settings icon
share icon
Swali

Je, Nini kitakachotokea Yesu atakaporudi?

Jibu


Ujio wa pili wa Kristo unarejelewa mara nyingi katika Maandiko, hivi kukiwa na zaidi ya vifungu 1,500 katika Agano la Kale na moja kati ya aya 25 katika Agano Jipya inayotaja kurudi kwa Masihi. Kiasi kikubwa cha taarifa zinazotolewa kwa ajili ya tukio hii muhimu hutilia mkazo yale Mungu anayosema katika kitabu cha Amosi 3:7: “Hakika Bwana Mwenyezi hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.”

Kwa muhutasari, kurudi kwa Kristo kunaleta kile kinachojulikana kama Ufalme wa Mungu katika Maandiko-utawala kamili wa Mungu juu ya uumbaji wake, ikiwa ni pamoja na wanadamu. Ili aweze kutumiza hilo, Yesu anaashiria hukumu mbili tofauti, ufufuo mbili tofauti, na umilele mbili tofauti.

Yesu atakaporudi, atakuwa tayari kwa vita ( Ufunuo 19:11-16). Mataifa yatakusanyika kupigana na Yerusalemu (Zekaria 14:2) katika kile tunachokiita vita vya Armagedoni. Lakini hiyo ndiyo siku ambayo Yesu atakaporudi: “Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, mashariki mwa Yerusalemu, nao Mlima wa Mizeituni utagawanyika mara mbili kuanzia mashariki hadi magharibi, ukifanya bonde kubwa, nusu ya mlima ukisogea kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini” (Zekaria 14:4 ). Itakuwa siku ya kipekee katika historia ya ulimwengu: “Siku hiyo hakutakuwepo nuru, baridi wala theluji. Itakuwa siku ya kipekee, isiyo na mchana wala usiku, siku ijulikanayo na Bwana. Jioni inapofika nuru itakuwepo” (Zekaria 14:6-7). Maadui wa Mungu watashindwa, na Mpinga-Kristo na nabii wa uongo “watatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti” (Ufunuo 19:20). Yesu ataanzisha ufalme wake, na “Bwana atakuwa mfalme juu ya dunia yote” (Zekaria 14:9).

Katika kuanzisha Ufalme wake duniani, kwanza Yesu ataweka hukumu kwa wale ambao bado wako hai baada ya dhiki na wale ambao wako duniani wakati wa ujio wa pili. Hii inajulikana kama “hukumu ya kondoo na mbuzi” au “hukumu ya mataifa” (Mathayo 25:31-46). Wale watakaookoka hukumu hii watasalia duniani na kufurahia wakati wa amani na ufanisi Pamoja naye Yesu kwa miaka 1,000 ( inajulikana kama milenia ; tazama Ufunuo 20:4-6). Wale wanaopatikana na hatia katika hukumu hii wanalaaniwa na kutupwa kwa “moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake” (Mathayo 25:41). Shetani amefungwa na kuzuliwa kufanya jambo lolote wakati wa milenia (Ufunuo 20:1-3).

Katika wakati huu pia kutakuwa na ufufuo wa waumini wote wa Mungu (Ufunuo 20:4-6). Waumini hawa waliofufuliwa wataungana na waumini walio hai wakati Kristo atakapokuja na wale Kristo atakaokuja nao toka mbinguni, na wote wataishi na Kristo wakati wa kipindi cha miaka 1,000 katika utawala wake duniani.

Mwishoni mwa kipindi cha milenia, Shetani ataachiliwa na vita vya mwisho vitatokea ambapo Kristo atashinda kwa upesi(Ufunuo 20:7-9). Na hapo Shetani atatupwa milele katika ziwa la moto. Katika hatua hii ufufuo wa pili utatokea na hukumu nyingine. Wale ambao sio waumini watafufuliwa ili wahukumiwe kwa kile kinaitwa hukumu kuu ya kiti cheupe; kulingana na matendo yao watatupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 20:11-15).

Kwa hivyo, ujio wa Yesu utaleta aina mbili za milele- milele ya pamoja na Mungu na milele bila Mungu. Ukweli huu umesemwa katika aya mbili katika kitabu cha Malaki: “Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na kila mtenda mabaya watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto…Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. Bali kwenu ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini” (Malaki 4:1-2).

Je! ni nini kitatokea Yesu atakaporudi? Uovu utashindwa, dunia itarejeshwa na Mungu anashidna. Itikio lako kwa ujio wa Yesu unategemea uhusiano wako naye. Itakuwa aidha uharibifu mkubwa katika historia ya mwanadamu au utimilifu wa tumaini lililobarikiwa (Tito 2:13). Imani katika Kristo ndio inaleta tofauti. “Lakini je, Mwana wa Adamu atakapokuja ataikuta imani duniani?” (Luka 18:8).

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Nini kitakachotokea Yesu atakaporudi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries