settings icon
share icon
Swali

Nani / nini walikuwa Wanefili?

Jibu


Wanefili ("walio anguka, majitu") walikuwa watoto wa mahusiano ya kimapenzi kati ya wana wa Mungu na binti wa binadamu katika Mwanzo 6:1-4. Kuna mjadala kama utambulisho wa "wana wa Mungu." Ni ubishi wetu kwamba "wana wa Mungu" walikuwa malaika walioanguka (mapepo) ambao walijunziana na wanawake binadamu na / au wanaume binadamu waliopagagwa na kisha wakajumbiana na wanawake binadamu. Uhusiano huu ulisababisha watoto Wanefili, kwamba walikuwa "mashujaa wa zamani, watu wenye sifa" (Mwanzo 6:4).

Kwa nini mapepo wafanye jambo kama hilo? Biblia haitupi jibu hasa. Mapepo ni maovu, viumbe-ivilvyo geuzwa kwa hivyo hakuna kitu wanachokitenda kinafaa kutushangaza. Kama motisha ya kipekee, uvumi bora zaidi ni kwamba mapepo walikuwa wanajaribu kuchafua damu ya binadamu ili kuzuia ujio wa Masihi, Yesu Kristo. Mungu aliahidi kwamba Masihi atakuja kutoka uzao wa Hawa (Mwanzo 3:15) ambaye ataponda kichwa cha joka hilo, Shetani. Hivyo, mapepo walikuwa uwezekano wa kujaribu kuzuia hili na kuchafua ukoo wa binadamu, na kuifanya vigumu kwa ajili ya Masihi asiye na dhambi siku moja kuzaliwa. Tena, hili si jibu hasa la kibiblia, lakini ni uwezakano na si katika utata na kitu chochote Biblia inafundisha.

Wanefili walikuwa nani? Kwa mujibu wa Hebraic na hadithi zingine (kitabu cha Henoko na nyinginezo za maandiko yasiyo ya kibiblia), walikuwa kizazi kikubwa cha mashujaa maarufu ambao walifanya vitendo vya uovu mkubwa. Kawaida ukubwa na nguvu zao zilitokana na mchanganyiko wa “chembe cha za damu” ya mapepo na zile za binadamu. Yote ambayo Biblia moja kwa moja inasema kuhusu wao ni kwamba walikuwa "mashujaa wa zamani, watu wenye sifa" (Mwanzo 6:4). Wanefili walikuwa si wageni, walikuwa halisi, viumbe wa kimwili zinazozalishwa kutoka muungano wa wana wa Mungu na binti wa watu (Mwanzo 6:1-4).

Ni nini kilichotokea kwa Wanefili? Wanefili walikuwa moja ya sababu za msingi kwa ajili ya mafuriko kubwa katika wakati wa Nuhu. Pindi tu baada ya Wanefili wametajwa, neno la Mungu linatuambia hivi: "Bwana akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba niewafanya" (Mwanzo 6:5-7). Hivyo, Mungu aliendelea na mafuriko kwa dunia nzima, na kuua kila mtu na kila kitu (ikiwa ni pamoja na Wanefili) zaidi ya Nuhu na familia yake na wanyama waliokuwemo ndani ya safina (Mwanzo 6:11-22).

kulikuwa na Wanefili baada ya mafuriko? Mwanzo 6:4 inatuambia, "Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baad ya hayo wan wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa." Inaonekana kwamba mapepo walirudia tendo la dhambi wakati mwingine baada ya mafuriko. Hata hivyo, ilifanyika kwa kiasi kidogo kuliko ilivyokuwa kabla ya mafuriko. Wakati wana wa Israeli walipeleleza nchi ya Kanaani wao walimpasa Musa taarifa: "Kisha huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona"(Hesabu 13:33). Basi, kifungu hiki hakisemi hasa kwamba Wanefili walikuwapo, ila wapelelezi waliwaza kuwa waliona Wanefili. Kuna uwezekano zaidi kuwa wapelelezi walishuhudia watu wakubwa sana katika Kanaani na kimakosa wakaamini kuwa wao ni Wanefili. Au, inawezekana kwamba baada ya mafuriko mapepo tena walijumbiana na wanawake binadamu, na kuzalisha zaidi Wanefili. Kwa hali yoyote ile, hawa "majitu" waliharibiwa na wana wa Israeli wakati wa uvamizi wao kwa Kanaani (Yoshua 11:21-22) na baadaye katika historia yao (Kumbukumbu 3:11; 1 Samweli 17).

Ni nini inazuia mapepo kutoka kuzalisha Wanefili Zaidi hii leo? Inaonekana kwamba Mungu alikomesha mapepo kuchumbiana na binadamu kwa kuweka mapepo yote waliofanya kitendo kama hicho katika lindi kuu. Yuda mstari wa 6 inatuambia, "Na, malaika walioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu." Ni wazi, si mapepo yamewekwa katika "gerezani" hii leo, hivyo lazima kuna kundi la mapepo wamekuwa wakifanya dhambi chungu zaidi ile ya awali ya kuanguka. Takribani, mapepo ambayo yalichumbina na wanawake binadamu ni wale ambao "wamefungwa minyororo ya milele." Hii itazuia mapepo yoyote zaidi kujaribu kitendo kama hicho.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nani / nini walikuwa Wanefili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries