settings icon
share icon
Swali

Yesu alikuwa wapi katika siku tatu toka siku ile ya kufa mpaka kufufuka?

Jibu


Petro wa kwanza 3:18-19 inaeleza, “kwa maana kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasiohaki, ili atulete kwa Mungu; mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokuwa kifungoni akawahubiri.”

Petro wa kwanza 3:18-22 inaeleza ushikamano wa kuteswa kwake Kristo (fungu la 18) na kutukuzwa kwake (fungu la 22). Petro ndiye anayefafanua yaliyotokea katikati ya matukio haya mawili. Neno “alihubiri’ katika fungu la 19 lin maana ya kuwa aliwasilisha ujumbe. Yesu aliteswa na kufa msalabani, mwili ukiuawa na roho yake pia kufa kwa kufanywa dhambi. Lakini roho yake ilifufuliwa naye akaikakabidhi Baba. Kulengana na petro, muda huo baada ya kufa mpaka kufufuka Yesu aliwasilisha hali Fulani ya ujumbe kwa “roho waliokuwa kifungoni.”

Bwana wetu aliikabidhi roho yake kwa Baba, akafa na wakati Fulani toka kufa mpaka kufufuka, akatembelea kuzimu alikowasilisha ujumbe kwa viumbe vya kiroho 9 pengine ni malaika waasi tazama yuda 6) waliokuwa na uhusiano na nyakati za kabla gharika la wakati wa Nuhu. Kifungu cha 20 kinafafanua zaidi. Petro hakutuambia kilichoambiwa roho hawa waliokuwa kifungoni lakini haiwezi kuwa ilikuwa habari ya wokovu kwa kuwa malaika hawaokolewi (waebrania 2:16). Pengine ilikuwa ni kutangazwa kwa kushindwa kwa shetani na milki yake (petro wa kwanza 3:22; wakolosai 2:15). Waefeso 4:8-10 pia inajaribu kueleza kuwa Kristo alienda “paradise” (luka 16:20; 23:43) na akawachukua mpaka mbinguni wale waliokuwa wamemuamini kabla kufa kwake.

Biblia haifafanui wazi wazi kilichotendeka ndani ya muda wa siku tatu hizi toka kufa mpaka kufufuka. Haiwezi kueleweka ya kuwa alikuwa ameenda kuwapa watu nafasi ya pili ya kuokolewa kwa kuwa biblia inatuambia ya kuwa tunakutana na hukumu punde tu baada ya kufa(waebrania 9:27).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yesu alikuwa wapi katika siku tatu toka siku ile ya kufa mpaka kufufuka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries