Swali
Bibilia inasema nini kuhusu uponyaji? Je! Kunao uponya katika damu ya Yesu Kristo?
Jibu
Isaya 53:5, ambayo imenukuliwa katika 1 Petero 2:24 ndio kuu juu ya uponyaji, lakini kila mara imeeleweka vipaya na imetumika vipaya. “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.” Neno ambalo limetafsiriwa “kuponywa” linaweza maanisha kiroho au kimwili. Ingawa katika mukhtadha wa Isaya 53 na 1 Petero 2 waifanya wazi kuwa inazungumzia juu ya uponyaji wa kiroho. “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa” (1 Petero 2:24). Aya hii inazungumzia ya dhambi na utakatifu, si ugonjwa na magonjwa. Kwa hivyo, “kuponywa” kwa aya hizi zote mbili ni kuzungumzia kuwa umesamehewa n akuokolewa, sio uponyaji wa kimwili.
Bibilia wazi wazi haishikanishi uponyaji wa mwili na uponyaji wa kiroho. Wakati mwingine watu wameponywa magonjwa ya kimwili wakati wanaweka Imani yao katika Kristo, lakini hii kila mara hakui hivo. Wakati mwingine ni mapenzi ya Mungu kuponya, lakini wakati mwingine sio mapenzi yake. Mtume Yohana anatupa mtazamo mzuri sana: “Na huu ndio ujaziri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawaswa namapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba” (1 Yohana 5:14-15). Mungu bado atenda miujiza. Mungu bado aponya watu. Ugonjwa na magojwa, maumivu, na kifo ni vitu halisi katika ulimwengu huu. Labda tu Bwana arudi, mtu yeyote aliye hai hii leo atakufa, na wengi wao (Wakristo wakiwemo) watakufa kwa sababu ya shida za kimwili (magonjwa, majeraha). Kila mara si mapenzi ya Mungu kutuponya kimwili.
Mwisho, uponyaji wetu kamili wa mwili unatungoja huko mbinguni. Mbinguni, hakutakuwa na maumivu, magonjwa, mateso au kifo (Ufunuo 21). Zote tunastahili kuwaza sana hali yetu ya mwili katika ulimwengu huu na tujishughulishe na hali yetu ya kiroho (Warumi 12: 1-2). Basi tutatizamia nyoyo zetu mbingu mahali ambapo hatutakuwa na shida yo yote kimwili. Ufunuo 21:4 yaelezea uponyaji wa kweli ambao wote tunastahili kuutarajia: “Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”
English
Bibilia inasema nini kuhusu uponyaji? Je! Kunao uponya katika damu ya Yesu Kristo?