Swali
Yesu alilipa fidia yetu aje na kwa nani?
Jibu
Fidia ni kitu kinacholipwa ili kutoa kuajiliwa kwa mtu aliyemateka. Yesu alilipa fidia yetu kutuokoa kutoka kwa dhambi, kifo, na kuzimu. Katika vitabu vya Kutoka, Mambo ya Walawi, Hesabu, na Kumbukumbu la Torati hupatikana mahitaji ya Mungu ya dhabihu. Katika nyakati za Agano la Kale, Mungu aliwaagiza Waisraeli kutoa dhabihu za wanyama kwa ajili ya upatanisho badala; yaani, kifo cha wanyama kilichukua kifo cha mtu, kifo kuwa adhabu ya dhambi (Warumi 6:23). Kutoka 29: 36a inasema, "Kila siku lazima utoe ng'ombe mchanga kama sadaka ya upatanisho wa dhambi."
Mungu anataka utakatifu (1 Petro 1: 15-16). Sheria ya Mungu inataka utakatifu. Hatuwezi kumpa Mungu utakatifu kwa sababu ya dhambi tunazofanya (Warumi 3:23); Kwa hiyo, Mungu anataka kuridhika kwa Sheria yake. Kutolea dhabihu kuridhisha mahitaji yake. Hapo ndipo Yesu anakuja ndani. Waebrania 9: 12-15 inatuambia, "Wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. Kwa maana, ikiwa damu ya mbuzi na mafahali na majivu ya ndama ya ng'ombe waliyonyunyiziwa wenye uchafu hutakasa hata kuusafisha mwili; basi si Zaidi damu yake Kristo, ambaye kwamba kwa Roho wa milelenalijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa na sadaka isiyo na mawaa, itawasafisha dhamiri zenu na matendo mafu, mpate kumwaabudu Mungu aliye hai? Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya, ili, mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makossa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi ya urithi wa milele."
Pia, Warumi 8: 3-4 inasema, "Maana yaliyowezekana kwa Sheria, kwa vile ilivyokuwa dhahifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. "
Kwa wazi, Yesu alilipa fidia kwa ajili ya maisha yetu kwa Mungu. Fidia hiyo ilikuwa maisha yake mwenyewe, kumwaga damu yake mwenyewe, dhabihu. Kwa sababu ya kifo chake cha dhabihu, kila mtu duniani ana nafasi ya kukubali zawadi hiyo ya upatanisho na kusamehewa na Mungu. Kwa maana bila ya kifo chake, Sheria ya Mungu ingehitaji bado kukamilika-kwa kifo chetu wenyewe.
English
Yesu alilipa fidia yetu aje na kwa nani?