settings icon
share icon
Swali

Je! Yesu alizungumza katika ndimi?

Jibu


Biblia haitupi Ushahidi wowote kuwa Yesu aliongea katika ndimi. Wengi hii leo huona "ndimi" kama aina fulani ya upumbavu, usemi uwio wa kawaida. Kibiblia, karama ya kuongea katika ndimi hutokea wakati mtu huongea lugha yenye haelewi ili kumfundisha mwingine ambaye anaongea lugha hiyo (1 Wakorintho 14:6).

Ikiwa Kristo alikuwa anaenda kuongea katika ndimi, ingekuwa mwafaka ikiwa angefanya hifo katika ubatizo wake wakati "Roho alishuka juu yake kama hua" (Marko 1:10). Tunajua kwamba muda mfupi baada ya Yesu kubatizwa, Baba aliongea kutoka mbinguni katika maneno ambayo wote wangeelewa (aya ya 11), lakini hatuna rekodi yeyote ya Yesu akiongea katika ndimi katika hili au ama katika matukio mengine.

Waungaji mkono wa ndimi huchukulia kuwa lazima Yesu aliongea katika ndimi. Ili kuunga hoja yao, wao hutaja vifungu kama Marko 7:34 ambamo kwamba "Yesu akatazama mbinguni, akavuta hewa ndani kwa nguvu." Walakini kuvuta hewa kwa nguvu sio sawa na karama ya ndimi isiyo ya kawaida. Mtu yeyote anaweza hema, kwa sababu nyingi sana, lakini huo sio ushahidi wa nguvu ya Roho.

Tuko na rekodi za Yesu akiongea Kiaramaiki, lugha iliyozungumzwa na wengi Israeli wakati huo (ona Marko 5:41 na Matendo 26:14). Kuna uwezekano kuwa alikuwa anajua Kiyahudi na Kigiriki, jinsi lugha zote mbili zilitumika pia. Lakini ikiwa Yesu alizungumza au hakuzungumza kwa nguvu isiyo ya kawaida katika lugha nyingine, Biblia haisemi hayo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yesu alizungumza katika ndimi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries