settings icon
share icon
Swali

Je, ninawezaje kugundua wito wangu wa kiroho?

Jibu


Watu wanataka kujua jinsi wanaweza kugundua miito yao ya kiroho, yaani, kile ambacho Mungu anawaita kufanya na maisha yao. Wanataka kujua kusudi moja kuu la Mungu kwa ajili yao, karama moja kuu ya kiroho ambayo itafikia mamia, maelfu au mamilioni ya watu, ukweli ni kwamba, hata hivyo, Mungu hawaiti watu wengi kuweka maisha yao wakfu katika eneo moja maalum. Na ikiwa anafanya hivyo, anafanya hivyo kwa wakati Wake.

Katika utamaduni maarufu wa Kikristo, kwa kawaida ni wale watu ambao hupata mafanikio yasiyosaaulika na kudumu huko kwa miaka mingi ndio hupata kuvutia. Viongozi wakuu wa makanisa, wanamuziki, na wainjilisti mara nyingi hutumia miongo kadhaa kufanya kazi na kukamilisha eneo moja ambalo Mungu amewaita kutumikia. Lakini idadi kubwa ya waumini hawajaitwa katika kuweka msingi wa huduma. Badala yake, tumeitiwa huduma mbalimbali, kulingana na kiwango chetu katika maisha, ukomavu wetu kiroho, na mahitaji ya wale wanaotuzunguka. Mungu ametuita kumtumikia mahali tunamoishi. Mtu aliye na kipaji cha kufundisha anaweza kuongoza darasa la shule ya Jumapili kwa muda, kufundisha katika shule ya Kikristo, na kisha kuandika mtaala. Au anaweza kufanya kazi katika benki na kupata fursa ya kuwafundisha wengine kuhusu Mungu kupitia hali zisizo rasmi. Hatimaye tumeitwa kukidi mahitaji ya mwili (1 Wakorintho 12:7), lakini hiyo haimaanishi kuwa tutakuwa na huduma moja katika maisha ya kuzingatia ijiapokwa wakati mwingi hufanyika hivyo.

Wakati mwingine Mungu humpa mtu binafsi huduma maalum, lakini Yeye hufanya hivyo kwa wakati Wake mwenyewe. Kama vile kufanya mazoezi kabla ya mashindano, inachukua muda kusitawisha hekima na ustadi tunaohitaji (1 Wakorintho 3:2). Ikiwa Mungu angetupa misheni kabla ya mafunzo, tungejaribu kufanya mengi kwa muda mfupi. Badala yake Mungu hutuzuia, akichukua muda kujenga ujuzi wetu wa vitendo (Luka 2:52), ujuzi wa Kiroho (2 Petro 3:18), na imani (Yakobo 2:22). Yakobo alizungumza kuhusu hili katika Yakobo 1:2-4: “Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi timilifu, ili mpate kuwa wakamilifu, mmekamilishwa, bila kupungukiwa na kitu chochote.”

Watu wengi wana hamu ya kutaka kugundua wito wao kutoka kwa Mungu, lakini neno “wito” linapotumika katika Agano Jipya, karibu kila mara linarejelea wito wetu kama waumini (Warumi 11:29; 1 Wakorintho 1:2; Waefeso 1:18, 4; 2 Wathesalonike 1:11; 2 Timothy 1:9; Waebrania 3:1; 2 Petro 1:10), sio wito wetu kwa huduma maalum. Hatimaye, “wito” wetu ni kumpenda Mungu, kuwapenda wengine, kumtii Mungu, na kuwajali wengine. Ikiwa tutazingatia kutimiza majukumu Aliyotupa sasa, Mungu atashughulikia ushawishi wetu kwa ulimwengu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninawezaje kugundua wito wangu wa kiroho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries