na kugundua baadaye kwamba ilikuwa tu huduma ya mdomo. Kila wachumba wanauia ndoa wanatakiwa kwendea ushauri kwa mshauri nasaha Mkristo wa ndoa au mchungaji. Kwa kweli, wachungaji wengi hawawezi funganisha harusi isipokuwa wamekutana mara kadhaa na wachumba katika mazingira ya ushauri nasaha.

Ndoa ni si kujitoa tu pekee, bali ni agano na Mungu. Ni ahadi ya kubaki na huyo mtu mwingine maisha yako yote yanayosalia, haijalishi kama mpenzi wako ni tajiri, masikini, wa afya, mgonjwa, mnono, mkonde, au wa kuchosha. Ndoa ya kikristo inafaa kuvumilia kila hali, ikiwa ni pamoja na mapigano, hasira, uharibifu, maafa, huzuni, uchungu, madawa ya kulevya, na upweke. Ndoa kamwe haipaswi kuingiwa na wazo kwamba talaka ni chaguo- sio eti ni jambo la mwisho. Biblia inatuambia kwamba kwa njia ya Mungu mambo yote yanawezekana (Luka 18:27), na bila ya shaka ni pamoja na ndoa. Kama wanandoa hufanya uamuzi mwanzoni kukaa na kujitolea na kumweka Mungu kwanza, talaka sio suluhisho ili kuepukika hali mbayai.

Ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu anataka kutupatia tamaa za moyo wetu, lakini hiyo in inawezekana tu kama tamaa zetu zinaingiana na zake. Mara nyingi watu huolewa kwa sababu "inahisika vizuri." Katika hatua za mwanzo wa uchumba, na hata wa ndoa, unaweza kuona mtu mwingine anakuja, na unapta tumbo joto. Mapenzi ni kilele chake, na unajua hisia ya kuwa "katika upendo." Wengi wanatarajia kuwa hisia hii itabaki milele. Ukweli ni kwamba haibaki. Matokeo yanaweza kukatisha tamaa na hata talaka hisia hizo zinapoisha, lakini wale walio katika ndoa na mafanikio hujua kwamba msisimko wa kuwa na mtu mwingine hauna mwisho. Badala yake, vitumbo joto hutoa njia ya upendo zaidi, ahadi nguvu, msingi imara zaidi, na usalama madhubuti.

Biblia ii wazi kwamba upendo hautegemei hisia. Hii ni dhahiri wakati tunaambiwa kuwapenda maadui zetu (Luka 6:35). Upendo wa kweli unawezekana tu wakati tunaruhusu Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yetu, kuzalisha matunda ya wokovu wetu (Wagalatia 5:22-23). Ni uamuzi sisi hufanya kila siku wa kujifia na ubinafsi wetu, na kumruhusu Mungu uangaze ndani yetu. Paulo anatuambia jinsi ya kuwampenda wengine katika 1 Wakorintho 13:4-7: "Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; ;upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauehesabu mabaya; haufarahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli ni; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahiimili yote." Wakati sisi tu tayari kumpenda mtu mwingine kama 1 Wakorintho 13:4-7 inaeleza huo ndio wakati muafaka wa kuoa.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni wakati ni wakati gani muafaka wa kuoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries