Swali
Kwa nini ni Wakristo wote ni wanafiki?
Jibu
Labda hakuna shutuma ya kuudhi zaidi kuliko ile ya "mnafiki" ingawaje, baadhi ya wengine hujiisi haki kwa maoni yao kwamba Wakristo wote ni wanafiki. Neno "mnafiki" linafurahia urithi tajiri katika lugha ya Kiingereza. Neno hilo (unafiki) linatujia sisi kupitia Kilatini lenye maana ya "uigaji, kujifanya." Tukienda nyuma kidogo, neno linaonekana katika vitabu vy elemu ya Wayunani na Warumi na Kigiriki cha Agano Jipya na lina dhana sawa na kiuga sehemu, kujifanya.
Hii ndio njia ya Bwana Yesu alilitumia neno. Kwa mfano, wakati Kristo alifundisha umuhimu wa sala, kufunga, na sadaka kwa watu wa ufalme, Yeye alitukataza sisi kufuata mifano ya wale ambao ni wanafiki (Mathayo 6:2, 5, 16). Kwa kufanya sala ndefu kwa umma, kukunja uso ili kuhakikisha wengine wamewaona wakifunga, na kuonyeshana vipaji vyao Hekalu na kwa maskini, wao walionyesha wazi uhusiano wao wa nje kwa Bwana. Wakati Mafarisayo walitekeleza vizuri wajibu wao mkubwa kama mfano kwa umma wa fadhila ya kidini, walishindwa vibaya sana katika ulimwengu wa ndani wa moyo ambapo nguvu za kweli hukaa (Mathayo 23:13-33; Marko 7:20-23).
Yesu kamwe hakuwaita wanafunzi wake wanafiki. Jina hilo lilipewa tu kwa kuwapotosha wakereketwa wa kidini. Badala yake, Aliwaita walio wake mwenyewe "wafuasi," " watoto wachanga," "kondoo," na "kanisa" yake. Aidha, kuna onyo katika Agano Jipya kuhusu dhambi ya unafiki (1 Petro 2:1), ambayo Petro anaiita "unafiki." Pia, mifano miwili ya wazi ya unafiki kumbukumbu yake iko katika kanisa. Katika Matendo 5:1-10, wanafunzi wawili wamewekwa wazi kwa kujifanya kuwa wakarimu kuliko vile walikuwa. Matokeo yake ni kali. Na kati ya watu wote, Petro anakabiliwa kwa kuongoza kundi la wanafiki jinsi wanavyo wachukulia waamini wa Mataifa (Wagalatia 2:13).
Kutoka kwa mafundisho ya Agano Jipya, basi, tunaweza kutoa angalau hitimisho mbili. Kwanza, wanafiki wapo kati ya wanaojiita Wakristo. Walikuwepo katika mwanzo, na kwa mujibu wa mfano wa Yesu wa magugu na ngano, hakika wao huwepo mpaka mwisho wa dunia (Mathayo 13:18-30). Fauka ya hayo, hata mtume anaweza kuwa na hatia ya unafiki, hakuna sababu ya kuamini kwamba Wakristo wa "kawaida" watakuwa huru kutoka humo. Tunapaswa kuwa macho ili sisi tusiche tukaanguka katika majaribu yale yale (1 Wakorintho 10:12).
Bila shaka, si kila mtu anayedai kuwa Mkristo kwa kweli ni Mkristo. Labda wote au baadhi ya wanafiki maarufu miongoni mwa Wakristo hakika walikuwa watu wanaodai ukweli na waongo. Hadi leo hii, viongozi maarufu wa Kikristo wameanguka katika dhambi ya kutisha. Fedha na kashfa ya ngono wakati mwingine huonekana pigo kwa jumuiya ya kikristo. Hata hivyo, badala ya kuchukua hatua ya wachache na kuitumia kwa kuikebehi jamii nzima ya Wakristo, tunapaswa kujiuliza kama wale wote wanaodai kuwa Wakristo kwa kweli ni wakristo. Mistari mbalimbali ya kibiblia huthibitisha kwamba wale ambao kwa kweli ni wa Kristo wataonyesho matunda ya Roho (Wagalatia 5:22-23). Mfano wa Yesu wa mbegu na udongo katika Mathayo 13 unaweka wazi kwamba sio wote wanadai imani kwake ni wa kweli. Cha kusikitisha, wengi wanaokiri kuwa wake itastaajabisha siku moja ukisikia akiwaambia, " Sikuwajua ninyi kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu "(Mathayo 7:23).
Pili, huku isiw ni kitu cha kutshangaza kwamba watu ambao hujifanya kuwa watakatifu zaidi ya vile walivyo, hudai kuwa Wakristo, hatuweza kuhitimisha kwamba Kanisa imeundwa takribani na wanafiki pekee. Mmoja hakika anaweza kukubaliana kwamba sisi sote ambao tunalitaja jina jina la Yesu Kristo hubaki kuwa wenye dhambi hata baada ya dhambi zetu kusamehewa. Hiyo ni, hata kama sisi tumeokolewa na dhambi ya adhabu milele (Warumi 5:1; 6:23), sisi bado hatujaokolewa na kutolewa katika uwepo wa dhambi katika maisha yetu (1 Yohana 1:8-9), ikiwa ni pamoja na dhambi ya unafiki. Kwa njia ya imani ya maisha yetu katika Bwana Yesu, tunaendelea kushinda nguvu za dhambi mpaka sisi hatimaye tukombolewe (1 Yohana 5:4-5).
Wakristo wote hushindwa kuishi kikamilifu kiwango kile Biblia inafundisha. Hakuna Mkristo aliyewahi kuwa mkamilifu kama Kristo. Hata hivyo, kuna Wakristo wengi ambao kwa dhati watafuta kuishi maisha ya Kikristo na wanamtegemea zaidi na zaidi Roho Mtakatifu kuwatia hatiani, kuwabadilisha, na kuwawezesha. Kumekuwa na umati wa Wakristo ambao wamekuwa wakiishi maisha yasiyo ya kashfa. Hakuna Mkristo aliye makamilifu, lakini kufanya makosa na kushindwa kufikia ukamilifu katika maisha haya sio jambo sawa na kuwa mnafiki.
English
Kwa nini ni Wakristo wote ni wanafiki?