settings icon
share icon
Swali

Je! Yesu yuko?

Jibu


Yesu ni nafsi halisi. Yeye ni mmoja wa watu mashuhuri wamesungumziwa na kuogopwa katika historia. Wasomi wengi, Wakristo na wale wasio Wakristo na makafiri wanaamini kuwa kulikuwa na Yesu wa historia. Ushahidi ni mwingi. Wanahistoria wa kale waliandika juu ya Yesu, wakiwa ni pamoja na Josephus na Tacitus. Kutoka kwa mtizamo wa kihistoria, hakuna swali ngumu: kwa kweli kulikuwa na mtu aliyeitwa Yesu ambaye aliishi katika karne ya kwanza Israeli.

Agano la Kale lilitabiri juu ya Masia, mtu halisi ambaye angekomboa Israeli kutoka kwa maadui zake. Masia alikuwa azaliwe Bethlehemu (Mika 5:2), katika kabila la Daudi (Mwanzo 49:10). Alikuwa awe nabii sawia na Musa (Kumbukumbu (18:18), mhubiri wa habari njema (Isaya 61:1), na mponyaji wa magonjwa (Isaya 35:5-6). Masiha atakuwa atakuwa mtumishi wa Mungu ambaye aliteseka kabla aingie katika katika utukuf Wake (Isaya 53). Yesu ni nafsi halisi ambaye alitimiza nabii hizo.

Agano jipya ina mamia ya marejeleo ya Yesu Kristo kama nafsi halisi. Injili ya kwanza huenda iliandikwa miaka kumi ya kufa kwa Yesu, na nyaraka za mapema za Paulo ziliandikwa miaka 25 baada ya kifo cha Yesu. Hii ni muhimu kwa sababu inamaanisha kwamba, injili ilipokuwa inasambaa, kuliwa na umati wa mashahidi ambao walikuwa hai ambao wangethibidhisha ukweli wa matukio ya injili.

mwandiko wa uthibitisho wa ukweli wa Agao Jipya ni mkubwa sana: kunazo takribani nyaraka 25,000 za Agano Jipya. Kwa ulinganisho Gallic Wars iliyoandikwa naye Kaisari katika karne ya kwanza kabla Yesu azaliwe ina nyaraka 10 bado singali-na ya mapema mno kati ya hizo iliandikwa miaka 1,000 baada ya ile halisi. Vile vile, Shairi lake Aristotle lina mwandiko tano wa kwanza bado ungaliko, ukikadiriwa kuandikwa mwaka wa 1,400 baada ya ile asili. Wale wanao tia shaka kuwa Yesu si nafsi halisi lazima wanaswali kuwepo kwake Julius Kasairi na Aristotle.

Nje ya Biblia, Yesu ametajwa katika Kurani na katika maandishi ya Kiyahudi, Aginostiki na Uhindu. Wanahistoria wa kwanza walimchukulia Yesu kuwa nafsi halisi. Mwanahistoria wa karne ya kwanza Tacitus aliwataja wafuasi wa Kristo. Flavius Josephus, mwanahistoria wa anamrejelea Kristo katika uandishi wake wa Uyahudi wa kale. Marejeleo mengine kwa Yesu yanaonekana katika Suetonius, katibu mkuu wa mfalme Hadriani; Julius Africanus, akimnukuu mwanahistoria Thallus; Lucian wa Samosata mwandishi wa Kigiriki wa karne ya pili; Pliny mdogo; na Mara Bar-Serapion.

Hakuna mwanahistoria yeyote ambaye amekuwa na ushawishi katika ulimwengu huu kama Yesu Kristo. Haijalishi ikiwa mtu anatumia KK (Kabra ya Kristo) au KKP (Kabra ya kipindi cha Pamoja), katika kuhesabu miaka kwa nchi za magaribi, hesabu hiyo utokana na matukio: kuzaliwa kwake Yesu, nafsi halisi. Kwa jina la Yesu boma za wato Yatima, hosipitali, zahanati, ma shule, vio vikuu, makao ya wasio na nyumba, mashirka ya dharura na mashirika mengine ya kusaidia. Mamilioni ya watu wanaweza kutoa shuhuda binafsi za kazi ya Yesu katika maisha yao.

Kuna Ushahidi mwingi unaonyesha kuwa Yesu ni nafsi halisi, katika historia ya kawaida na ile ya biblia. Pengine Ushahidi mkuu wa kuwepo kwake Yesu na kwamba alitenda chenye Biblia inasema kuwa alifanya ni ushahidi wa kanisa la kwanza. Kiuhalisia maelfu ya Wakristo katika karne ya kwanza, ikiwa ni pamoja na wanafunzi kumi na wawili, walikuwa tayari kuyatoa maisha yao kuikufia injili ya Yesu Kristo. Watu watakufia kile wanachokiamini kuwa kweli, lakini hakuna mtu anaweza kufia kile wanajua ni uwongo.

Tumeitwa kuwa na imani-sio imani pofu ambayo ni ile unafanywa kuamini-lakini Imani ya kweli kwa mtu ambaye amewai ishi mahli panapojulikana katika historia. Huyu mtu ambaye alithibidhisha uasili wake kupitia ishara alizosifanya na unabii alioutimiza, alikufa juu ya msalaba wa Kirumi, alizikwa kwa kaburi ya Kiyahudi, na akafufuka tuthibidhishwe kuwa haki. Yesu yuko. "Heri yao wale ambao hawajaona, lakini wameamini" (Yohana 20:29).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Yesu yuko?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries