settings icon
share icon
Swali

Je, nafsi za watoto wa kuavya huenda mbinguni?

Jibu


Utaoaji mimba kama tunavyoujua leo haukuwa ukitekelezwa katika nyakati za Biblia, na Biblia hasa haitaji kamwe suala la kuavya mimba. Ni wazi kutoka katika Maandiko kwamba mtoto ambaye hajazaliwa anajulikana na Bwana, hata tangu wakati wa kutungwa mimba (Zaburi 139:13-16). Ingawa Biblia haitaji kuavya mimba au watoto wa kuavya, tuna mambo mawili ya kutusaidia kujibu swali la ikiwa nafsi za watoto walitolewa mimba huenda mbinguni.

Jambo la kwanza ni katika kifungu pekee cha Biblia ambapo jambo mahususi linasemwa kuhusu kifo cha watoto wachanga. Katika 2 Samweli 12 tunasoma kuhusu uhusiano kimapenzi wa Daudi na Bathsheba, mke wa mtu mwingine. Daudi alijulishwa na nabii Nathani kwamba mtoto aliyezaliwa na muungano huo angekufa. Ndipo Daudi akaanza kufunga na kuomba, akimwomba Bwana asitekeleza hukumu yake. Wakati mtoto huyo alipokufa, Daudi aliinuka kutoka kwa kuomba na kufunga na akala kitu.

Alipoulizwa kuhusu tabia hiyo, Daudi alitamka maneno yaliyoandikwa katika 2 Samweli 12:23, “Lakini sasa kwa kuwa amekufa, kwa nini nifunge? Je, naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake, lakini yeye hatanirudia mimi.” Maneno ya Daudi yanaonyesha kwamba mtoto hawezi kurudi ulimwenguni, lakini Dauni angekuwa pamoja na mtoto wake mbinguni siku moja. Hii haionyeshi tu uhakikisho wa Daudi wa wakati ujao wake mbinguni lakini (Zaburi 23:6), lakini pia uhakikisho kwamba mtoto wake angeshiriki wakati huo ujao. Kutokana na simukizi hii, tunaweza hitimisha kwamba watoto wachanga wanaofariki wamekusudiwa kwenda mbinguni.

Jambo la pili katika kushughulikia suala hili ni ufahamu wa tabia na sifa za Mungu. Mungu wa haki lazima aadhibu dhambi, kwa kuwa Biblia inatufundisha kwamba “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23). Mtoto ambaye hajazaliwa na watoto waliotolewa mimba hawajapata fursa ya kuteenda dhambi kimakusudi; hata hivyo, kila mtoto anayetungwa mimba hubeba asili ya dhambi iliyoridhiwa kutoka kwa Adamu (Zaburi 51:5) na kwa hivyo yuko chini ya hukumu. Wakati huo huo, Mungu anajidhihirisha kama Mungu wa wema na fadhili (Zaburi 136:26). Yeye ni “mwenye haki katika njia zake” (Zaburi 145:17). Inaweza kuwa kwamba Mungu, kwa neema yake, anatumia dhabihu ya Yesu kwa watoto amabo hawajazaliwa wa uavyaji mimba. Tunajua kwamba damu ya Kristo inatosha kwa jambo hilo. Baada ya yote, Kristo alikufa “kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote” (1 Yohana 2:2).

Biblia haijasema bayana ikiwa mtoto ambaye hajazaliwa anapofariki anaenda mbinguni au la. Bila kifungu wazi, tunaweza kukisia tu. Hata hivyo, tunajua kuhusu upendo wa Mungu, wema na huruma yake. Tunajua uhakika wa Daudi kwamba angekuwa pamoja na mtoto wake tena. Na tunajua kwamba Mungu aliwaalika watoto waje Kwake (Luka 18:16). Tukizingaztia uhakika huu, tunaamini inafaa kuhitimisha kwamba nafsi za watoto huwa mbele ya Mungu mara moja wakati maisha yao yanapokatizwa kwa uavyaji mimba.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, nafsi za watoto wa kuavya huenda mbinguni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries