settings icon
share icon
Swali

Je! Wakati wa kifo ni upi kulingana na Biblia?

Jibu


Biblia inasema kifo hakiwezi kutenduliwa bila muujiza wa kimungu (Waebrania 9:27; 1 Wakorintho 15:22). Isichokisema kwa uwazi ni wakati kifo kinakuwa “rasmi.” Maendeleo ya matibabu yametoa njia za kuwarudishia fahamu wale ambao hapo awali hawakuwa na matumanini. Hiyo imeelekeza kwa swali, hakika ni lini tofauti inawekwa kuwa “hai” au “mfu.” Hili limeibua mjadala wa iwapo mwili wa mtu unaweza kuwa hai kimatibabu, huku nafsi na roho zikiwa zimeondoka kabisa. Hali kama hizo ni nadra lakini zinashangaza. Ingawa Maandiko yanatoa mwongozo, hatuwezi kupata vitambulisho kamili hakiki vya kumtanga mtu kuwa kweli amekufa.

Kutoka kwa mtazamo wa kibiblia, kifo “halisi” hutokea wakati nafsi na roho vinatoka kwenye mwili wa nyama. Kwa wazi, hii sio tuko ambalo linaweza kuzingatiwa kwa macho au kupimwa na vifaa vya matibabu. Badala yake, mtazamo wa kibiblia ungekuwa kulinganisha ishara za kimwili na kazi za nafsi na roho. Wakati mtu anaonekana kupoteza hali ya kufanya kazi kiwango hauwezi rejeshwa, ni muhimu kuamini kuwa amekufa kweli.

Kuna mifano mingi ya wale walio katika hali ya kuzimia au hali ya kutojifahamu na wakapona, n ahata kuwa katika hali ya kuzimia wakati mwingine walionyesha dalili za ufahamu. Kulingana na Biblia, watu hao hawakuwahi kuwa “wafu kikweli.” Kiroho, walikuwa katika hali sawa na mtu ambaye amelala: nafsi iko lakini haifahamu kikamilifu mazingira yake. Wale waliofunguliwa kuwa “ubongo umekufa” kwa upande mwingine, wanaonekana kuwa hai kibaolojia, na seli zinazoendelea kufanya kazi, lakini ubongo wao umeacha kufanya kazi, na hawana ufahamu wowote wa roho; kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kutokuwa na nafsi au roho.

Jumuiya ya matibabu inachukulia kifo kuwa cha mchakato, badala ya kuwa cha muda mfupi. Vipimo vinavyotumiwa kutambua kifo vimetofautiana katika historia. Kwa karne nyingi, kupumua kulizingatiwa kuwa kigezo cha kupimia uhai. Wale ambao hawakupumua walitangazwa kuwa wafu. Vifaa vya matibabu vilipoimarika, kiwango hicho kilihamia kwneye mpigo wa moyo. Leo hii, unaweza kupima kupumua, mpigo wa moyo, na shughuli za ubongo kwa kiwango kisichoweza kuonekana kwa jicho. Kwa hiyo, wataalamu wa matibabu leo wanatofautisha kati ya “kifo cha kimwili,” na “kifo cha kibaolojia,” n ahata “kifo cha kisheria,” kulingana na mada ya mazungumzo.

Tunaweza kuwa na uhakika kwamba kifo, kinapotokea kweli, hakiwezi kutenduliwa na dawa au utaalamu. Mara tu mtu “amekufa kweli,” nafsi na roho yake hutenganishwa kabisa na mwili. Utengano huo unaweza tu kubatilishwa kwa kuingilia moja kwa moja kwa Mungu katika muujiza wa kweli. Kwa hiyo, watu wanapozungumza kuhusu “kurudishwa”kutoka kwa kifo kwenye gani la wagonjwa au “kufa kwa dakika kumi,” wanatumia maneno yasiyo sahihi kibiblia. Katika hali kama hizo, watu hao walikaribia kufa, lakini hakuwa wamekufa kwa kweli.

Ubinadamu kwa muda mrefu umetambua utata wa kutambua kifo halisi kinapotokea. Kwa mtazamaji wa kawaida, inawezekana kwa mtu kuonekana amekufa lakini kwa kweli awe hai. Utambuzi huo unaonyeshwa katika unabii na miujiza katika Biblia. Kw amfano, Yesu alichelewesha kimakusudi kumfufua Lazaro hadi siku ya nne baada ya kifo chake (Yohana 11:17). Ukawiaji huu ulizuia dai lolote linalowezekana kwamba ilikuwa hila au kwamba Lazaro alikuwa tu katika hali ya kukosa fahamu au amelala. Kwa kweli, wakati Yesu alipofika, familia ya Lazaro ilikuwa na wasiwasi juu ya uvundo wa kuharibika (Yohana 11:39).

Vile vile, Yesu alitabiri kwamba Angekuwa kaburini kwa “mchana tatu na usiku tatu,” kwa kuwa hicho ndicho kilikuwa kipindi cha kungoja kidesturi ambacho kisha kifo kingeonekana kuwa rasmi (Mathayo 12:40). sio kwamba hii ilikuwa muhimu kabsia-Yesu aliuawa na wauaji wa kitaalamu (Yohana 19:13-18), alichomwa mkuki kwa moyo (Yohana 19:33-34), na kuzikwa katika kaburi lililolindwa (Mathayo 27:62-66). Kipindi cha muda wa siku tatu, katika kisa cha Yesu, kilikuwa zaidi kwa sababu za kinabii kuliko sababu za “Ushahidi.”

Katika kisa cha Yesu na Lazaro na watu wengi katika historia, si lazima kufafanua wakati hususani wa kifo-bila shaka walikuwa wamekufa. Mijadala juu ya wakati kifo kinatokea inahusisha eneo nyembamba sana la “kijivu” na haitumiki kwa uzoefu mwingi wa mwanadamu. Utataa zaidi ni matukio wakati mwili wa mtu unaonyesha ishara za kibaolojia za maisha lakini kuna shaka juu ya kazi ya ubongo. Hali ya kutokuwa na fahamu, hali ya kuwa na fahamu, na “ubongo kufa” huingia katika eneo hili.

Kwa sehemu kubwa, wale walio katika hali ya kutokuwa na fahamu, na hali kuwa na fahamu bado huchukuliwa kuwa “hai,” pamoja na ufahamu mdogo. Kuruhusu mtu kama huyo afe kwa kuondoa msaada wa maisha au kutomtunza kunaweza kusababisha utengano wa roho kutoka kwa mwili, yaani, ingesababisha kifo cha “kweli.” Mwili unaoonyesha kifo cha ubongo, kwa upande mwinine, utaonekana kuwa ambao nafsi na roho tayari zimeachwa nyuma. Kutoa mtambo wa kusaidia kutoka kwa mwili uliogunduliwa na kifo cha umbongo hakutaonekana kusababisha kifo, kwa maana ya kibiblia, kwa kuwa huyo mtu ashakufa.

Kwa sababu hii, Wakristo wengi wanapinga kukomesha maisha ya mtu akiwa katika hali ya kutokuwa na fahamu. Katika visa vya kifo cha ubongo, au wakati maisha yanwezekana tu kwa hatua kali, Wakristo mara nyingi hugawanyika juu ya maadili ya kuruhusu mtu kufa kwa kawaida. Wosia hai ziliundwa mahsusi kushughulikia maswala haya. Kwa wazi, hii ni mada iliyo wazi kwa tofauti kubwa za maoni. Wakati wa kujadili au kuamua mada kama hiyo, Wakristo wanapaswa kutanguliza utakatifu wa maisha huku wakiwa na neema na kusamehe wengine.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Wakati wa kifo ni upi kulingana na Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries