settings icon
share icon
Swali

Agnostiki ni nini?

Jibu


Agnostiki ni mtazamo kuwa uwepo wa Mungu si kitu kisichoweza kujulikana au kuthibitishwa. Neno “agnostiki” kimsingi lamaanisha “bila elimu/maarifa.” Uagnostiki ni mtindo wa ukanaji Mungu. Ukanaji Mungu kuwa Mungu haishi- msimamo ambao hauwezi kuthibitishwa. Ukanaji Mungu wapinga kwamba uwepo wa Mungu hauwezi thibitishwa au siothibitishwa, kuwa kamwe hauwezi kujua kuwa kuna Mungu au hayupo. Katika hali hii, ukanaji Mungu huu uu kweli. Uwepo wa Mungu hauwezi kuthibitishwa au kukanwa kwa kubahatisha.

Bibilia inatuambia ya kwamba lazima tukubali kwa imani kuwa Mungu yupo. Waebrania 11:6 yasema bila imani “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendaza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamfuatao.” Mungu ni roho (Yohana 4:24 kwa hivyo hawezi oonekana au kuguzika. Ila tu Mungu aamue kujidhihirisha Yeye mwenyewe, katika hisia zetu hawezi kuonekana (Warumi 1: 20). Bibilia yatangaza kwamba uwepo wa Mungu unaweza oonekana vizuri sana katika ulimwengu (Zaburi 19:1-4), inayohisika katika masingira (Warumi 1:18-22), na umethibitishwa katika mioyo yetu (Mhubiri 3:11).

Waagnostiki/wamkanao Mungu hawako tayari kufanya uamuzi kukubali kuwa Mungu yupo au hayupo. Ni upeo wa msimamo wa “kufanya mwanya katika ua.” Wasiomwamini Mungu pia wanaamini kuwa Mungu anaishi. Wasiomwamini Mungu wanaamini kuwa Mungu haishi. Waagnostiki wanaamini kwamba tusiamini au tukose kuamini kuwepo kwake Mungu, kwa sababu ni vigumu mno kutambua kama Mungu yupo au hayupo.

Kwa ajili ya pingamizi, hebu tuweze kuleta wazi ushaidi usioweza kukanwa wa uwepo wake Mungu. Ikiwa tutauweka msimamo wa wamkanao Mungu na waagnostiki katika kiwango sawa, ambao waleta “maana” sana kuamini kuambatana na uwezekano wa maisha baada ya kifo? Kuma kuna Mungu, wasiomwamini Mungu na waagnostiki wote sawa wataisha kuwepo wakati wamekufa. Kama kuna Mungu, wote wasiomwamini Mungu na waagnostiki watakuwa na mtu wa kuwajibikia pindi tu wanapokufa. Kutoka kwa mtazamo huu, ni wazi kuwa afadhali kuwa asiyemwamini Mungu kuliko kuwa agnostiki. Kama msimamo wowote unaweza thibitishwa au usiweze, yaonekana busara kuwa kufanya juhudi zote kuunguza msimamo ambao hauna mwisho na milele yote matunda yake ni ya kuthamanika

Ni kawaida kuwa na shuku. Kuna vitu vingi katika dunia hii ambavyo hatuvielewi. Kila mara, watu wanashuku kuwepo kwa Mungu kwa sababu hawaelewi au kukubaliana na mambo ayafanyayo na kuyaruhusu. Ingawa, kama mwanadamu tuliye na hatima, tusitarajie kuweza kumfahamu Mungu asiye na mwisho. Warumi 11: 33-34 yasema, “Jinsi silivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake: hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani! Maana ni nani aliyeijua nia ya Mwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake?” lazima tumwamini Mungu na kumtumainia katika imani. Mungu ako karibu na tayari kujidhihirisha kwa njia za kustaajabisha kwa wale watakao mwamini. Kumbukumbu La Torati 4:29 yasema, “Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako utampta, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.”

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Agnostiki ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries