Swali
Ikiwa adhabu ya dhambi zetu ni Jahannamu ya milele kifo cha Yesu kililipaje adhabu yetu ikiwa hakuwa kuzimu milele?
Jibu
Ikiwa tunadhani ya Yesu ni kama mtu tu, basi swali hili ni la kawaida kuuliza. Lakini sababu Yesu hakuwa katika Jahannamu ni kwamba Yeye sio tu mtu, bali Mungu-mtu. Mtu wa pili wa Uungu alifanya mwili na kuishi kati ya wanadamu kwa namna ya mtu. Lakini alikuwa mtu wa kipekee, hakuna mwingine kama yeye, kwa sababu asili yake ilikuwa ya Mungu-mtakatifu, mkamilifu na asiye na mwisho.
Vifungu kadhaa vinathibitisha ukweli huu, kama vile kifungu cha ufunguzi katika Injili ya Yohana. Huko pale tunasoma yafuatayo:
"Hapo mwanzo Neno alikuwako, naye alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu. Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa;hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye mwana wa pekee wa Baba, amejaa neema na kweli "(Yohana 1: 1-3, 14).
Kifungu hiki kinatoa ushuhuda wazi kwamba Neno la milele, ambaye ni mzima wa milele pamoja na Mungu na kiini sawa na Mungu, alichukua mwili wa mwanadamu na akafanya makao yake ("akaweka hema lake" au "madhabau") kati yetu. Kama Mtume Paulo anasema juu ya Yesu, "Maana ndani yake Kristo katika ubinadamu wake, umo ukamilfu wote wa Mungu" (Wakolosai 2: 9).
Tukitilia maanani hayo, hebu tuangalie kwa makini zaidi swali hilo. Ni hakika kwamba adhabu ya dhambi zetu ni milele kuzimu. Biblia inasema kwamba wote wamefanya dhambi (Warumi 3:23) na kwamba mshahara wa dhambi yetu ni kifo (Warumi 6:23). Kitabu cha Ufunuo kinasema kwamba wale ambao majina yao hayako katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo watatupwa katika ziwa la moto ambako watateswa "milele na milele" (Ufunuo 20:10, 15).
Lakini je, kifo cha Yesu kinalipiaje dhambi za kila mtu aliyewahi kuishi? Hapa ndio ambapo mjadala wa Yesu kuwa Mungu-mtu anazungumziwa. Ikiwa Yesu alikuwa mtu wa kawaida (akiwa na dhambi ya wake mwenyewe), basi kifo chake hakingelipia dhambi zake mwenyewe, n ahata zaidi hakingelipia dhambi za mwingine. Lakini Yesu sio mwanadamu; Yeye ni Mungu katika mwili wa kibinadamu. Yeye kama mtu, anaweza kujishirikisha na wale ambao alijitoa nafsi yake kwa ajili yao. Yeye kama mtu asiye na dhambi, anaweza kuipia dhambi za wanadamu bila ya kwanza kulipia dhambi zake mwenyewe. Hatimaye, yeye kama Mungu, anaweza kukidhi kikamilifu ghadhabu ya Mungu inayosababishwa na dhambi zetu.
Dhambi dhidi ya Mungu wa milele lazima ipokezwe kabisa. Pengine mtu aliye na mwisho agharamie dhambi zake kwa muda usio na kipimo au Yesu wa milele agharamie dhambi hizo mara moja kwa watu wote. Hakuna chaguzi nyingine. Dhambi dhidi ya Mungu mtakatifu inahitaji kugharamiwa milele na hata milele katika Jahannamu haitapoteza ghadhabu isiyo ya mwisho ya Mungu dhidi ya dhambi. Mtu wa kipekee anaweza kuhimili ghadhabu isiyo na mwisho ya Mungu mtakatifu dhidi ya dhambi zetu. Inahitaji kiumbe kisicho na mwisho kama mbadala kwa wanadamu kukidhi ghadhabu ya Mungu. Yesu, kama Mungu-mtu, ndiye peke yake Mwokozi.
English
Ikiwa adhabu ya dhambi zetu ni Jahannamu ya milele kifo cha Yesu kililipaje adhabu yetu ikiwa hakuwa kuzimu milele?