settings icon
share icon
Swali

Ni namna gani Yesu ni mkuu kuliko watu mashuhuri katika historia?

Jibu


Biblia inamwakilisha Yesu kuwa mkuu kuliko wale wote walioishi mbele Yake na wale watakaokuja baada yake. Wakolosai 1 inaiweka wazi kwa njia inayoeleweka mafunzo ya ukuu wa Kristo "kwa kila kitu" (Wakolosai 1:18). Waefeso 1:22 inasema, "Mungu ameweka vitu vyote chini ya miguu yake, akamkabidhi kwa kanisa akiwa mkuu wa vitu vyote."

Yesu ni mkuu kuliko viumbe vyote. Kama muumbaji wa vitu vyote, lazima awe mkuu. Yesu alidhihirisha mamlaka Yake juu ya viumbe wakati alituliza mawimbi makali (Marko 4:39), alizidisha mikate na samaki (Marko 8:6-9), aliwafungu macho vipovu (Marko 8:22-25), na alitembe juu ya maji (Marko 6:48). "Maana kwake vitu vyote viliumbwa kila kitu duniani na mbinguni" (Wakolosai 1:16).

Yesu ni mkuu kuliko Ibrahimu. Baba Ibrahimu alikuwa na bado ni mmoja wa watu ambao wemeheshimika sana katika historia. Wakati mmoja wakati Yesu alipokuwa anasungumza na Wayahudi kuhusu kizazi chao, walimuuliza, "Wewe u mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu, ambaye amekufa?" (Yohana 8:53). Jibu la Yesu lilikuwa la kustaajabisha, "Ibrahimu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi…Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko (Yohana 8:56,58).

Yesu ni mkuu kuliko Yakobo. Mzee mwingine mkuu ni Yakobo, ambaye pia aliitwa "Israel" (Mwanzo 32:28). Yesu alipokuwa akihojiana na mwanamke katika kisima cha Yakobo huko Samaria, alimwambia kuwa ataweza kumpa "maji ya uzima" (Yohana 4:10). Mwanamke alifikiria kuwa alikuwa anamaanisha maji mengine ya kisima, akauliza, "Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo?" (aya ya 12). Yesu alimjibu kwa kulinganisha zawadi iliyoonekana ya Yakobo na zawadi ya maisha Yake ya milele: "Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele" (aya ya 13-14).

Yesu ni mkuu kuliko Musa. Kuna uwezekano kuwa hakuna nabii katika Aga la Kale aliyeheshimika sana kuliko Musa. Alikuwa mtoa sheria na mkombozi wa Israel, na mtenda miujiza. Musa alikuwa na bahati ya kipekee ya kunena na Mungu "uso kwa uso, kama vile mtu asemavyo na rafiki yake" (Kutoka 33:11). kabla afe, Musa aliwaamuru Waisraeli kutizamia kuja kwa nabii mwingine ambeye atakuwa na nembo kama ya Musa: "msikilizeni yeye" (Kumbukumbu 18:15). Yesu alitimiza sheria (Mathayo 5:17), alitukomboa kutoka dhambi na kifo (Warumi 8:2), na hakika alikuwa mtenda miujiza (Matendo 2:22). Waebrania 3:3 yasema kwamba "Lakini Yesu anastahili heshima kubwa kuliko Musa."

Yesu ni mkuu kuliko Daudi. Katika siku za Yesu jina la heshima la masiha kuwa "Mwana wa Daudi" lilikuwa la kawiada ona (Mathayo 9:27). utumiaji wa hili jina wa Wayahudi kulionyesha imani yao katika unabii, kuwa Masiha atatoka katika uzao wa Daudi (2 Samueli 7:16). katika masungumzo pale hekaluni, Yesu alinukuu Zaburi 110:1, akionyesha kuwa Daudi alimwita Masiha "Bwana wangu" (Mathayo 22:45). Mwana wa Daudi kwa hivyo ni mkuu kuliko Daudi na ako na uzao ulio mkuu kuliko ule wa kifalme hapa duniani.

Yesu ni mkuu kuliko Sulemani. Mfalme Sulemani hakuwa na mwingine aliye kuwa na hekima, utajiri, nguvu na raha (1Wafalme 10:23-24). falme kutoka ulimwenguni kote walisulu Yerusalem wakati wa utawala wa Sulemani na kumpa heshima kuu. Na bado Yesu alisema, "na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani" (Mathayo 12:42).

Yesu ni mkuu kuliko Yona. Nabii Yona alikuwa kiungo muhimu katika uamsho mmoja mkuu katika historia. Chini ya uhubiri wake, mji wote wa Nineva ulitubu dhambi zao na kumrudia Mungu ili wahurumiwe. Taifa lililojulikana kwa sanamu na ukatili walinyenyekea mbele za Mungu and kugeuka toka ibada ya sanamu. Na bado Yesu alisema, "Na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yona" (Mathayo 12:41).

Yesu ni mkuu kuliko Yohana mbatizaji. Yesu alisema kwamba Yohana mbatizaji alikuwa "aliye zaidi ya nabii" na "hakuna aliye mkuu kuliko Yohana" (Luka 7:26,28). Hakika, Yohana alikuwa nabii wa mwisho wa kizazi cha Agano la Kale, alitimiza Malaki 3:1, na aliona nguvu sawia na za Eliya (Luka 1:17). Lakini Yohana alikuwa na mtizamo gani kwa Yesu? Utabiri wake unaonyesha ni nani aliye mkuu: "Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama kuilegeza gidamu ya viatu vyake" (Marko 1:7). Kwa maneno mengine, Yohana hakuwa kitengo kimoja na Yesu. Yohana alibatiza kwa maji, lakini Yesu atabatiza na Roho Mtakatifu (Marko 1:8).

Yesu ni mkuu kuliko hekalu. Hekalu kule Yerusalem palikuwa mahli patakatifu, ulikuwa umejawa historia, umuhimu, na madhara ya kidini (angalia Mathayo 24:1). huku Yesu aliwaambia Mafarisayo, "Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko haekalu" (Mathayo 12:6). hekalu ilikuwa ni mahali ambapo kuhani mkuu alikua anamwomba Mungu, na huduma ya Yesu ya uombezi ni kuu zaidi (Waebrania 8:6).

Yesu ni mkuu kuliko Sabato. Ishara ya agano la Musa ilikuwa kuitunza Sabato (Ezekieli 20:12), na Wayahudi walikuwa makini katika kutunza hii ishara. Wakati Yesu alikuja, aliishi chini ya sheria (Wagalatia 4:4), alitimiza sheria (5:17), na akaonyesha kuwa "Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato"

Yesu ni mkuu kuliko kanisa. Kanisa ni mteule wa Mungu ambaye ameitwa toka ulimwenguni, amekombolewa na kufanywa haki, kutakazwa na kutukuka (Warumi 8:30). hatimaye kanisa itakuwa "lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa" (Waefeso 5:27). Bado Kristo ni mkuu. Yeye ndiye kichwa cha kanisa, ambayo ni mwili wake (Wakolosai 1:18; cf Yohana 13:16; 15:20).

Yesu ni mkuu kuliko malaika. Malaika ni watumishi wa Mungu, lakini Yesu ndiye mwana pekee wa Mungu, ameketi mkono wa kuume na Mungu mkuu (Waebrania 1:3,5 Yohana 3:16). Siku moja mamlaka yote nguvu zote mbinguni na duniani sitapiga magoti mbele ya Kristo (Wafilipi 2:10). Yesu ni "amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao" (Waebrania 1:4).

Jina la Yesu ni kuu kuliko majina yote. Yesu mwanadamu kamili na dhabihu pekee ya dhambi ameinuliwa juu. Mungu amempa "akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina" (Wafilipi 2:9). majina mengine ya historia- Budha, Mohammed, Gandhi, Confucius, Krishna, Joseph Smith, na Sun Myung Moon na mengineyo- hayana umuhimu wowote ikilinganishwa na utukufu wa Yesu Kristo. Ndilo jina hilo la Kristo ambalo tunahubiri hadi mwisho wa dunia, kwa sababu ni kupitia kwake tunapata wokovu (Matendo 4:12).

"Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili" (Wakolosai 2:9). Kama neno la Mungu (Yohana 1:1), Yesu ni ufunuo kamili kutoka kwa Mungu kwa mwanadamu. Hakuna njia nyingine ambayo Mungu angesungumza wazi wazi ila tu Yeye.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni namna gani Yesu ni mkuu kuliko watu mashuhuri katika historia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries