Swali
Je! Yesu ana mwili halisi mbinguni?
Jibu
Kufufuliwa kwa mwili kwa Yesu ni ngunzo kuu kwa kanuni ya Kikristo na tumaini letu la mbinguni. Kwa sababu Yesu alifufuka kutoka kwa wafu na mwili wa nyama, kila mkristo ana uhakikisho wa kufufuliwa na mwili wa kibinafsi (Yohana 5:21,28; Warumi 8:23). Na sasa Yesu yuko mbinguni, mahali anachukuliwa kuketi katika mahali pa mamlaka, katika mkono wa kuume wa Mungu (1Petro 3:22). Lakini je! mwili wa Yesu uliye mbinguni unafana na ule wa kidunia?
Biblia ii wazi kuwa mwili wa Yesu ulifufuliwa. Kaburi lilikuwa wazi. Alitambulika na wale waliomjua mbeleni. Yesu alijionyesha mwenyewe kwa wanafunzi wake wote baada ya ufufuo wake, na zaidi ya watu mia tano walishuhudia uwepo wake wa ufufuo duniani (1Wakorintho 15:4-6). Katika Luka 24:16, njiani kuelekea Emau, wawili wa wanafunzi wake "walizuiliwa kumtambua [Yesu]." Ingawa, baadaye, "Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua" (aya ya 31). Sio kwamba Yesu hangeweza kutambulika; ni kwamba kwa nguvu ya kiasili wanafunzi kwa muda walizuiliwa kumtambua.
Baadaye katika mlango huo huo wa Luka, Kristo anaiweka wazi kwa wanafunzi wake kuwa ana mwili wa nyama; Yeye si kivuli cha roho: "Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkaone, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo" (Luka 24:39). Baada ya Yesu kukaa na wanafunzi wake siku arobaini, alipaa kwenda mbinguni na mwili (Matendo 1:9). Yesu bado ni mwanadamu, na sasa hivi ana mwili wa kibinadamu mbinguni. Mwili wake ni tofauti, ingawa; mwili wa nyama wa kidunia inaharibika, lakini miili ya mbinguni haiaribiki (1Wakorintho 15:50). Yesu ana mwili halisi, ulio tafauti na mingine. Mwili wake uliofufuliwa umebuniwa kutokana na mtazomo wa milele.
Wakorintho wa Kwanza 15:35-49 inaelezea jinsi mwili wa mkristo utakuwa mbinguni. Mili yetu ya mbinguni itakuwa tofauti na ile ya duniani kwa umbo, kwa uzuri, katika nguvu, na kwa muda mrefu. Mtume Paulo pia anasema kuwa mwili wa muumini utakuwa mfano wa mwili wa Kristo (aya ya 49). Paulo anasungumzia suala hili tena katika 2 Wakorintho, ampabo analinganisha miili ya dunia na hema na miili ya mbinguni kuwa makao ya mbinguni (2 Wakorintho 5:1-2). Paulo anasema kwamba, pindi hizi hema za dunia zinatoweka, Wakristo hawataachwa "uchi"-hiyo ni kusema kuwa, bila mwili wa kuishi (2 Wakorintho 5:3). Wakati mwili mpya umevaliwa tutatoka katika hali ya kuharibika hadi hali ya kutoharibika. (2 Wakorintho 5:4).
Kwa hivyo, tunajua kwamba Wakristo watukuwa na mwili wa mbinguni kama "mwili wa utukufu" wa Yesu (Wafilipi 3:21). Katika utwalizi wake Yesu alichukua mwili wa binadamu, na katika ufufuo wake mwili wake ulitukuka-ingawa bado alikuwa na kovu (Yohana 20:27). Milele atakuwa Mungu-mwanadamu, aliyetolewa dhabihu kwa ajili yetu. Kristo, muumbaji we ulimwengu, milele atajishusha hadi kiwango chetu, na atajulikana kwetu mbingu kwa mfano uanaoguzika ambao tunaweza kuuona, kumsikia, na kumguza (Ufunuo 21:3-4; 22:4).
English
Je! Yesu ana mwili halisi mbinguni?