Swali
Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya kunifikisha Mbinguni?
Jibu
Ndiyo, Yesu ndiye njia ya pekee ya kukufikisha Mbinguni. Hatakama hiyo kauli yawezaleta makwazo katika kizazi hichi cha kisasa kila waisikiapo, lakini kweli yake haibadiliki. Biblia yafundisha kwamba hakuna namna yoyote ile mtu aweza kuokolewa isipokuwa kupitia kwa Yesu Kristo. Yeye mwenyewe alisema katika Yohana 14:6, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi” (TMP). Huo mstari haufundishi kuwa Kristo ni moja ya njia kati ya nyingi za kufika kwa Baba, bali yeye ndiye njia ya pakee ya kumfika Baba. Hakuna mtu, hatakama anaheshima kubwa kiasi gani, au amefanikiwa sana, au ana elimu ya juu, au anamatendo mengi matakatifu, atakayeweza kumfikia Mungu Baba bila kumpitia Yesu.
Kuna sababu kadhaa za Yesu kuwa njia ya pekee ya kukufikisha Mbinguni. Yesu ndiye “aliyeteuliwa na Mungu” awe mwokozi (1 Petro 2:4, KCV). Yesu pekee ndiye aliyeshuka chini toka mbinguni na kupaa kurudi mbinguni (Yohana 3:13). Yeye pekee ndiye aliyefanikiwa kuishi maisha makimilifu yasiyo na dhambi (Waebrania 4:15). Yeye pekee ndiye dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu (1 Yohana 2:2, Waebrania 10:26). Yeye pekee ndiye aliyekamilisha Torati ya Mungu na kile manabii walichonena (Mathayo 5:17). Yeye ndiye mtu wa pekee aliyeshinda mauti milele (Waebrania 2:14-15). Yeye pekee ndiye Mpatanishi kati ya Mungu na mwanaadamu (1 Timotheo 2:5). Yeye ndiye mtu ambaye Mungu ame “mtukuza juu sana” kuliko watu wote (Wafilipi 2:9, KCV).
Mara kadhaa, Yesu alizungumza juu ya Yeye kuwa njia ya pekee ya kufika Mbinguni tofauti na Yohana 14:6. Katika Mathayo 7:21-27, Yeye alijidhihirisha kuwa chanzo cha imani yetu. Sehemu nyingine alisema Maneno yake ni uzima (Yohana 6:63). Akaahidi kwa yeyote atakeyemwamini anao uzima wa milele (Yohana 3:14-15). Kuwa yeye ndiye mlango wa kondoo (Yohana 10:7); ndiye chakula cha uzima (Yohana 6:35); na ndiye ufufuo (Yohana 11:25). Hakuna mtu awezaye kujipa vyeo vyote hivyo.
Mafundisho ya mitume ililenga katika kifo na ufufuo wa Bwana Yesu. Petro, wakati akizungumza na Baraza kuu la Wayahudi (yaani Sanhedrini), aliwatangazia wazi kwamba Jesu ndiyo njia ya pekee ya kufika mbinguni: “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.” (Matendo 4:12, TMP). Paulo wakati akihubiri kwenye sinagogi kule Antiokia, alimlenga yesu pekee kama mwokozi: “Kwa hiyo ndugu zangu, nataka ninyi mjue kwamba kwa kupitia huyu Yesu msamaha wa dhambi unatangazwa kwenu. Kwa kupitia yeye, kila mtu amwaminiye anahesabiwa haki kwa kila kitu ambacho asingeweza kuhesabiwa haki kwa sheria ya Musa.” (Matendo 13:38-39, KCV). Yohana akiliandika kanisa kwa ujumla, alikazia kwamba jina la Kristo ndiyo msingi wa msamaha wetu wa dhambi: “Nawaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu, kwa ajili ya Jina lake.” (1 Yohana 2:12, TMP).
Uzima wa milele kule mbinguni wawezekana tu kupitia Kristo. Yesu alisali hivi, “Na uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.” (Yohana 17:3, TMP). Kupokea wokovu, kama zawadi ya bure toka kwa Mungu, ni lazima tumtazame Yesu, na Yesu peke yake. Ni lazima tuamini kile kifo chake pale msalabani kama malipo ya dhambi zetu na ufufuo Wake “Haki hii itokayo kwa Mungu hupatikana kwa imani kwa njia ya Yesu Kristo kwa wote wamwaminio. Kwa maana hapo hakuna tofauti,” (Warumi 3:22, KCV).
Kuna wakati katika huduma ya Yesu, ambapo makundi ya watu yalimtelekeza na kujitenga naye wakiwa na tumaini la kupata mwokozi mwingine. Na yesu akawauliza wale Thenashara, ”Je, ninyi nanyi mwataka kuondoka?” (Yohana 6:67, TMP), na Petro akamjibu Yesu kwa usahii kabisa, “Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.” (Yohana 6:68b-69, TMP). Nasi tufananishe imani yetu sawa na Petro kwa kutambua kuwa uzima wa milelewapatikana kwa Kristo pekee.
Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.
English
Je, Yesu ndiye njia ya pekee ya kunifikisha Mbinguni?