Swali
Je! Yesu yuko hai hai? Je! Inamaanisha nini kuwa Yesu yuu hai?
Jibu
Alitembe duniani takribani zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Tunasikia juu ya kusulubiwa kwake na mafundisho yake. Pasaka ni kuhusu ufufuo wake. Lakini hapo ndio baadhi ya watu hujikwaa. Je! Hiyo inamaanisha kuwa yuu hai? Itakuwaje mtu ambaye alisulubiwa hadharani kufufuka toka wafu? Historia inatupa Ushahidi usiopingika kwamba Yesu Kristo wa Nazarethi aliishi, lakini je! bado yuu hai hii leo? Wakristo wanaabudu, huimba, na kuomba kwa Yesu kana kwamba yuu hai. Je! Wanakosea kwa kufanya hivyo? Ni katika kiwango gani Yesu yuu "hai"?
Sisi kama wanadamu tuliofungiwa katika dunia, kila mara tunaelewa maisha kuwa yamehuzishwa moja kwa moja kwa – maisha ya mtu ikiwa mwili wake bado uko hai. Lakini maisha in zaidi ya hayo. Ulimwengu wa kiroho ni halisi jinsi eneo la mwili wa ulimwengu ni halisi. Wafilipi 2:5-11 inaeleza kwamba Yesu alikuwapo, kama mmoja na Mungu, kabla ya nchi na sungumziwa na ikawa (linganisha Yohana 1:1-3). Mwana wa milele wa Mungu amekuwa hai nyakati hizi zote. Yesu hawai kosa kuwa hai hata wakti mwili wake ulikuwa umelazwa kaburini.
Yesu alisungumzia maisha yaliyo zaidi ya ulimwengu wa mwili (Yohana 10:10). Aliahidi uzima wa milele kwa kila amwaminiye (Yohana 3:16-18). Alieleza kuwa ufalme ambao alikuja kuuanzisha haukuwa wa ulimwengu huu (Yohana 18:36).
Wakati Mungu alimuumba mwanadamu wa kwanza, "akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai" (Mwanzo 2:7). Uhai huo ulitoka kwa Mungu ambaye ni wa milele. Mungu alipuliza uhai wake mwenyewe kwa mtu, na hiyo ndio sababu maisha ya mwanadamu si kama ile ya majani na Wanyama. Wanadamu wana roho ambayo itaishi milele kama vile Mungu ataishi milele. Mwili wa nyama utakufa, lakini hata hivyo utafufuliwa tena. Wakati Yesu alikufa msalabani, mwili wake hakika ulikufa na ukazikwa, lakini roho yake ilikuwa mahali kwingineko ikiwa hai na salama. Alikwisha iweka roho yake mikononi mwa Baba yake (Luka 23:46).
Wakati Mungu alimfufua Yesu kutoka wafu, roho yake iliungana na mwili wake, ambayo sasa ulikuwa mwili uliojawa utukufu (Wafilipi 3:21). Paulo aliandika kuwa zaidi ya watu mia tano walimwona Yesu baada ya kufufuka (1 Wakorintho 15:6). Agano Jipya liliandikwa na mashahidi ambao walikuwa wamejionea wenyewe kuwa Yesu hakika alikuwa hai na alikuwa na mwili.
Yesu bado yuu hai hii leo. Alifufuka kimwili kutoka kwa wafu na akapaa kwenda mbinguni. Matendo 1 inanakili jinsi siku arobaini baada ya ufufuo zilikuwa, wanafunzi wa Yesu walikuwa Naye kwa ghafula wakati alianza kupaa angani. Walimtizama kwa mshangao alipozidi kupaa na kutoweka machoni mwao (Matendo 1:9-11). Yesu alikuwa ametabiri kuwa atarudi kwa Babaye, na hivyo ndivyo alifanya (Yohana 14:1-2; Yohana 20:17).
Yesu yuu hai mbinguni pamoja na Mungu, malaika na wale wote ambao wamemwamini Yeye kwa wokovu (2 Wakorintho 5:8). Ameketi katika mkono wa kuume wa Baba (Wakolosai 3:1), "aliyepaa juu ya mbingu zote" (Waefeso 4:10). "Anaishi kwa kuwaombea" wafuasi wake duaniani (Waebrania 7:25). Na aliahidi kuwa atarudi tena (Yohana 14:1-2).
Kama vile roho ya Yesu haikufa, vile vile roho zetu hazitakufa (Yohana 11:25-26). Tutaishi milele mahali. Namna tunayoitikia fursa ya Mungu ya wokovu itaamua hatima yetu (Yohana 3:16-18). Yesu aliwambia wanafunzi wake, "kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai" (Yohana 14:19). Juu ya tumaini hilo tunaweza kujenga maisha yetu, tukijua kwamba kama Bwana wetu Yesu, tunaweza kufa, lakini kifo sio mwisho.
English
Je! Yesu yuko hai hai? Je! Inamaanisha nini kuwa Yesu yuu hai?