settings icon
share icon
Swali

Je! Ikiwa ushoga ni dhambi, ni kwa nini Yesu hakuutaja jambo hilo kamwe?

Jibu


Wengi wanaounga mkono ndoa za jinsia moja na haki za mashoga wanasema kwamba, kwa kuwa Yesu hakuwahi kutaja ushoga, hakuuona kuwa ni dhambi. Baada ya yote, hoja huwa, ikiwa ushoga ni mbaya, ni kwa nini Yesu hakuuchukulia kuwa suala muhimu?

Kihalisi, ni kweli kuwa Yesu hakuzungumzia ushoga hasa katika simulizi za Injili; hata hivyo, Alizungumza waziwazi kuhusu ujinsia kwa ujumla. Kuhusu ndoa, Yesu alisema, “Akawajibu, “hapo mwanzo Muumba aliwaumba mwanaume na mwanamke, naye akasema, ‘Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, na hao wawili watakuwa mwili mmoja’? Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Mathayo 19:4-6). Hapa Yesu alirejelea waziwazi Adamu na Hawa na kuthibitisha mpango uliokusduwa wa Mungu kwa ajili ya ndoa na ujinsia.

Kwa wale wanaomfuata Yesu, mazoea ya ngono yana mipaka. Badala ya kuwa na maoni yanayoruhusu uasherati na talaka, Yesu alithibitisha kwamba watu wanapaswa kuwa waseja na watawa au kuolewa na kuwa waaminifu kwa mwenzi mmoja wa jinsia tofauti. Yesu aliona usemi mwingine wowote wa kujamiiana kuwa dhambi. Hii inajumuisha matendo ya ngono ya jinsia moja.

Je! pia tunapaswa kuamini kwamba tendo lolote na kila tendo ni jema isipokuwa Yesu alikataze hasa? Lengo la Injili halikuwa kutupatia orodha pana ya matendo ya dhambi, na kuna dhambi nyingi za wazi ambazo Yesu hakuzungumiza hasa. Utekaji nyara, kwa mfano. Yesu hakusema hususan kwamba utekaji nyara ni dhambi, lakini tunajua kwamba kuiba watoto ni kosa. Jambo ni kwamba Yesu hakuhitaji kuorodhesha dhambi, hasa wakati ufunuo zaidi uliomo katika Nyaraka unaondoa mashaka yote kuhusu dhambi ya ushoga.

Maandiko yako wazi kwamba waumini hawapaswi kujihusisha na usherati: “Ikimbieni zinaa. Dhambi zingine zote atendazo mtu ziko nje ya mwili wake, lakini yeye aziniye hutenda dhambi ndani ya mwili wake mwenyewe” (1 Wakorintho 6:18). Uasherati, iwe ni matendo ya ngono ya jinsia moja au vingenevyo, ni dhambi dhidi ya mwili wa mtu mwenyewe.

Ni muhimu kutambua kwamba uasherati, ikiwa ni pamoja na matendo ngono kati ya watu wa jinsia moja, yanaorodheshwa pamoja na dhambi nyinginezo katika Maandiko, kuonyesha kwamba Mungu haorodheshi dhambi moja kuwa mbaya zaidi kuliko zingine. Ingawa matokeo ya dhambi fulani ni makubwa kuliko nyingine, Maandiko mara nyingi huorodhesha dhambi bega kwa bega. Kwa mfano, Yesu alisema, “Kwa maana ndani ya moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushahidi wa uongo na masingizio. Haya ndiyo yamtiayo mtu unajisi” (Mathayo 15:19-20; ona pia Warumi 1:24-31).

Biblia inafundisha kwamba wafuasi wa Yesu wanapaswa kufuata utakatifu wa ngono, na hiyo ni pamoja na kujizuia kutokana na matendo ya ngono ya jinsia moja. Kwa kuongezea, wasioamini wanaofanya ushoga huhitaji wokovu kama mtu mwingine yeyote asiye muumini. Wakristo wanaalikwa kuwaombea wale wasiomjua Kristo, kuwatumikia wengine kwa upendo, na kushiriki ujumbe wa Yesu na watu wote, wakiwemo wale wanaojihusisha na ushoga.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ikiwa ushoga ni dhambi, ni kwa nini Yesu hakuutaja jambo hilo kamwe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries