settings icon
share icon
Swali

Je, Yesu alizaliwa wapi?

Jibu


Biblia inaelezea kuzaliwa kwa Yesu Kristo katika Mathayo 1:18-25; 2:1-12; Luka 1:26–38; na 2:1–20. Wakati wa uja uzito wa Mariamu, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto ya kwamba "watu wote nchini kote wahesabiwe" (Luka 2:1). Hii ilimaanisha kwamba kila mtu katika eneo la Kirumi alitakikana kurudi kwa mji wa baba zao ili kukesabiwa.

Yusufu alikuwa anaishi katika mji wa Nazareti wakati huo lakini alihitaji kusafiri kwenda kusini katika mkoa wa Yudea, "mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi" (Luka 2:4). Kwa kawaida, Yusufu aliandamana na mchumba wake Mariamu ili kuhesabiwa kama mmoja wa familia yake. Basi, wanandoa hao walienda mji mdogo wa Bethlehemu wakati wa kuzliwa kwa Yesu.

Mahali hapo panaambatana na unabii uliotabiriwa na Mika, uliotangaza kwamba Kristo atazaliwa katika Bethlehemu: "Lakini wewe Bethlehemu katika Efratha, wewe ni mdogo tu kati ya jamii za Yuda, lakini kwako kutatoka mtawala atakayetawala juu ya Israeli kwa niaba yangu,asili yake ni ya zama za kale"(Mika 5:2).

Mji huo mdogo wa Bethlehemu ulikuwa umejaa watu kwa sababu watu wengi walikua wamerudi huko kwa sababu ya shughuli ya kuhesabiwa. Hakukuwa na nafasi ya Mariamu na Yusufu katika chumba cha wageni basi walilazimika kukimbilia makazi ya wanyama. (Ingawa Biblia haijataja kamwe kuwa wanyama walikuwepo wakati wa kuzaliwa kwa Yesu, Luka anasema kwamba mtoto Yesu alilazwa katika hori la ng'ombe-kuwepo kwa hori inamaanisha kuwa wanyama walikuwepo pia.

Kihistoria, "mkahawa" iliyotajwa katika Luka 2:7 inadhaniwa kuwa aina ya hoteli ya kibiashara. Na mahali ambapo Mariamu na Yosefu walifanya makao ni katika zizi lililokuwa karibu na eneo hilo. Walakini hatujui bila shaka kwamba ndivyo ilivyokuwa kwa sababu neno la Kiyunani iliyotafsiriwa kama "mkahawa" (kataluma) linaweza pia kutafsiriwa kama "chumba cha wageni." Tafsiri hii inafanya tutafakari ikiwa ilikuwa nyumba ya kibinafsi iliyojawa na wageni, pamoja na eneo tofauti iliyotumika kuweka wanyama wa familia hiyo.

Wakati mwingine, mahali pa wanyama palikuwa chini ukilinganisha na eneo la nyumba, palikuwa pia mbali na mahali watu walikuwa wanaishi. Kwa hivyo, wakati Luka anaposema "hakukuwa na nafasi katika kataluma," pengine alimaanisha hakukuwa na nafasi katika eneo la juu zaidi, ambalo lilijaa wageni waliokuwa wanalala au familia. Matokeo ya vifusi vya mambo ya kale yanaonyesha nyumba ambazo zilikuwa na ukuta uliotenganisha mbele ya nyumba kutoka nyuma, ambapo wanyama waliwekwa. Muundo wa sakafu hizo mbili unaonyesha kuwa makazi ya wanyama ya ndani yaliyounganika na nyumba kwa njia fulani. Haijalishi, kulikuwa za zizi au kihori mahali ambapo Kristo alizaliwa na zizi hio ilitumika kama mahali pa kupumzisha mtoto Yesu, kama inavyosemwa katika Luka 2:7.

Kuna pia nadharia kwamba makazi ambapo Yesu alizaliwa ilikuwa mahali katika kaskazini mwa Mnara wa Ederi. Huo ulikuwa mnara wa zamu uliokuwa na mahali chini ambapo wachungaji walitumia wakati wa kondoo kuzaa ili kuwaweka vikondoo ambao baadaye wangetumika kama dhabihu katika hekalu la Yerusalemu. Nabii Mika ambaye alitabiri Bethlehemu kama mahali pa kuzaliwa kwa Yesu, pia alitaja Mnara wa Ederi: "Na wewe, Ee mnara wa kundi, kilima cha binti Sayuni, utajiliwa; naam, mamlaka ya kwanza yatakuja, ufalme wa binti Yerusalemu" (Mika 4:8). Nadharia hii inatumika kueleza mbona wachungaji walionekana kujua mahali pa kuangalia, wakati malaika walipotoa ishara kwamba mtoto atakuwa "amevikwa vitambaa na amelala katika zizi." Na ingefaa kwa Masihi kuzaliwa katika sehemu ile ile ambayo wanakondoo wa dhabihu walizaa.

Ikiwa eneo halisi ambapo Yesu alizaliwa palikuwa makazi ya ndani ya wanyama, ghala tofauti, au mnara uliotumika kuweka vikondoo, Biblia imeweka wazi kwamba Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, alizaliwa katika eneo duni, katika mji wa Bethlehemu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Yesu alizaliwa wapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries