Swali
Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?
Jibu
Yesu hakunakiliwa mahali popote katika biblia akisema, “Mimi ni Mungu.” Lakini hiyo haimaanishi ya kwamba hakusema kuwa yeye ni Mungu. Kwa mfano ni maneno ya Yesu katika Yohana 10:30, “ Mimi na Baba yangu ni mmoja.” Kwa mtazamo wa kwanza, hili linaweza kuwa si dai la kuwa Mungu. Lakini angalia mapokezi ya ujumbe huu kwa wayahudi, “hatukupigi mawe kwa lengine lile ila kufuru, kwa sababu wewe ni mwanadamu, unayejidai kuwa Mungu” (Yohana 10:33). Wayahudi walielewa matamshi ya Yesu kuwa alijijulisha kwao kuwa yeye ni Mungu. Katika aya zifuatazo hawasahihishi wayahudi kwa kusema, “si kusema mimi ni Mungu.” Hii ina maana ya kuwa aliposema haya yafuatayo alikuwa akimaanisha kweli kuwa ni Mungu, “Mimi na Baba yangu ni mmoja” (Yohana 10:30). Yohana 8:58 ni mfano mwingine. Yesu akasema, Amini, Amini nawaambia, kabla ya Abrahamu kuweko mimi nilikuwa.” Tena kwa ajili ya hayo wayahudi wakashika mawe ili wampige nayo Yesu (Yohana 8:59). Je, wayahudi wangetaka kumpiga mawe yesu kama haingekuwa ya kuwa alisikika akikufuru kwa kusema yeye ni Mungu?
Yohana 1:1 inasema “Neno alikuwa Mungu”. Yohana 1:14 inasema “Neno akafanyika mwili.” Hii inaonyesha wazi ya kwamba Yesu ni Mungu katika mwili. Matendo 20:28 inatuambia, “…Muwe wachungaji wa kanisa la Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe,” Ni nani aliyelinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe? Yesu kristo. Matendo 20:28 inasema ya kwamba Mungu alilinunua kanisa kwa damu yake mwenyewe. Kwa hivyo Yesu ni Mungu!
Tomaso mwanafunzi wa Yesu alisema kuhusu Yesu, “Bwana na Mungu wangu” (Yohana 20:28). Yesu hamsahihishi kwa kuyasema haya. Tito 2:13 inatuhimiza kusuburi kurudi kwa Mungu wetu na mwokozi – Yesu kristo (Pia tazama petro wa pili 1:1). Waebrania 1:8, Baba asema juu ya Yesu, “Lakini juu ya mwana asema haya, “Na Kiti chako cha enzi, wewe Mungu, Kitadumu milele, na haki itakuwa fimbo ya ufalme wako.”
Katika kitabu cha ufunuo wa Yohana, Malaika alimwamuru mtume Yohana kumuabudu Mungu tu(ufunuo wa Yohana 19: 10). Mra nyingi Yesu katika maandiko aabudiwa (Mathayo 2;11; 14:33; 28:9,17; Luka 24:52; Yohana 9:38). Hakemei watu kwa kumuabudu. Kama Yesu hakuwa Mungu, angewaambia watu wasimuabudu, kama vile malaika alivyofanya. Kuna aya nyingi za maandiko zinazoshuhudia ya kwamba Yesu ni Mungu.
Sababu muhimu ya kwamba Yesu sharti awe Mungu ni kwamba kama si Mungu, kufa kwake hakungetoshea kufidia dhambi za ulimwengu wote (Yohana wa kwanza 2:2). Mungu pekee ndiye angeweza kulipia adhabu kama hiyo. Mungu pekee ndiye angeweza kufidia dhambi za ulimwengu wote w (Wakorintho wa pili 5: 21), afe na afufuke kuthibitisha ushindi juu ya dhambi na mauti.
English
Je, Yesu ni Mungu? Je, Yesu alitoa madai ya kuwa yeye ni Mungu?