settings icon
share icon
Swali

Inamaanisha nini kwamba Yesu alitimiza sheria, lakini hakuikomesha?

Jibu


Katika rekodi ya Mathayo ya kinachoitwa kwa kawaida Mahubiri ya Mlimani, maneno haya ya Yesu yameandikwa: "Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua torati au manabii; la, Sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie."(Mathayo 5: 17-18).

Ni mara nyingi inasemwa kwamba kama Yesu "hakukomesha" sheria, basi ni lazima bado inafuatwa. Kwa hivyo, vipengele kama vile mahitaji ya siku ya Sabato lazima yanatumika bado,pengine pamoja na mambo mengine mengi ya Sheria ya Musa. Dhana hii ina msingi katika kutoelewa kwa maneno na dhamira ya kifungu hiki. Kristo hakupendekeza hapa kwamba asili ya kutangamana kwa sheria ya Musa ingebakia kutumika milele . Mtazamo kama huo unaweza kinzana na kila kitu tunachojifunza kutoka kwa usawa wa Agano Jipya (Warumi 10: 4, Wagalatia 3: 23-25; Waefeso 2:15).

Ya umuhimu maalum katika utafiti huu ni neno "kukomesha." Linatafsiri tamko la Kigiriki kataluo, maana halisi ya "kulegeza chini." Neno ili linapatikana mara kumi na saba katika Agano Jipya.Limetumika, kwa mfano, na uharibifu wa hekalu la Wayahudi na Warumi (Mathayo 26:61; 27:40, Matendo 6:14), na kumumunyisha mwili wa binadamu wakati wa kifo (2 Wakorintho 5: 1) .Neno ili linaweza kubeba maana pana ya "kupindua," yaani, "kutoa bure, kunyang`anya mafanikio." Katika tamaduni na elimu ya Kigiriki, ilitumika kwa utangamano na taasisi, sheria, nk, kufikisha wazo la "kubatilisha ".

Ni muhimu hasa kutambua jinsi neno hili limetumika katika Mathayo 5:17. Katika mukdhada huu, "kukomesha"limewekwa kukinzana na "kutimiza." Kristo alikuja "... si kwa kukomesha, bali kutimiza." Yesu hakuja katika dunia hii kwa madhumuni ya kuwa kama mpinzani wa sheria. Lengo lake halikuwa kuzuia utimilifu wake. Badala yake, aliiheshimu sana ,akaipenda, akaitii, na kuileta kwa mafanikio. Alitimiza matamshi ya kinabii ya sheria yaliyomuhusu yeye mwenyewe (Luka 24:44). Kristo alitimiza mahitaji ya sheria ya Musa, ambayo iliitaji utiifu kamili chini ya tishio la "laana" (tazama Wagalatia 3:10, 13). Kwa maana hii,azimio takatifu la sheria litakuwa na athari ya kudumu milele. Daima itatimiza kusudi ambalo ilipewa.

Kama, hata hivyo, sheria ya Musa huzaa uhusiano huo kwa wanadamu siku hizi , katika suala la hadhi yake kisheria, basi alikutimizwa, na Yesu alishindwa katika kile alikuja kufanya. Kwa upande mwingine, kama Bwana alitimiza lengo lake, basi sheria ilitimia, na si taasisi inayotangamana kisheria siku hizi. Zaidi ya hayo, kama sheria ya Musa haikutimizwa na Kristo-na hivyo kubaki bado kama mfumo tangamano wa kisheria kwa siku hizi-basi si tu sehemu ya utangamano. Badala yake, ni mfumo wa kulazimisha kabisa. Yesu waziwazi alisema kuwa si moja "nukta au jina kuu" (mwakilishi wa alama ndogo ya hati ya Kiyahudi)itapita mpaka yote yatimie. Kwa hivyo, hakuna lolote la sheria lingeshindwa mpaka litimize madhumuni yake. Yesu alitimiza sheria. Yesu alitimiza yote ya sheria. Hatuwezi kusema kwamba Yesu alitimiza mfumo wa kafara, lakini hakutimiza mambo mengine ya sheria. Yesu alitimiza yote ya sheria, au hakuna kabisa.Maana ambayo kifo cha Yesu kinayo kwa mfumo wa kafara, pia ina maana kwa mambo mengine ya sheria.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inamaanisha nini kwamba Yesu alitimiza sheria, lakini hakuikomesha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries