Swali
Ni namna gani Yesu na Biblia wote wanaweza kuwa Neno la Mungu?
Jibu
Kifungu, "Neno la Mungu" linaonekana mara kwa mara katika Biblia na linaeza kuwa na maana tofauti kidogo huku ikitegemea muktadha na neno la Kiebrania au Kigiriki limetumika. Yohana 1:1-2 inasema, "Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu." Hapa Neno kidogo ni Bwana Yesu. Neno lililotafsiriwa "Neno" ni logos ambalo linamaanisha "dhihirisho la wazo." Logos linaeza fikiriwa kuwa ujumbe wa Mungu kamili kwa mwanadamu (Matendo 11:1; 1Wathesalonike 2:13). Yesu alikuwa ujumbe huo kamili, na ndio sababu anaitwa "Logos," au "Neno," la Mungu (Wakolosai 1:19; 2:9).
Neno (Logos) pia limetumika mara nyingi wakati linarejelea ujumbe andhishi wa Mungu (Yohana 17:17; 1Timotheo 4:5; Ufunuo 1:2; Wakolosai 1:25). Waebrania 4:12 yasema, "Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu." Yesu alionyesha uhusiano kati ya Neno lililoandikwa la Mungu na Yeye, kwamba Yeye ndiye kiini cha Neno lililoandikwa: "Nyinyi huyachunguza Maandiko Matakatifu mkidhani kwamba ndani yake mtapata uhai wa milele; na kumbe maandiko hayohayo yananishuhudia" (Yohana 5:39).
Neno linguine la Kigiriki lililotumika kwa niaba ya "neno" ni rema (rhema" likirejelea lile neno lililosungumzwa/kuandikwa la Mungu (Waebrania 6:5). Wakati Yesu alikuwa anajaribiwa na Shetani, alijibu, "Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu" (Mathayo 4:4). Tunaambiwa katika Waefeso 6:17, "Upokeeni wokovu kama kofia yenu ya chuma, na neno la Mungu kama upanga mnaopewa na Roho Mtakatifu." Yesu alionyesha kuwa tulihitaji neno andishi la Mungu ndio tuyashinde mashambulio ya Shetani.
Kifungu "neno la Mungu" linamaanisha zaidi ya maneno yaliyochabishwa katika kurasa. Mungu ni msemaji na amekuwa kisungumza na mwanadamu tangu mwanzo. Anasungumza kupitia uumbaji wake (Zaburi 19:1), kupitia manabii wa kale (Hosea 12:10; Waebrania 1:1), kupitia kwa Roho Mtakatifu (Yohana 16:13; Matendo 16:6), kupitia kwa maandiko (Waebrania 4:12), na kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo (Yohana 14:9). Tunaweza jifunza kumjua Mungu vyema kwa kutafuta kumsikia Yeye kwa kila Njia Yeye hunena.
English
Ni namna gani Yesu na Biblia wote wanaweza kuwa Neno la Mungu?