settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Yesu alipitia mateso mengi?

Jibu


Isaya 52:14 yasema, “Kama vile wengi walivyokustaajabia, uso wake ulikuwa umeharibiwa san zaidi ya mtu ye yote, na umbo lake zaidi ya wanadamu.” Yesu aliteswa sana katika kipindi chote cha majaribu, mateso, na kusulubiwa (Mathayo 27, Marko 15, Luka 23; Yohana 19). Vile mateso yake ya mwili yalikuwa ya kutisha sio jambo linaloweza linganishwa nay yale mateso aliyoyapitia kiroho. 2 Wakorintho 5:21 inasema, "Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye”. Yesu aliubebaa mzigo wa dhambi ya dunia nzima juu yake (1 Yohana 2:2). Ilikuwa dhambi ambayo ilimfanya Yesu kupiga kelele, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?" (Mathayo 27:46). Hivyo, vile mateso ya Yesu mwilini yalikuwa ya kikatili, sio kitu ikilinganishwa na kule kuchukua dhambi zetu na kufa kwa kulipa adhabu kwa ajili yao ( Warumi 5:8).

Isaya anatabiri mateso ya Yesu katika lugha wazi: "Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakikia ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni zetu; Lanini tulimdhania ya kuwa amepigwa, na Mungu, na kuteswa. Bali aliejeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu; adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona” (Isaya 53:3, 5). Zaburi 22:14-18 ni kifungu kingine chenye nguvu kinachotabiri mateso ya Masihi : "Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya mtima wangu. Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; unaniweka katika mavumbi ya mauti. Kwa maana mbwa wamenizunguka; kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenizua mikono na miguu. Naweza kuihesabu nifupa yangu yote; Wao wananitizama na kunikodolea macho. Wanagawanya nguo zangu, Na vazi langu wanalipigia kura.”

Ni kwa nini Yesu aliweza kuteseka vibaya hivyo? Baadhi yaw engine wanadhani kwamba mateso ya kimwili ya Yesu yalikuwa ni sehemu ya adhabu yake kwa dhambi zetu. Kwa kiasi fulani, hii ni kweli. Wakati huo huo, mateso ambayo Yesu alyapitia yanaongea zaidi juu ya chuki na ukatili wa mwanadamu zaidi kuliko adhabu ya Mungu kwa ajili ya dhambi. Chuki ya Shetani kamili kwa Mungu na Yesu ilikuwa hakika sehemu ya motisha ya mateso na kuendelea bila kufa moyo katika unyanyasaji. Mateso aliyokusanyiwa ya Yesu ni mfano wa mwisho wa chuki na hasira mtu mwenye dhambi anahisi mka Mungu mtakatifu (Warumi 3:10-18).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Yesu alipitia mateso mengi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries