Swali
Inamaanisha nini kuwa Yesu ni mtetezi wetu?
Jibu
Mtetezi ni mtu ambaye huja kwa usaidizi wetu au kutoa udhuru wa shitaka letu mbele ya hakimu. Wakili hutoa msaada, nguvu, na ushauri na kutuombea wakati kunahitajika. Biblia inasema kwamba yesu ni mtetezi wa wale ambao wameweka Imani yao Kwake: "Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa" (1 Yohana 2:1). Katika aya zingine, Yesu anamwita Roho Mtakatifu mtetezi wetu (Yohana 14:16, 26; 15:26; 16:7). Neno la Kigiriki lililotumika katika aya hizo ni parakleton (parakiletoni) ambalo humaanisha "msaidizi, mshauri, mwonya."
Katika mfumo wa mahakama za mwanadamu, wakili hutetea haki za mteja wake. Wakili wa sheria au mwalimu wa sheria/mnenezi wamesomea sehemu nyingi za sheria na mara nyingi wanaweza kuongoza zile sehemu ngumu kwa usahihi na uhakika. Hiyo ndiyo taswira Yohana anatupa wakati anamrejelea Yesu kama "Mwombezi kwa Baba." Sheria thaki ya Mungu hututamka kuwa na hitia katika makosa yote. Tumeasi kanuni za Mungu, tukaikataa haki yake ya kuyatawala maisha yetu, na tukaendelea kutenda dhambi hata baada ya kufahamu ukweli (Waebrania 10:26; Warumi 1:21-23; 1 Timotheo 2:4). Adhabu pekee ya haki kwa uovu kama huo ni kuzimu ya milele (Ufunuo 14:10; 21:8; 1Wakorintho 6:9).
Yesu ndiye wakili kati ya moyo wetu wa kutubu na sheria. Ikiwa damu yake imetumika katika maisha kwa imani na kumkiri Yeye kuwa Bwana wetu (Warumi 10:9-10; 2 Wakorintho 5:21), atatetea kesi yetu mbele za Hakimu mwenye haki. Tuneweza waza masungumzo yakienda kama hivi: "Baba ninajua kuwa huyu ametedna dhambi na kuasi amri zetu. Yeye ana hatia vile amehukumiwa. Haki yaki ilitumika kwa makosa yake wakati aliniamini kwa wokovu na msamaha. Nimelipa gharama, ili aweze kutangazwa kuwa 'Hana hatia.' Hakuna deni ambayo imebaki kwake yeye kulipa" (Warumi 8:1; Wakolosai 2:14).
Yesu ni mtetezi/wakili wetu wakati Mungu ametukubali kwanza katika familia Yake kama watoto wake (Yohana 1:12). Na anabaki kuwa mtetezi wetu milele yote.Yohana wa Kwanza 1:9 inasema kuwa, wakati tunakiri dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na mwenye haki kusizamehe dhambi zetu na kututakaza kutoka kwazo. Kama wafuasi wake, bado tutaendelea kutenda dhambi. Lakini, tunapofanya dhambi, tumeamrishwa kukiri dhambi hiyo kwa Mungu. Kukiri ni kukubaliana na Mungu kuhusu jinsi dhambi hiyo ilivyo mbaya. Tunasimama na hatia mbele zake bila ubishi wowote na bila haki yetu wenyewe. Mtetezi wetu anasimama mbele ya Hakimu, na Pamoja wanakubaliana kwamba, kwa sababu tuko "ndani ya Kristo," hakuna haja ya adhabu zaidi. Tayari Yesu amekwishatoa dhamana ya kutosha ya kutukomboa.
Hali ingine inayomfanya Yesu kuwa mtetezi wa huruma ni hoja kwamba amewahi ishi maisha ya ulimwengu huu. Amewahi jaribiwa, kukataliwa, kudharauliwa, kutoeleweka, na kudhulumiwa. Yeye hatuwakilishi kinadharia; bali Yeye hutuwakilisha kwa uzoefu. Aliishi maisha tuanayoishi, na bado alifanya hivyo bila kutumbukia katika maovu yanayotupata. Kwa ushindi alikataa kushindwa na majaribu na sasa anaweza kuwa Kuhani wetu Mkuu kwa sababu kikamilifu alitimiza sheria ya Mungu (Waebrania 4:15; 9:28; Yohana 8:29). Mtetezi wetu anaweza kutete kesi zetu kutokana na mazoea, mfano wa hali kama hii: "Baba, huyu dada mdogo amekaidi amri yetu yenye haki, lakini anakupenda na anatamani sana kukutumikia. Ninakumbuka vile ilivyo kuwa kujaribiwa hivyo, na moyo wangu umeguzika naye. Ameikiri dhambi hii na anatamani kugeuka kutoka kwayo. Kwa sababu ya dhabihu yangu, unaweza kusamehe dhambi hii na kuutakaza moyo wake mara nyingine tena. Hebu na tumfunze jinsi ya kuruhusu Roho Mtakatifu kumfariji na kumtia nguvu ya kuping majaribu wakati mwingine."
Wakili wetu wa dunia anaweza tu kutetea kesi yetu kutokana na ushahidi unaonekana au mashahidi. Mtetezi wetu wa mbinguni anajua mioyo yetu na anatetea kesi zetu kwa msingi wa kile kilichoko (Luka 5:22; Marko 2:8). Pia anajua ugumu wa mfumo wa sheria za Mungu. Amekwisha toshelesha mahitaji ya haki, kwa hiyo uwakili wake ni kutoka kwa kiwango cha nguvu na haki. Mungu anakubali utetezi wa Mwanawe kwa niapa yetu kama mojawapo ya makubaliano yao ya kiungu yaliyoanzishwa kabla dunia kuumbwa (1Petro 1:20; Yohana 17:24; Ufunuo 13:8). Nafasi yetu kama "wenye haki wa Kristo" ii salama kwa sababu yule aliyetununulia nafasi hiyo kwa damu yake mwenyewe yeye pia ni mtetezi wetu (Warumi 4:25; 8:3; 1Wakorintho 1:30).
English
Inamaanisha nini kuwa Yesu ni mtetezi wetu?