Swali
Ina maana gani kwamba Yesu ni rafiki wa wenye dhambi?
Jibu
Ukweli kwamba Yesu ni rafiki wa wenye dhambi inamaanisha kwamba Yeye ni rafiki yetu na anatusubiri sisi kutambua kuwepo kwake na upatikanaji wake. Upendo wa Mungu kwetu ni zaidi ya fikra zetu. Tunapochunguza kufanyika mtu halisi kwake Kristo- kwa kuondoka mbinguni ili kuzaliwa kama mtoto asiyejiweza kusaidia ili kukua na uzoefu wa maisha kati yetu — tunaanza kupata mwanga wa kina cha upendo huo. Tunapoongeza kifo chake cha dhabihu msalabani, tunaona kwamba upendo huo ni wa kushangaza.
Ili kuwa "rafiki wa wenye dhambi," Yesu alijiweka chini na kuishi katika ulimwengu ulioanguka, unaodharauliwa, kwa maana "watu wote wametenda dhambi na wametindikwa utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23). Licha ya hali yetu ya dhambi, Yesu anataka uhusiano nasi.
Maneno "rafiki wa wenye dhambi" hutoka kwenye vifungu sambamba katika Injili. "Yesu akaendelea kusema, 'Basi nitawafananisha watu wa kizazi hiki na kitu gani? Ni kama vijana waliokuwa wamekaa sokoni na kuambiana, kikundi kimoja na kingine: 'Tumewapigieni ngoma lakini hamkucheza! Tumeimba nyimbo za huzuni lakini hamkulia!' Kwa maana Yohana alikuja, akawa anafunga na hakunywa kunywa divai, nanyi mkasema : 'Amepagawa na pepo!' Naye Mwana wa Mtu alikuja akila na kunywa, nanyi mkasema, 'mwangalieni mlafi huyu na mlevi, rafiki ya watoza ushuru na wenye dhambi" "(Luka 7: 31-34; tazama Mathayo 11: 16-19).
Katika kifungu hiki Yesu anaelezea kiwango cha ukosefu wa ukomavu wa kiroho kati ya wale ambao walijiona kuwa "wenye haki" na ambao walikomaa "kiroho." Wao wanaweka msimamo wao juu ya kufuata kwao kwa ibada, sheria, na kuonekana nje badala ya kuelewa kweli ya moyo wa Mungu na uhusiano na Yeye. Wakamshutumu Yesu kwa kujihusisha na watu waliotengwa na "watu wasiokubalika katika jamii", wakimwita "rafiki ya wenye dhambi."
Hadithi ya kondoo waliopotea inaonyesha umuhimu wa waliopotea na walio katika mazingira magumu, wale ambao wamekwenda mbali na mahali pa usalama. Kwa Mungu waliopotea ni muhimu sana kuwa atawatafuta mpaka watakapopatikana na kurejeshwa katika mahala pa usalama. "Siku moja watozaushuru na wenye dhambi wengi walikwenda kumsikiliza Yesu. Mafarisayo na walimu wa sheria wakaanza kunung'unuka: "Mtazameni Mtu huyu! Anawakaribisha wenye dhambi na kula pamoja nao." Yesu akawajibu kwa mfano: "Hivi mmoja wenu akiwa na kondoo mia moja, akigundua kwamba mmoja wao amemoptea, atafanya nini? Atawaacha wale tisini na tisa mbugani na kwendwa kumtafuta yule aliyepotea mpaka ampate "(Luka 15: 1-4).
Yesu alieleza wazi kwamba "alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea" (Luka 19:10). Alikuwa tayari kushirikiana na wale waliokuwa sio wazuri, kulingana na Mafarisayo waliodai ni wenye haki. Lakini ndio wale waliotaka kumsikiliza Kristo, na walikuwa na maana kwa Mungu!
Mathayo 9: 10-13 inaelezea wakati mwingine wakati Yesu alichekwa na viongozi wa kidini kwa sababu ya uhusiano Wake na wenye dhambi. Anawajibu kwa kusema, "Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi" (mstari wa 13).
Katika Luka 4:18, Yesu anukuu Isaya 61: 1-2: " BWANA ,wenyezi Mungi amenijaza roho yake , maana Mwenyezi Mungi ameniweka wakfu, akanituma niwaletee wanaokandamizwa habari njema, niwatibu waliovunjika moyo, niwatangazie mateka kwamba watapata uhuru, na wafungwa kwamba watafunguliwa. Amenituma nitangaze mwaka wake wa neema, na siku ya Mungu wetu kulipiza kisasi, niwafariji wote wanaoomboleza", Yesu hakuwa na kutangamana nao.
Yesu hakukubali dhambi au kushiriki katika tabia za uharibifu za wasiomcha Mungu. Kuwa "rafiki ya wenye dhambi," Yesu alionyesha kwamba "fadhili za Mungu zinalenga kukusababisha kutubu" (Warumi 2: 4). Yesu aliishi maisha kamilifu, isiyo na dhambi na alikuwa na "mamlaka duniani kusamehe dhambi" (Luka 5:24). Kwa sababu hiyo, tuna fursa ya kupata moyo na maisha yaliyobadilika.
Yesu, rafiki yetu, alitangamana na wenye dhambi, si kujiunga na njia zao za dhambi lakini kuwasilisha habari njema kwamba msamaha unapatikana. Wengi wenye dhambi walibadilishwa kwa maneno yake ya uhai-Zakeo akiwa mfano mkuu (Luka 19: 1-10).
Wakati maadui wa Yesu walimwita "rafiki ya wenye dhambi," walisema kana kwamba wanamtusi. Kwa utukufu wake na faida yetu ya milele, Yesu alivumilia mashaka kama hayo na akawa "rafiki aliye karibu zaidi kuliko ndugu" (Methali 18:24).
English
Ina maana gani kwamba Yesu ni rafiki wa wenye dhambi?