settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani Yesu kuwa Mwana wa Mungu?

Jibu


Yesu si Mwana wa Mungu kulingana na ubaba wa kawaida wa binadamu. Mungu hakuoa na kupata mwana wa kiume. Mungu hakufanya tendo la ndoa na Mariamu, na pamoja naye kuzaa mtoto wa kiume. Yesu ni Mungu katika hali kwamba ni Mungu anajithirihisha kama mwili. (Yohana 1:1, 14) Yesu ni mwana wa Mungu kwa dhana kwamba Mariamu alipata mimba kupitia Roho Mtakatifu. Luka 1:35 yasema, “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.”

Wakati wa kujaribiwa kwake mbele ya viongozi wa Kiyahudi, kuhani mkuu alimtaka Yesu, “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu” (Mathayo 26:63). “Yesu akamwambia wewe umesema,’ Yesu akamwambia, wewe umesema; lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni” (Mathayo 26:64) viongozi wa Kiyahudi walimdhania kwa kukufuru (Mathayo 26:65-66). Baadaye mbele ya Pilato, “Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu” Yohana 19:7) ni kwa nini makisio yake kuwa Mwana wa Mungu yachukuliwe kuwa kufuru na astahili hukumu ya kifo? Wayahudi wilielewa vizuri sana chenye Yesu alimaanisha kwa maneno haya “Mwana wa Mungu” kuwa Mwana wa Mungu ni kuwa hali moja na Mungu. Mwana wa Mungu “wa Mungu” kusema uko katika hali sawa na Mungu-hakika kuwa Mungu- kulikuwa sawa na kukufuru kwa viongozi wa Kiyahudi; kwa hivyo walimtaka Yesu auwawe, kulingana na Mambo ya Nyakati 24:15. Waebrania 1:3 inadhihirisha haya wazi, “Yeye kwa kuwa ni mng’ao wa utukufu wake, akiisha kufanya utakaso wa dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko juu.”

Mfano mwingine unaweza patikana katika Yohana 17:12 mahali Yuda anaelezwa kama mwana wa “upotevu”? jina upotevu lamaanisha “uharibivu” Yuda hakuwa mwana wa uharibivu, lakini mambo hayo ndio ya kutambulisha maisha ya Yuda. Yuda anadhihirisha upotevu. Vile vile Yesu mwana wa Mungu. Ni Mungu anajidhihirisha (Yohana 1:1,14).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani Yesu kuwa Mwana wa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries