Swali
Je! Inamaanisha nini kuwa Yesu alikuja kwa mfano wa mwili wa dhambi?
Jibu
Warumi 8:3-4 yasema, "Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho." Ili kuelewa chenye ilimaanisha kuwa Yesu "mfano wa mwili ulio wa dhambi," tunafaa kufafanua meneno kadha wa kadha.
Wakati Biblia inamrejelea kuwa "mwili" (Yohana 6:63; Warumi 8:8), mara nyingi humaanisha kuwa mazoea ya binadamu ya kufanya dhambi ambayo sisi wote hurithi kutoka kwa Adamu (Warumi 5:12). Wakati Adamu na Hawa waliamua kuasi dhidi ya amri ya Mungu, walikuwa "mwili ulio na dhambi." Katika wakati huo, dhambi ilingia katika ulimwengu kamilifu wa Mungu na ikaanza kuharibu kila kitu (Mwanzo 3). Kwa kuwa vile wanadamu wote walitoka kwa Adamu, sisi wote tumerithi hali yake ya kuanguka. Kwa hiyo kila mtu anazaliwa akiwa mwenye dhambi (Warumi 3:10, 23).
Neno mfano linamaanisha "kufanana" au "hali ya kulingana na kitu kingine." Mfano ni sio kuwa sawia katika mwili au asili, bali ni mfanano katika mwonekano. Mfano ni picha ya kitu asili. Kwa mfano, sanamu zinatengenzwa katika mfano wa ndege na Wanyama na vitu vilivyoumbwa (Warumi 1:22-23; Kutoka 20:4-5). Picha iliyopigwa ni mfano. Wafilipi 2:6-8 yamwelezea Yesu kuweka kando manufaa aliyokuwa nayo ya kiungu kama Mungu na kuuchukua mwili wa manadamu ambaye aliumba (ona pia Yohana 1:3). Walakini, Yesu hakuwa na baba wa daunia, kwa hiyo hakurithi dhambi ya asili kama vile wanadamu wengine wote hufanya (Luka 1:35). Alichukua mwili wa mwanadanu, huku akibaki na uungu wake wote. Aliishi maisha tunayoishi, akateseka vile tunavyoteseka, na akajifunza na kukua vile twajifunza na kukua, lakini alifanya hayo yote bila dhambi (Waebrania 4:15;5:7-8). Kwa sababu Mungu alikuwa Baba Yake, aliishi tu kwa mfano wa mwili ulio na dhambi. Yesu alirithi mwili wa nyama kutoka kwa mama yake, Mariamu, lakini sio dhambi kutoka kwa Yusufu.
Yesu alikuwa mwanadamu ili awe njia yetu mbadala. Katika mwili Wake, ilibidi ateseke uchungu wa mwili, hisia, kukataliwa, utengano kiroho na Mungu (Mathayo 27:46; Marko 15:34). Aliishi maisha wanadamu huishi, lakini alifanya hivyo namna ilie tulistahili kuishi-katika uhusiano kamilifu na Mungu mtakatifu (Yohana 8:29). Kwa sababu alikuja katika mfano wa mwili ulio na dhambi, basi angejiwakilisha kama dhabihu ya mwisho iliyotosha kulipia dhambi za wanadamu wote (Yohana 10:18; Waebrania 9:11-15).
Ndiposa upokee karama kamili ya msamaha wa Mungu, kila matu lazima amuruhusu Yesu kuwa njia mbadala. Hii inamaanisha kuwa tuje kwake kwa imani, tukitambua kuwa, kwa sababu alikuja katika mfano wa mwili wa dhambi, alisulubiwa, na kuzichukua dhambi za ulimwengu, dhambi zetu zinaweza kulipwa kwa ukamilifu (2 Wakorintho 5:21). Mwili wetu wa dhambi umesulubiwa naye ili tuwe huru kumfuata Roho katika utiifu kamili kwa Mungu (Warumi 6:6-11; Wagalatia 2:20). Wakristo ni wale ambao wamepata kuhesabiwa kifo cha Kristo na ufufuo wake, hivyo deni yao kwa Mungu imefutiliwa mbali (Wakolosai 2:14). Kwa sababu ya msamaha wake kamili, Wakristo kila siku wanajihesabu kuwa wafu kwa mwili wao wa dhambi. Tangu Kristo alishinda dhambi na kifo katika mwili wake, tunaweza kuishi katika nguvu ya Roho wake, ambaye atashinda dhambi na kifo kwa wale wote wanaoamini katika Kristo (Wagalatia 5:16, 25; Warumi 8:37).
English
Je! Inamaanisha nini kuwa Yesu alikuja kwa mfano wa mwili wa dhambi?